Wasanii wengi sana waitwa Dodoma mkutano wa CCM

Wasanii wengi sana waitwa Dodoma mkutano wa CCM

Muite

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2013
Posts
2,971
Reaction score
6,607
Hakika CCM ni chama kubwa sana.

Lakini ninawaza tu kuwa:
1. Bila wasanii ni wazi kikao kingefanyika
2. Bila wasanii wengi CCM kwa ukubwa wake itashinda tu kwenye uchaguzi wa mwaka huu tena kwa kishindo kikubwa tu.

Gharama za wasanii:
1. Usafiri
2. Malazi
3. Chakula
4. Posho

Ninajua hizo ni hela za chama , lakini ingekuwa ni uzalendo mkubwa sana kama chama kinaona kina fedha nyingi kingesema kizielekeze hata kwa baadhi ya huduma zenye changamoto kubwa. Magufuli aliwahi kuelekeza fedha za maadhimisho ya sherehe za uhuru zikajenga barabara ya Mwenge to Morocco (ule ni uzalendo mkubwa sana).

Mitaani kuna barabara za vumbi nyingi tu na hazitengenezwi sababu hakuna fedha, nafikiria kuliko kutumia Gharama kubwa kwenye mikutano kwanini fedha zisielekezwe hata kujenga barabara ya km 2 au 5 tu( fedha ya kuwalipa wasanii wa muziki, Bongo move , wachekeshaji na kina mwijaku).
Chama kingebaki na vikundi vyake vya TOT kama zamani kipindi cha Nyerere, Mwinyi, mkapa.

Naipenda sana nchi yangu, naiheshimu sana CCM kwasababu ni chama kilicholiunganisha taifa na kuwa nchi ya amani na siku zote nawakubali viongozi wetu. Sema tu ninachoamini kuna watendaji na washauri ndani ya chama na serikali ambao sio wazuri kabisa na mengi wanayafanya either kwasababu ya uelewa mdogo, kukosa uzalendo au KWA MASLAHI BINAFSI
 
Back
Top Bottom