Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 1,831
- 5,489
Ukisikiliza nyimbo za kihaya na Design yake ya uchezaji, vikitumika vizuri tunapeleka Bongofleva kwenye Grammy.
Grammy wanapenda vitu asilia, na sio vya ku-copy. Ukisikiliza hii nyimbo ya Mwanamama "Sauda Haulat - Dereva Babili" ni nyimbo iliyotoka miaka ya 2000 mwanzoni lakini ingefanyiwa Mastering na Mixing vizuri ni nyimbo moja ambayo inachezeka Club, Harusini, na kila mahali.
Ukisikiliza huo wimbo vizuri inapigwa ngoma "Drum" moja kali inayoleta msisimko wa kukushawishi kucheza. Achilia mbali maneno yanayoimbwa uenda ukawa huyaelewi, ila beat yani instrument na melody ni vitu vya kiasilia na vyenye kumfanya mtu ambaye hata huelewi lugha aweze kutaka kuucheza wimbo huu ukizingatia na namna ya uchezaji wa Wahaya basi nyimbo ndio inazidi kukukosha.
Miaka ya Nyumba Diamond Platnumz na Rayvanny waliamua kuufanyia sampling wimbo wa "Salome" wa Saida Karoli, na ukaenda Global na kupendwa na watu wengi. Saida Karoli ni moja ya wasanii waliopaisha sana mziki wa asili wa Tanzania barani Afrika.
Mimi niliwasiliana na Rafiki yangu mmoja wa Zambia kupitia Facebook tukawa tunaulizana vitu kadha wa kadha, nikashangaa alivyoniuliza na kunitajia nyimbo za Saida Karoli na akasema zilikuwa zinapigwa huko Zambia enzi hizo.
Anadai nyimbo hizo za kihaya zilikuwa na mdundo ambao hakukwepeki kucheza hasa za Saida Karoli na namna ya uchezaji
Wasanii wetu wanashindwa kufika Kimataifa kwa sababu wanacopy sana vya watu mfano Afrobeat na Amapiano, soukus, zhuku, Rumba.... Ambazo kiasilia sio identity yetu, kwenye nomination za grammy uwezi msanii wa Tanzania uwezi kutajwa kwa sababu hakuna mziki wetu.
Wasanii wetu wote waanze kujikita kufanya sampling ya muziki yetu ya Asilia, na ile ya kizazi kipya unayozalishwa hapa hapa Tanzania mfano Singeli, kama kweli wanataka kuwa na Identity ya Tanzania Kimataifa.