Vien
JF-Expert Member
- Mar 6, 2020
- 8,508
- 15,276
Kwa upande wa Hip Hop, imekuwa ni kawaida sana kukuta msanii ana zaidi ya miaka 20 kwenye game, lakini ukichunguza vizuri utakuta ngoma iliyompa heshima ndiyo ileile iliyomtoa kwenye game. Baada ya hapo hajawahi tena kutengeneza ngoma iliyofikia kiwango kilekile.
Yaani unakuta msanii kila akienda kwenye show, interview au akitajwa kwenye mijadala ya Hip Hop, kinachowafanya watu wamtambue ni ile ngoma moja au mbili alizotoa zamani. Kazi nyingine zote zilizofuata zimekuwa za kawaida (average) kiasi kwamba hazikuacha impact ya kudumu.
Naomba nieleweke mapema, hapa nazungumzia solo projects, si nyimbo za makundi wala collaborations.
Twende kwenye mifano, ndiyo tutaelewana vizuri.
Nikki Mbishi
Huyu jamaa ana albums kama saba hivi sasa. Lakini cha kushangaza, nyimbo zinazozungumziwa kila siku ni zilezile:
• Playboy
• Sauti ya Jogoo
• Nyakati za Mashaka
• Kila Wakati
Hizi ni nyimbo za zaidi ya miaka 10 iliyopita. Tangu hapo ametoa kazi nyingi, lakini hakuna iliyoweza kufikia impact ya nyimbo hizo. Matokeo yake, hizo ndizo zimeendelea kumtambulisha mpaka leo.
Kalapina
Kwa upande wa solo projects, Mstari wa Mbele ndiyo kazi yake inayobaki kuwa benchmark. Baada ya hapo ametoa nyimbo nyingine nyingi, lakini hakuna iliyofikia uzito wa wimbo huo, wakati ana zaidi ya miaka 20 kwenye game.
Rado
Usiulize ndiyo project inayomtambulisha zaidi mpaka leo. Ana nyimbo nyingi, lakini ukiwatazama mashabiki wengi, wakimtaja Rado wanaanza na huu wimbo.
Soggy Dogg
Kibanda cha Simu ndiyo wimbo unaomtambulisha zaidi. Nyimbo nyingine zilikuja, lakini hazikuacha impact ya kiwango hicho.
Jafarai
Nipo Bize ndiyo wimbo uliobeba jina lake. Mpaka leo ndiyo kazi ambayo watu wengi wanamkumbuka nayo.
Oten
Hebu Nicheki ndiyo project yake yenye impact kubwa zaidi. Baada ya hapo hakukuwa na wimbo ulioweza kufikia kiwango hicho.
P One Black
• Nini Mnataka
• Nisikilize Mimi
Hizi ndizo nyimbo zinazobeba jina lake mpaka leo.
Chid Benz
• Dar es Salaam Stand Up
• Raha za Dunia
Hizi ndizo nyimbo ambazo zimeendelea kumtambulisha zaidi kuliko kazi zake nyingine za solo.
M.H. Temba
• Nampenda Yeye
• Amekoma
Mpaka leo, hizi ndizo nyimbo ambazo watu wengi wanazitaja wakimtaja M.H. Temba.
Noorah (Baba Style)
Ice Cream ndiyo wimbo ambao umebaki kuwa alama yake kubwa zaidi.
Hawa ni baadhi tu ya wasanii walionijia kichwani.
Jambo la kushangaza ni kwamba msanii anaweza kuwa na miaka zaidi ya 20 kwenye industry, albums nyingi na nyimbo nyingi, lakini mwisho wa siku atambulike kwa nyimbo mbili au tatu tu alizotoa mwanzoni mwa career yake.