Wasanii wanaoongoza kuzitambulisha sehemu walikotoka/wanakoishi

vampire_hunter007

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2015
Posts
1,034
Reaction score
2,624
Imekuwa mara nyingi watu wa jamii fulani wakijisifia pale mtu kutoka jamii yao anapokuwa maarufu kwa usanii au mengineyo....But sio wasanii wote walioweza kuzitambulisha sehemu wanazotoka....Wapo waliozitambulisha sehemu/Mitaa wanayoishi na wapo wale waliotambulisha sehemu walikozaliwa....Kwa haraka haraka wasanii ninaowakumbuka waliotambulisha sana maeneo yao ni hawa...

1. Juma Nature na Wanaume TMK - Temeke
Hawa jamaa walifanya temeke ijulikane Tanzania nzima...Kiasi watu wengi wa mikoani waliifahamu Temeke huku wengine wakiwa hata hawajui wilaya za mikoa yao....Jamaa waliwakilisha sana Temeke...

2. Crazy GK na East Coast - Upanga
Hawa nao walijitahidi kuitambulisha Upanga. Japo hawakufikia level ya TMK...Na watu wazima wenangu watakuwa wanakumbuka ushindani uliokuwepo baina ya makundi haya mawili...

3. Diamond Platnumz - Tandale
Dah jamaa kaiwakilisha sana Tandale...Mpaka nje ya Tanzania wanaijua Tandale... Baadhi ya wakenya huko wanadhani Tandale ni bonge la sehemuuuu........

4. Mangwea na Chamber Squad - Dom
Jamaa hawa nao waliipaisha Dodoma kimtindo...

5. Shilole - Igunga
Bibie naye hayupo nyumba kuiwakilisha Igunga..Huenda akizidisha vituko Igunga itakuwa maarufu sana siku zijazo....

6. Joh Makini na Weusi - A-town
Haya machalii ya Arusha nayo yanawakilisha vema pande zile....A-town imekuwa ikitrend sana haswa kama mji wa hip hop flani hivi....Wanajitahidi

7. Wagosi wa Kaya - Tanga
Wimbo maarufu wa Tanga kunani na lafudhi zao ziliifanya Tanga pia kujulikana kuwa kuna wasanii...Sijui siku hizi wapo wapi hawa jamaa....Huenda muda umewatupa mkono

8. Afande Sele na Stamina Sharo Bweeenz - Moro
Jamaa nae wameiwakilisha sana Moro town...

9. Fid Q aka Ngosha - Mwanza
Dah huyu jamaa sijui nilimsahau vipi....Ameweza sana

Kwa haraka haraka nnaowakumbuka ni hao...Wewe unadhani ni nani amewakilisha kitaa chake/ home town yake vya kutosha na kuifanya ikajulikana ....Karibuni
 
haaa, hapo anaongoza izzo biznes na weuc tu, hao wengne wanajaribu jaribu tu
 
Me nadhani wa kwanza anatakiwa awe

1. Wagosi wa kaya Tanga
2. Juma nature Temeke
3. Nako2Nako Joh Makini Weusi Arusha
4. Fid Q Mwanza
5. Chid Benz Ilala
6.Afande Sele Morogoro
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…