Marta journalist
New Member
- Jul 18, 2022
- 2
- 1
Nchini Tanzania ukiwazungumzia vijana asilimia kubwa utawakuta kwenye sekta ya utamaduni, sanaa na michezo, wengi wanashiriki katika michezo, muziki, maigizo, ucheshi na sanaa nyingine hali inayochangia ukuaji wa kasi wa sekta hii.
Kwa mwaka 2023, sekta ya sanaa imekuwa kwa asilimia 17.7% , kwa mujibu wa taarifa ya hali ya Uchumi kwa mwaka 2023 na mpango wa maendeleo wa taifa wa mwaka 2024-2025 iliyotolewa na wizara ya mipango na uwekezaji.
Lakini pia hadi mwaka huu 2024 tumeendelea kushuhudia ukuaji wa kasi wa sekta ya utamaduni, sanaa na michezo ambapo wachezaji na wasanii wetu wanaiwakilisha vyema Tanzania ndani na nje ya nchi.
Andiko hili linawazungumzia wasanii wa muziki ambao wanasikilizwa na kutazamwa na watanzania wengi kuanzia kundi la watoto hadi watu wazima, na pia muziki unabeba asilimia kubwa ya maudhui yanayorushwa kwenye vyombo vya habari kama redio na televisheni.
Kwasasa si ajabu kukutana na mtoto wa shule ya msingi akiimba, kucheza au kutazama wimbo fulani hasa bongo fleva, japo si vibaya lakini baadhi ya maudhui ya nyimbo wanazosikiliza na kutazama ni kinyume na maadili ya Mtanzania.
Maudhui ya muziki wa baadhi ya wasanii yanachangia kuporomosha maadili ya watoto na vijana wanaowatazama kama mfano wa kujifunza utungaji na uandaaji wa sanaa bunifu.
Kwamaana hiyo wanakwenda kinyume na muongozo wa uzingatiaji maadili katika kazi za sanaa kifungu cha 4 cha sheria ya Baraza la Sanaa la Taifa, sura ya 204 ambacho kimetaja mambo ya kimaadili wanayotakiwa kuzingatiwa wakati wa kuandaa kazi za sanaa, ikiwemo kutohudhurisha lugha chafu au matusi na kutoshawishi wala kuhamasisha vitendo vya ngono, ushoga, usagaji, ulawiti na matumizi ya dawa za kulevya.
Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) katika kusimamia muongozo huo imekuwa ikiwasimamisha kwa muda baadhi ya wasanii wasiozingatia, kuzifungia nyimbo za sauti pekee na za picha jongefu (video) na kuwatoza faini ili kulinda maadili na utamaduni wa kitanzania.
Novemba 4, 2023 BASATA ilimfungia msanii Oscar John Lelo (Whozu) kufanya kazi za sanaa kwa miezi sita baada ya kuchapisha video ya wimbo “ameyatimba” wenye maudhui yanayokiuka kanuni za maadili ikiwemo matusi, vitendo vya unyanyasaji, ukatili na udhalilishaji wa utu wa mwanamke na kumtoza faini ya shilingi milioni tatu.
Pia wasanii “Mbosso” na “Billnass” walitozwa faini ya shilingi Milioni 3 kila mmoja na kufungiwa kutojihusisha na kazi za sanaa kwa muda wa miezi mitatu kwa kushirikishwa katika wimbo huo.
Tumeshuhudia pia baadhi ya wasanii wakiimba kwa kusifia utumiaji wa vilevi kama pombe mfano wimbo wa msanii ‘Marioo- Bia tamu” na nyingine zikihusu mahusiano, huku picha jongefu (video) za baadhi ya nyimbo zao zikiwa na mavazi na maudhui yasiyofaa kutazamwa na kila kundi la umri katika jamii hasa watoto.
Licha ya uwepo wa baadhi ya wasanii wanaotoa nyimbo kwa kuzingatia maadili, lakini vyombo vya habari nchini havitoi nafasi stahiki kwa kucheza nyimbo hizo ili wawe mfano mzuri wa kuleta mabadiliko chanya katika sanaa ya muziki.
Kwa upande wa wasanii je, baadhi ya nyimbo wanazoimba wangetamani kizazi kijacho au hata watoto wao waziimbe na kuzitazama? Ni vema wakafikiria hilo kabla ya kutoa nyimbo zao.
Nini kifanyike?
Wasanii wa muziki watambue kwamba wao ni kioo na wanatazamwa na jamii kupitia muziki wao unaopigwa sehemu mbalimbali hivyo ubunifu wao ujikite kwenye kujenga jamii bora na kuhamasisha mabadiliko chanya.
Wazalishaji wa muziki na waongozaji wasitumbukie kwenye wimbi la utamaduni wa nchi za magharibi kwa kisingizio cha biashara bali watengeneze maudhui yanayowahusu watanzania na afrika kwa ujumla ili wawe walinzi na sehemu ya usambazaji wa utamaduni wetu.
Ili kuepuka kuwa daraja la kusambaza maadili yasiyofaa kwa jamii, vyombo vya habari visitazame umaarufu wa msanii anayetoa wimbo bali wazingatie maudhui yaliyomo katika wimbo husika, muda wa kurusha maudhui ya wimbo kwa kuzingatia aina ya kipindi na kundi lengwa la msikilizaji au mtazamaji.
Wizara ya utamaduni, sanaa na michezo kupitia Baraza la Sanaa la Taifa waendelee kufuatilia kwa ukaribu sanaa za wasanii na kutoa adhabu kulingana na sheria zilizopo ili kuwepo na msisitizo katika ubunifu sahihi na salama kwa jamii ya kitanzania.
Aidha BASATA kwa kushirikiana na Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) wanatakiwa kuchuja maudhui ya wimbo wa msanii na matumizi ya lugha sahihi, bunifu na inayoishi kabla ya kuwafikia wanajamii, ili kuepuka kuruhusu nyimbo zinazohamasisha vitendo visivyofaa katika jamii.
Vyombo vya habari vitakavyobainika kurusha maudhui kinzani na maadili ya kitanzania na Afrika kwa ujumla kutoka kwa wasanii wa nchi za nje, viwajibishwe na mamlaka ya mawasiliano Tanzania kwa mujibu wa sheria na miongozo.
Mwisho.
Usimamizi wa maadili utasaidia kujenga Tanzania ambayo sanaa itaheshimiwa, itaheshimisha nchi na itakuwa na watu makini watakaotumia sanaa yao kuibadilisha jamii kutoka kwenye mambo hasi kwenda chanya, isiyojikita kwenye kuburudisha pekee bali pia kuelimisha jamii.
Pia kutasaidia kutengeneza Tanzania ambayo watoto wetu na watanzania kwa ujumla watakuwa wenye maadili na kuzingatia, kuutetea, kuutunza na kuusambaza utamaduni wao.
Sanaa ni ubunifu, hivyo wasanii watumie ubunifu wao vizuri ili wawe kioo kwa kuhamasisha mabadiliko chanya katika jamii.

Upvote
4