Rais Magufuli ni mtu huru, ni fikra huru. Na hiki ndicho kinachomfanya awe rais bora miongoni mwa marais tuliowahi kuwa nao Tanzania. Anawaza kivyake, anasema anavyotaka iwe kingreza, kiswahili au kisukuma. Akosee au asikosee.
Rais wetu si mtumwa wa mtu yeyote, akili zake hajashikiwa na mtu yeyote. Anafanya anavyoona inafaa popote pale na muda wowote ule.
Ogopa kiongozi anayesema kwa staili ya ajili kuwaridhisha watu fulani au eti aendane na fikra fulani. Political correctness. Ni wabaya maana hawana ubunifu, hawawezi fanya maamuzi magumu, yaani wapo wapo tu kama maroboti ya kikundi fulani cha watu au fikra. Tulipopata uhuru kutoka kwa mkoloni maana yake ilikuwa ni uhuru kamili -- kimwili, kifikra na kimaamuzi.