de Gunner
JF-Expert Member
- Nov 2, 2021
- 2,044
- 4,558
Kuna watu, ambao wapo na wewe wakati wa raha na huwamkaribu nawe kwa manufaa yao,
Kuna watu wapo na wewe, wakati wa shida na huja tu endapo utakua katika wakati mgumu,
Kuna watu wapo na wewe sababu tu kuna vitu mnafanya pamoja, yaweza kuwa kazini, masomoni, au kwenye shughuli mbalimbali za kijamii.
Kuna watu utakutana nao, ili wakuvushe kutoka sehem moja kwenda nyingine. Hao ni kama daraja la wewe kupanda katika safari yako.
Kuna watu, watakuja kukupa funzo. Funzo ambalo laweza kuwa zuri ama baya. Ila ulitakiwa kukutana nao ili uweze kujifunza kitu fulani ambacho ni muhimu kwa mambo utakayo kumbana nayo mbeleni.
Ila kuna aina hii ya watu, ambao wapo nawe katika nyanja zote. Hawahitaji uwafanyie chochote, wala kitu chochote toka kwako, wapo nawe na wanakujali bila matarajio ya aina yoyote. Mara nyingi watu huwachukulia poa hawa watu, na kuona kama wanatupenda kupita kiasi, yaweza kuwa ila, kumbuka duniani watu wa aina hii ni nadra sana kuwapata. Wakuu hiki kitu nimechelewa sana kujifunza na sasa najutia napenda isijirudie tena.
Sema ukweli dunia ya leo, hakuna raha na watu wanastress, garama za maisha zimepanda, makazini watu kusnichiana! Majirani kusemana vibaya, ndugu wa familia moja kurogana, ajira nazo ngumu, wasichana wameharibika, yaani hakuna eneo unaweza sema lipo vizuri. Hii imepelekea hasira na taharuki kwa watu na jamii kwa ujumla. Saiz kila mtu kajifungia ndani hataki stress na majungu coz watu wamevurugwa. Hakuna uaminifu miingoni mwa watu. Sisi ni viumbe social yaani tunategemeana sasa ukitaka kuish maisha marefu lazima uwe na watu sahihi. Watu sahihi ndo hao tunaowachukulia poa.
#Washikilie wanaokujali.