Huu ndiyo ukweli, Alikiba ameshinda Tuzo nyingi sana mwaka 2016, Wapinzani hawajakubali kabisa au hawajaamini kama jamaa anadeserve.. Mara waseme analilia Tuzo, Mara za Mchangani, Mara hastahili, Mara wengine EATV AWARDS hawakushiriki kwa vile za kujiandikisha, Mara Ben Pol alistahili!
Kama umewahi kusoma hesabu za probability: Ni kwamba kuwa tu nominee katika Awards inamaanisha wewe una nafasi sawa ya kushinda, ishu ni nani ana vigezo zaidi! Kwa hiyo kama ALIKIBA alishinda Tuzo MTVEMA, BEFFTA, WANAcorp, SOUNDCITYMVP, ASFA n.k na bado amepata nafasi ya kuperfom MTV MAMA, KENYA NA CHRISS BROWN, UGANDA, NIGERIA. HUwezi kufanikiwa siku moja! Yaani huyo huyo Alikiba ametoa Collabo na Sauti sol, Ommy, mziwanda, Baraka, Blue, Mauzo na Bado ana Mengine ya kumstress! Ifike kipindi anayeshinda tumheshimu.
swali la kujiuliza ukimtoa Alikiba, Vanessa na Diamond kwa 2016, Ni Msanii gani ambaye wewe unadhani anastahili kupata Tuzo za kimataifa??????
Issue siyo kwamba jamaa wanataka kutangaza Tuzo zao, hapana ni kawaida kabisa! Sema unayemfahamu toka mdogo huwezi kumthamini kama yule aliyemjua akiwa staa.
kwa kifupi Tujitahidi kusapoti wasanii wetu wote