WASHINGTON: Mataifa zaidi ya 50 yamesema yapo tayari kuondoa vikwazo kwa bidhaa za Marekani

MTZ 255Dar

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2018
Posts
1,152
Reaction score
3,967
Mataifa zaidi ya 50 duniani yamesema yapo tayari kujadiliana na Marekani juu ya kuondoa vikwazo vya kibiashara kwa bidhaa za Marekani zinazoingizwa katika mataifa hayo. Hii inakuja baada ya Marekani kuongeza ushuru wa asilimia kadhaa kwenye bidhaa zinazouzwa nchini Marekani kutoka mataifa yote duniani. Nyongeza hiyo ya Ushuru ya Marekani imeanza kufanya kazi leo tarehe 07 April.

Ushuru huo umesababisha kuyumba kwa masoko ya Hisa duniani kote huku Dolar ya Marekani ikipanda thamani kwa asilimia 1.4 kwa siku ya 6 mfululizo tangu Rais wa Marekani, Donald Trump atangaze orodha ya ushuru kwa mataifa mbali mbali duniani.

Mataifa kadhaa tayari yameondoa vikwazo kwa bidhaa za Marekani zinazoingizwa kwenye mataifa hayo. Zimbabwe, Lethoto, Thailand za Vietnum tayari zimeweka ushuru wa 0.00% kwa bidhaa za Marekani zitakazoingizwa nchi hizo, huku zikitarajiwa kufutiwa ushuru ulioongezwa hivi sasa na Trump.

Nchi za Japan, Taiwan, Israel na Cambodia zimesema zitatuma mawaziri wao wa fedha nchini Marekani ili kumaliza mzozo huo wa Kibiashara.

Nchi ya China imelipiza kwa kuongeza ushuru wa 34% kwa bidhaa zote za Marekani zinazouzwa nchini humo, jambo ambalo limemkera Trump na kuliita ni Kosa la hatari lililofanywa na viongozi wa Beijing kwa kukurupuka. Trump ameahidi majibu makali kwa China mda ujao.

Umoja wa Ulaya umesema unapitia hatua kadhaa za kuiadhibu Marekani kama jibu la ushuru wa 20% kwa bidhaa za Ulaya zinazoingia nchini Marekani. Italia, Uingereza na Uhispania zinapinga wazo la kuongeza ushuru wa bidhaa za Marekani kwani zitaifanya Marekani nayo kujibu vikali, badala yake, wanashauri kujadiliana na Marekani ili kuutatua mzozo huo kwa njia ya Mazungumzo zaidi.

View: https://youtu.be/gbXOn8WRI9k?si=XFrE26fuSVefS6r_
 
Washachelewa sana,USA ilitakiwa kupata Rais wa Aina ya Trump muda sana.
Kwa sasa China ndo anaenda kudhibitiwa Rasmi na bidhaa za MADE IN USA zitaanza kuingia nchi nyingi kwa sababu ushuru utakua umepunguzwa.

Haiwezekani bidhaa original toka USA zikaingizwa kwa ushuru sawa na bidhaa fake za China,huo ni upumbavu na marekani kishaona huo uhuni anaotumia mchina kujipandisha kuwa super power.

Viwanda vya bidhaa kutoka USA vitaanza kufanya kazi ya uzalishaji na kutupa vitu original na kwa bei affordable
 
Upo sahihi kabisa tayari baadhi ya nchi wameshaanza kuweka ushuru wa o.oo kwa bidhaa za marekani, mvimba macho kajaa mazima atanyooka muda si mrefu! Na yale madini alikuwa anaiba kule kongo muda si mrefu marekani inatinga kule jumla!
 
Washachelewa sana,USA ilitakiwa kupata Rais wa Aina ya Trump muda sana.
Kwa sasa China ndo anaenda kudhibitiwa Rasmi na bidhaa za MADE IN USA zitaanza kuingia nchi nyingi kwa sababu ushuru utakua umepunguzwa.

Haiwezekani bidhaa original toka USA zikaingizwa kwa ushuru sawa na bidhaa fake za China,huo ni upumbavu na marekani kishaona huo uhuni anaotumia mchina kujipandisha kuwa super power.

Viwanda vya bidhaa kutoka USA vitaanza kufanya kazi ya uzalishaji na kutupa vitu original na kwa bei affordable
Ila MAGA ni watu wajinga sana
 
Ndo shida ya kumpa nchi mtu ambae hana cha kupoteza.

Hadi Bill Ackman jana kasema "This is not what we voted for"

Trump atasababisha recession kubwa sana, hadi aje kutoka madarakani basi Wallstreet itakua ishapoteza hela vya kutosha, stock zitakua cheap sana. Hapa ndio naona mzee Warren Buffet aliona mbali sana kuuza baadhi ya stocks mapema kabisa.

Trump ashakua kichaa wa madaraka ila anachokitafuta atakipata tu. Anadhan China itampigia magoti wakati kwa sasa china wapo mbele sana ya muda hasa upande wa technology. Mwaka ule aliipiga China vikwazo hadi huawei ikaachana na android ila bado huawei iko juu sana kiteknolojia ukilinganisha na makampuni ya US.

Kama ningebet basi ningempa odds zote mchina kwenye hili vanga
 
Washachelewa sana,USA ilitakiwa kupata Rais wa Aina ya Trump muda sana.
Kwa sasa China ndo anaenda kudhibitiwa Rasmi na bidhaa za MADE IN USA zitaanza kuingia nchi nyingi kwa sababu ushuru utakua umepunguzwa.

Haiwezekani bidhaa original toka USA zikaingizwa kwa ushuru sawa na bidhaa fake za China,huo ni upumbavu na marekani kishaona huo uhuni anaotumia mchina kujipandisha kuwa super power.

Viwanda vya bidhaa kutoka USA vitaanza kufanya kazi ya uzalishaji na kutupa vitu original na kwa bei affordable
Time will tell
 
Marekani ilipandisha kiwango cha maisha ya watu wake, kiasi kuwa kutengenezea bidhaa Marekani itabidi ziuzwe kwa bei ghali zaidi ili faida ipatikane.

Sasa unakuwa na sera unaenda kuweka viwanda vingi nnje ili kutengeneza bidhaa zako.

Sielewi kwanini hawakuliona hilo mapema.

Ilibidi waweke madaraja ya wafanyakazi, ili kuendana na ushindani.

Sasa ndio wanakuja kushtuka muda huu...
 
Kwakweli ni upumbavu,unanunua kiatu kutoka china unavaa mwezi 1 au 2 kimeisha
China Wana mambo ya ajabu ht ukivaa kitu sshv kutofautisha km og na fake ni ngumu 🤣
 
Marekani ilipandisha kiwango cha maisha ya watu wake, kiasi kuwa kutengenezea bidhaa Marekani itabidi ziuzwe kwa bei ghali zaidi ili faida ipatikane.

Sasa unakuwa na sera unaenda kuweka viwanda vingi nnje ili kutengeneza bidhaa zako.

Sielewi kwanini hawakuliona hilo mapema.

Ilibidi waweke madaraja ya wafanyakazi, ili kuendana na ushindani.

Sasa ndio wanakuja kushtuka muda huu...
Biden mpuuzi 😅
 
Back
Top Bottom