Washabiki wa mpira nchini ni vilaza, Arajiga amewahi kufungiwa mara tatu

Washabiki wa mpira nchini ni vilaza, Arajiga amewahi kufungiwa mara tatu

Hakuna refa mzuri kama Arajiga kwa sasa labda kama ni shabiki maandazi utabisha. Hoja ya kwamba aliwahi kufungiwa hivyo hawezi kuwa bora ni hoja ya hovyo sana na inatolewa na mashabiki oya oya.
 
Leo hii ukifungwa jela kwa wizi hautaaminika tena na wananzego kuwa umeacha wizi
Sheria mnatunga nyie wenyewe kulalamika mna lalamika wenyewe hizo hizo mbovu mnashindwa kizisimamia. Mna akili za kusamehe kadi nyekundu lakini akili za kubadilisha matokeo mnakuwa hamnazo

Je kadi nyekundu haikusababisha matokeo chanya kwa timu pinzani?
 
Sijui ni ukilaza ujinga au??
2022 alifungiwa
2020 alifungiwa
2019 alifungiwa

Tena kuna mechi kati ya Yanga na Azam aliwabeba Yanga akafungiwa

Acheni ujinga
Basi mechi zenu zote wachezeshe Tatu Malogo na Smart ili kupunguza hivi vilio. Maana penati na kadi nyekundu hapo ni uhakika kwa 💯%
 
Hatutaki achezeshe mechi zetu, kwanini hatupi penalty? alf kila akichezesha tunafungwa
Kama vipi tuungane kupiga kelele ili Tatu Malogo na Smart ndiyo wawe waamuzi pekee wa kuchezeshe hizo mechi zenu.
 
Arajiga huwezi kumfananisha na refa yeyote kwenye ligi kwa sasa, kwanza akichezesha unaona hata kwenye fouls wachezaji hawalalamiki maamuzi hake kama wanavyochezesha marefa wengine, kwa sasa anachezesha vizuri labda kama ataharibiwa na marefa wa pembeni.
Wewe ulitakiwa kuwa Mwananchi! Sasa sijui ilikuwaje ukachangamana na hao ndugu zako walalamishi wa kila kitu. Yaani isitokee tu timu imefungwa au kutoa sare! Ni malalamiko tu.
 
Wewe ulitakiwa kuwa Mwananchi! Sasa sijui ilikuwaje ukachangamana na hao ndugu zako walalamishi wa kila kitu. Yaani isitokee tu timu imefungwa au kutoa sare! Ni malalamiko tu.
Mkuu maamuzi ya marefa wengi tunayaona kwenye hii ligi,mpira ni wa wazi kuna wakati unaona hapa refa amekosea na hapa yuko sahihi,unadhani kwa msimamo wa haki kama wa Arajiga wachezaji watafanya rafu za kijinga?maana hapindishi,sehemu inayostahili anakupa njano au nyekundu wachezaji wanaji-tune kisaikolojia kwamba akifanya kosa anaadhibiwa ipasavyo.

Tukiwa na marefa watano kama Arajiga hii ligi msimamo ungekuwa tofauti kabisa kuanzia anayeongoza hadi wale wanaofuatana.
 
Hitimisho Biodi ya Ligi ya Tanzania ni dhaifu kwasababu hiyo vilabu vyote vichukue hatua sitaki badala ya kulalamika kwenye mashuka na pengine kwenye mablanketi
 
uko sahihi hakuna refa mbovu kama Arajiga, alishafungiwa mara kibao ila kwa sababu kuna timu inanufaika naye inampigia debe.
Mechi ya Simba na Azam siyo tu hakuona rafu ya Feitotot kwa Chemalon lakini aliacha mpira uendelee pamoja na kwamba mchezaji alikuwa akichechemea. Sababa alikuwa mzito na kushindwa kufika eneo la tukio kwa wakati. Aliacha kuwapa penati Simba wakati mchezaji waAzam ameshika ili kukwepa lawama waamuzi wanaatoa penati kwa Simba za upendeleo.
Mara tatu aliingiliana na wachezaji kwa kushindwa kuendana na kasi ya mpira.
Kamaa angekuwa mzuri kama wanavyomsifia asingekosa kwenye orodha ya waamuzi 25 waliochaguliwa kuchezesha mechi za robo fainali za klabu bingwa na shirikisho huku kukiwa na timu kutoka Tanzania.
 
Back
Top Bottom