Washauri wa Rais Magufuli, mshaurini aache kutumia Kiingereza kwenye hadhara

Hii suala ni kubwa sana, haupaswi upanic
 
Ndugu yangu macho_mdiliko hata wewe hujaandika lugha sahihi hapo juu. Hakuna binadamu mkamilifu. Ila ujumbe umeshafika kwa walengwa na washauri wa mjomba Pombe.
Nani kasema kuna binadamu mkamilifu? Naomba tusichanganye mapungufu ya kibinadamu ya kawaida na u-kiazi wa darasani! Yaani mtu asome mpaka level ya Phd tena kwa kiingereza, halafu awe mwalimu afundishe kwa kiiingereza na kisha awe waziri kwa muda mrefu tu na bado simple english inamshinda kama mtoto wa darasa la saba? Hapana. Kuna kitu ambacho hakiko sawa kabisa kwenye mfumo wetu wa elimu. Na huyu tumebahatika kujua kwa sababu tu ni kiongozi. This is serious issue ndugu yangu.
 
Sasa kwanini msimshauri kutumia kiswahili badala ya kuliaibisha Taifa kiasi hiki?
 
Wewe kwa upeo wako ndiyo unaona ni hoja ya kijinga. Hapa tunazungumzia mtu aliyeandika thesis ya kitaalam ya kuhitimu Phd baada ya kufanya utafiti na baadae akawa mwalimu akifundisha kwa kutumia lugha ya kiingereza. Aliwezaje kumudu yote hayo wakati hawezi kuongea kiingereza ''cha kuridhisha''? Na wala siongei kile kizuri.

Nimekutana na wasomi wengi ambao english inawapiga chenga lakini wakizungumza unaona kabisa wana mwelekeo wa usomi na unaridhika. Hata maswali rahisi anashindwa kuelewa sembuse kujibu! Something very very wrong with his education!
 
"The Eclipse of the English Language" in the middle of native Local vernacular and overal national Swahili.

Kimalkia ni kigumu asikuambie mtu. Sisi tuliosoma before ni shida. Vijana wetu tumewapeleka international schools na kusomea nje ya nchi huwezi kuwalinganisha na sisi wa Kiingereza cha kukariri tulichoanza kusoma tukiwa darasa la 5. 😂😂😂🤣🤣🤣
 
Hahahahaaaa... (alisikika akicheka mtoto wa darasa la pili wa English medium). Anapenda sana kujifaragua na kutia watu million 60 aibu ya bure. Aongee tu Kiswahili.
 
Ni aibu kwa rais wa nchi, ambaye amesoma mpaka chuo kikuu kwa kiingereza, akaishi ulaya, akafanya Phd kwa kiingereza halafu hajui kuongea kiingereza fasaha.​
Acha uongo. Magufuli hajawahi kuishi Ulaya.
 
Rais Magufuli ni mtu huru, ni fikra huru. Na hiki ndicho kinachomfanya awe rais bora miongoni mwa marais tuliowahi kuwa nao Tanzania. Anawaza kivyake, anasema anavyotaka iwe kingreza, kiswahili au kisukuma. Akosee au asikosee.

Rais wetu si mtumwa wa mtu yeyote, akili zake hajashikiwa na mtu yeyote. Anafanya anavyoona inafaa popote pale na muda wowote ule.

Ogopa kiongozi anayesema kwa staili ya ajili kuwaridhisha watu fulani au eti aendane na fikra fulani. Political correctness. Ni wabaya maana hawana ubunifu, hawawezi fanya maamuzi magumu, yaani wapo wapo tu kama maroboti ya kikundi fulani cha watu au fikra. Tulipopata uhuru kutoka kwa mkoloni maana yake ilikuwa ni uhuru kamili -- kimwili, kifikra na kimaamuzi.
 
Ndio hapo utashangaa ana mrukia Dkt Avemaria Semakafu aliye katika program ya kuinua walimu wa cheti kuwa na diploma kuwa ni mpumbavu sasa dunia ione Mpumbavu wa kweli no yupi hiyu mtu hashauriki ngoja tarehe 28/10 aumbuke ndipo siri zake za upumbavu wake utakavyo anikwa kwa speed ya moto wa petrol
 
Usitujumuishe kwenye dhambi yako.

"Aibu kwetu sote" kivipi??
 
Ingekua ni Rais wa nchi nyingine ameongea kiswahili kibovu msingemcheka wala kushangaa ila mtampongeza kwa kujitahidi.

Ila kwa sababu za kisiasa mmeamua kumshikia bango JPM, anyway ndio siasa zilivyo.

Kama huyo rais wa nchi nyingine kapata PhD Kwa kiswahili kisha aongee kiswahili kibovu, atafurahi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…