Wasanii wetu, oneni umuhimu wa kuacha angalau mtoto pindi mtakapoaga dunia

Wasanii wetu, oneni umuhimu wa kuacha angalau mtoto pindi mtakapoaga dunia

hawa maboya hawajielewi mtoto ni muhimu sana,Nafkiri baadhi yao watakua wagumba wengine tasa kama "M.wema"

LIKE Niku ADD
 
Last edited by a moderator:
Bora ya Zari bosslady...kafanya kweli...wasichana wa tz wanacheza cheza tu na wanaume yeye kaja na kufanya kweli....kazi wanayo
 
Ni mifano mingi tumeona pindi msanii au mtu yoyote yule ambaye amefikia umri wa kuanzisha familia inapotokea amefariki bila hata ya kuacha angalau mtoto mmoja ambaye atakua faraja kwa familia au jamii kwa ujumla.

Nimeamua kusema hivi kwa sababu nimetoka kusikiliza historia ya marehemu MEZ B, R.I.P ikisomwa leo wakati amezikwa sikusikia kuwa marehemu alianzisha familia yake achilia mbali hata mtoto tu. Kweli inaumiza ukizingatia marehemu alivuka miaka 30 na zaidi.

Sio tu Mez-b pia na Ngwear pia R.I.P bila kusahau Kanumba R.I.P pamoja na wengine wengi. Tujifunze jaman inaleta faraja kwa familia pindi wakimwona mtoto alieachwa na marehemu.

wazae wazeeke?? according to wema sepetu
 
Eti ni bora mtu aache mtoto ili aifurahishe jamii yake, bila kujali huyo atalelewaje pindi mzazi akifariki bila kumjengea mwanae misingi mizuri! 😞😞 No wonder watoto wa mtaani kuwa janga la kitaifa Tz!
 
Wakiwaacha watt nani atawalea? Jamii imebadilika asee.. haikotayari kulea mtt wa mtu.. au unataka idadi ya wtt wa mtaani iongezeke?
 
Alieleta wazo ka kutumia fake Id adumu maana tungekuwa tunachekana hata kupigana pia.
 
Ni mifano mingi tumeona pindi msanii au mtu yeyote yule ambaye amefikia umri wa kuanzisha familia inapotokea amefariki bila hata ya kuacha angalau mtoto mmoja ambaye atakuwa faraja kwa familia au jamii kwa ujumla.

Nimeamua kusema hivi kwa sababu nimetoka kusikiliza historia ya marehemu MEZ B, R.I.P ikisomwa leo wakati amezikwa sikusikia kuwa marehemu alianzisha familia yake achilia mbali hata mtoto tu. Kweli inaumiza ukizingatia marehemu alivuka miaka 30 na zaidi.

Sio tu Mez-b pia na Ngwear pia R.I.P bila kusahau Kanumba R.I.P pamoja na wengine wengi. Tujifunze jamani inaleta faraja kwa familia pindi wakimwona mtoto alieachwa na marehemu.

Mkuu hakuna sababu ya kuzaa mtoto kama hujapanga kupata wala humtaki akaja kuishia kulaumu maisha yake yote kwa kumtelekeza
 
fikiria aftermath ya huyo mtoto mkuu...siku hizi utu haupo kulea mwana wa mwingine..mbaya zaid wasanii wengi wana majina hevi kuliko wanavyovimiliki..hawaachi cha kusapoti waliobaki..na hata kama wataacha chochote ndugu watadhulum..matata mazito kwa dogo yatima..ni hayo tu.
 
Wakiwaacha watt nani atawalea? Jamii imebadilika asee.. haikotayari kulea mtt wa mtu.. au unataka idadi ya wtt wa mtaani iongezeke?

Ha ha ha ha!!Kwahyo nawewe usizae, maana ukiacha mtoto nani atamlea?
 
Ni mifano mingi tumeona pindi msanii au mtu yeyote yule ambaye amefikia umri wa kuanzisha familia inapotokea amefariki bila hata ya kuacha angalau mtoto mmoja ambaye atakuwa faraja kwa familia au jamii kwa ujumla.

Nimeamua kusema hivi kwa sababu nimetoka kusikiliza historia ya marehemu MEZ B, R.I.P ikisomwa leo wakati amezikwa sikusikia kuwa marehemu alianzisha familia yake achilia mbali hata mtoto tu. Kweli inaumiza ukizingatia marehemu alivuka miaka 30 na zaidi.

Sio tu Mez-b pia na Ngwear pia R.I.P bila kusahau Kanumba R.I.P pamoja na wengine wengi. Tujifunze jamani inaleta faraja kwa familia pindi wakimwona mtoto alieachwa na marehemu.

Wengine hawana uwezo wa kuzaa ,siyo kila mwanaume ana uwezo wa kutia mwanamke mimba na siyo kila mwanamke ana uwezo wa kushika mimba uko hapo kijana
 
Nadhani mngetumia nguvu na muda mwingi kuhimiza uhifadhi wa mazingira badala ya kuhimiza kuzaa tuuu.

My friend Ally k ana watoto kadhaa....sina haja ya kumdisrespect ila nashawika kuhoji kama tumewahi kujiuliza ni dunia gani haswa tuliyo/tunayomuandalia mtoto/watoto kila pale tunaposhangilia kwa kufungua champagne kusheherekea ujio wao ?

ifike mahali kila unapopata mtoto umuangalie na kulia machozi kwa kuwa dunia unayomuachia haina tena uhai....

Tumeiangamiza dunia kwa akili zetu "kubwa"...akili za kuona pesa ndio suluhisho la kila kitu na sio mazingira yetu wenyewe.

Sina takwimu za kitafiti ila naamini asilimia tisini kama sio tisini na tisa ya mito yote tuliyonayo Tanzania imekauka kabisa au kubaki na maji kidogo sana na kwa msimu wa mvua pekee.

Hivi mmewahi kujiuliza ni dunia gani tutakuwa nayo miaka hamsini ijayo bila ya mito/maji ? hivi mmewahi kujiuliza ni nini kinafuatia baada ya mito kukauka, ofcoz maziwa ndio yatafuata ?

Hivi mmewahi kujiuliza huyo/hao wanao wakikuamsha miaka hamsini ijayo kukuuliza "baba umenileta dunia hii ili niishi vipi jibu lako litakuwa nini ?

Na kama huna jibu hilo sasa hivi, ni vipi kudhani kuwa ni ufahari kutotoa tu watoto bila kujali wanakuja kuishi wapi ?

Nadhani heshima ni kuhakikisha kila mmoja awe msanii ama la, tunatunza mazingira na kuirudishia dunia uhai na kupunguza kuzaa bila mpango badala ya kufikiri "kibinadamu" kuwa kwa kutoboatoboa ziwa Victoria ndio suluhisho la kudumu la wanainchi kupata maji.
 
Back
Top Bottom