Mcqueenen
JF-Expert Member
- Nov 2, 2019
- 6,843
- 11,702
Kwan unaweza kuandika zaidi ya moja?Napanga madini Mkuu...soon naanza kushusha nondo usikae mbali
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwan unaweza kuandika zaidi ya moja?Napanga madini Mkuu...soon naanza kushusha nondo usikae mbali
Wewe utakuwa kati ya watu ambao hawasomi vigezo na masharti 😂 😂 unaweza kuandika zaidi ya moja, ni wewe tu na uwezo wakoKwan unaweza kuandika zaidi ya moja?
Hapana,mainbody tu,kichwa cha habari kinahitaji maneno yasiyopungua 4.Halafu hivi katika hayo maneno 700 - 1000 kichwa cha habari kinahesabiwa?
🙌Lengo la hiyo kitu kwanza sio kupata hela, ni kuonesha njia ya mabadiliko wengine waipitie, kama njia yako ikiwa nzuri zaidi basi utapata hiyo unayosema kama zawadi kwa mchango wako, kuanzia mwanzo usiifanye kwa lengo la kupata hela
Mbona ni machache, hasa ukiwa na cha kuandika... ukiwa unapiga porojo lazima uone ni mengiManeno 700 sio mchezo, kweli pesa sabuni ya roho
😂😂😂😂😂😂😂Hahahaha sizani kama ni pumba hata kama ni pumba yaani si ungetokea ndo waufute? Yaani hata kutokea hautokei
Je, mkuu wewe hili bandiko lako linahusu utawala bora au uwajibikaji? Mpaka sasa una kura 15 lakini kuna baadhi wameandika minakasha kwa kufuata vigezo vyote hadi sasa wana kura 0.
Kama tunavyojua mchongo ushaanza na nimeona kuna milioni 20 za kubeba. Watu tunaotaka kuchota hizi milioni 20 tunafata vigezo kweli au mnafikiri ni kazi rahisi kuzipata?
Mtu unaandika tu ovyo ovyo kama uropoka, vigezo hufati halafu unajiwekea asilimia za kushinda!
Kuna baadhi ya Vigezo na Mashari hatufati ambavyo nimeona vitatukosti sana sisi tunaotaka kunyakuwa hizo Milioni 20:
Kigezo cha idadi ya maneno
Katika vitu naona itakula vichwa ni kigezo hiki 🤣 🤣. We unaambiwa andika maneno kati ya 700 hadi 1000 unaandika maneno 1050, au maneno 400, mwingine anajikuta kukamia anaandika maneno 2000+🤣🤣. Mpo humu mnaojikuta Mataikoni wa kuandika, nyie mjue hii milioni 20 haiwahusu, mmetuachia.
Kwa kuwasiadia kama unaandika moja kwa moja hapa jukwaani, kopi uzi wako na uuweke kwenye Microsoft Word pale itakuonesha idadi ya maneno kwa chini kushoto hivyo utajua kama umezidisha maneno au la.
Idadi ya maneno kwenye kichwa cha habari
Hapa kigezo kimekwambia kweupeee, kwamba kichwa cha andiko lako kisipungue maneno manne, jitu linakwenda kuandika maneno matatu au mawili, wewe jua ushajiondoa kwenye shindano. Kama umeacha likichwa lako hivyo peleka ujumbe kwa Mods mapema ubadilishe.
Kuna hili kundi maalum😂😂 kichwa chao cha habari kinakuwa Stories of Change, au Utawala Bora au Uwajibikaji kwenye nyanja mbalimbali
Bwana bwana, hawa wanafosi maneno haya yaonekane kwenye kichwa cha habari na kwenye maandiko yao wakati wanaongea pumba na cha maana ni hayo maneno. Embu kuwa serioua bwana. Milioni 20 sio mchezo, we unafikiri utaipata kirahisi hivi?
Una njia nyingi za kufanya usifosi kuweka maneno hayo kwenye kichwa cha habari au kuyataja maneno hayo mara kwa mara, sema moja moja unavyotaka mtu/sekta fulani iwajibike, sema vile unavyoona utawala bora uko vipi badala ya kutaja tu Utawala Bora halafu maudhui sifuri. Kwa kufanya hivi andiko lako litaeleka vizuri tu na hutaonekana hujui unachofanya.
