Tetesi: Washtakiwa kesi ya Uhujumu Uchumi waachiwa kwa dhamana

Tetesi: Washtakiwa kesi ya Uhujumu Uchumi waachiwa kwa dhamana

Lema alie ota ndoto ananyimwa dhamana kwa maelekezo toka mbinguni,lakini hawa wanaomaliza rasilimali zetu wanapewa dhamana?.

Kweli mktaa pema pabaya panamwita(watu walikataa mabadiliko sasa wanaitwa na fisiemu).
 
Watuhumiwa wa kesi ya Uhujumu Uchumi, mauaji ya tembo 85, wameachiwa kwa dhamana katika namna inayotia shaka. Hapa ijulikane kuwa kesi za aina hii hazina dhamana.

Wazalendo tusimame imara.
unaifahamu hadithi ya nyani waliompamba mwenzao ili akaolewe na mwenye shamba na wao wale mahindi kirahisi?
 
Manyerere Jackton bado kuna watu waamini "Mtukufu " ana nia ya dhati ya kupambana na ufisadi ndani ya nchi yetu kama wahujumu uchumi waachiwa kwa dhamana unategemea nini?
Kuna wabunge wa CCM walihongwa milioni 10 kila mbunge wapitishe muswada wa habari ambao waliupitisha wa kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari.
Ulisikia kauli ya mtukufu kuhusu tuhuma za wabunge hao?
Tembo watu wetu watakuja kuwaona kwenye picha tuu.
 
Kwa Nchi za Afrika yote yanawezekana ,waachiwe tu hamna tatizo..
 
Sheria ya kuwanyima dhamani watu wasiotuhumiwa kwa mauaji au uhaini ni za kinyonyaji. Mtu anakaa selo kwa muda mrefu anasubiri upelelezi ukamilike, ruling inatoka mtu anaachiwa huru wakati ashakaa miaka mitatu jela.

Nani anamfidia hasara ya muda, mateso ya kisaikolojia na hasara za kiuchumi na kijamii alizopata? Wapewe tu dhamana waendelee na maisha mengine.
 
Back
Top Bottom