Wanaodhani Utawala Bora au Uwajibikaji unalenga Siasa pekee🤔
Jamani, yaani unakuta mtu mchovu kwenye Siasa lakini anang'ang'ana aandikie Siasa kwakuwa amezoea kusikia Uwajibikaji na Utawala bora kwenye Siasa.
Hivi unajua unaweza kuongelea chochote kwenye jamii yako kuchochea Utawala Bora au Uwajibikaji? Watu hapa mnafanya kazI maeneo mbalimbali inaweza kuwa kwenye sekta ya afya, burudani au hata urembo, usiniambie hapo ulipo kila kitu kipo sawa 100% na usingependa mambo yaboreshwe hata kidogo? Usiniambie hapo ulipo watu wanawajibika na majukumu yao kwa kiwako cha kuridhisha kiasi kwamba huoni sehemu ya kuboresha kufanya watu wawajibike zaidi na kuchangia kuwa na utawala bora unaomfaidisha kila mtu.
Watu mna malalamiko kibao kibao kwenye sekta ya afya, elimu, wastaafu, jeshini, burudani (tuzo za mziki zimetola juzi tu hapo malalamiko kibao) malalamiko kwenye sekta ya ulimbwende (urembo) yapo kibaooo kweli inakosa kitu cha kuongelea kuchochea mabadiliko na kupendekeza mambo yawe bora? Wewe Mwalimu, Mwanajeshi, Daktari, Mwanafunzi, Mwanamuziki, Mchoraji, Mstaafu, Mama ntilie, Machinga, Bodaboda, nk, huna lolote la kusema kuhusu Uwajibikaji au Utawala wa sekta hiyo uliyopo? Umeridhika kabisa na kila kitu na hakuna pa kuboresha? Em kuwa serious bwana, lete nondo hizo.
Nadhani sasa mmepata mwanga na hii mada haitaonekana ngumu tena na watu wataacha kung'ang'ania mambo ya siasa ambayo hata hawayawezi. Kila mtu ataleta nondo zake kutoka sehemu aliyopo zinazooneaha kweli watu wanajua wanaongelea nini, hata mtu kukupigia kura asione mzigo au anakupigia kura sababu umemtumia ujumbe PM.
Mwisho ni hawa wenzangu na mimi ambao, pamoja na Vigezo na Masharti kuwepo hatasoma chochote, yaani ni kama vile yeye 'stafu' mwezenu. Si mnawajua hawa stafu wakiingia kwenye madaladala wanakuwa hawalipi nauli? Sasa hawa wanajikuta kama stafu wa stories of change🤣🤣🤣. Nyie ndugu zangu tunawaombea tu Mungu awarehemu🤣🤣🤣 kwani hili shindano haliwahusu.
Ndugu zangu ni katika kukumbushana tu, kama unataka kuiwania hii Milioni 20 kama mimi basi lazima ujipinde utoe kitu ambacho watu wakisoma wanaona yes umeleta nondo kweli. Na uzuri ni kwamba ukileta nondo yaani haiwezi kujificha, utaonekana tu.
Nawatakia ushandani mwema, mwenye kisu na atoboe. Kwenu Wakuu.
Wapi hii mkuu?Ingia kwa webView attachment 2623294
Huu uzi itakua modz waliona unafaa kuwambusha watu kuhusu shindano wakaona watu wauone huku, afu acha makasiriko...kupigiwa kura ni uamuzi wa wanaosoma andiko lako, kwaiyo we andika kinachowavutiwa watu basi watu watakuja kutia neno na kukupa kura zao. Unaandika kitu ambacho hakishawishi watu kuchangia kama vile unapiga somo la uraia unatemea utapata kura?Je, mkuu wewe hili bandiko lako linahusu utawala bora au uwajibikaji? Mpaka sasa una kura 15 lakini kuna baadhi wameandika minakasha kwa kufuata vigezo vyote hadi sasa wana kura 0.