Tetesi: Washtakiwa kesi ya Uhujumu Uchumi waachiwa kwa dhamana

Tetesi: Washtakiwa kesi ya Uhujumu Uchumi waachiwa kwa dhamana

Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, maarufu Mahakama ya Mafisadi imewapa masharti sita ya dhamana washtakiwa wa kesi ya uhujumu uchumi wanaodaiwa kukutwa na nyavu haramu za kuvulia samaki katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Katika masharti hayo, Mahakama imemtaka mshtakiwa Ally Raza (34) kuwasilisha mahakamani fedha taslimu Sh2,582,191,666 (zaidi ya Sh2.5 bilioni), au hati ya mali yenye thamani sawa na kiasi hicho.

Mshtakiwa Jeremiah Kerenge (40), ametakiwa kuwasilisha mahakamani Sh4,454,241,666 (zaidi ya Sh4.4 bilioni), au hati ya mali yenye thamani sawa na kiasi hicho.

Chanzo:Mwananchi

Manyerere Jackton hii habari sio ndio hiyo uliotuletea labda umechanganya tu?Kama ni habari tofauti,basi tunahitaji wanasheria watusaidie katika hili.
 
Hahhahah mahakama iachwe ifanye kazi halafu ww nilikushusha thaman tokea ulipoomba whiskey ikulu nikajua tu huna tofauti na kina makonda

Acha porojo! Sijaomba whisky! Weka clip hapa ujue maudhui ya swali. Hapa tunajadili hawa majangili kuachiwa.
 
Mkuu ungejitahidi kutoa complete package ya hii issue.Jangili kuachiwa kama sio udhaifu wa sheria zetu haikubaliki
 
Acha porojo! Sijaomba whisky! Weka clip hapa ujue maudhui ya swali. Hapa tunajadili hawa majangili kuachiwa.
Hivi tunafikiri kuna hakimu ataweza kukataa mshiko wa nguvu? ....Hata kama angekuwa mzalendo sana atajiuliza ''wabunge wanahongana milioni kumi kupitisha miswada, mimi kwanini nisile''? Vita ya kupambamba na rushwa sio rahisi tunavyofikiria. Kipimo kilekile wanachopimiana viongozi wa siasa na hicho hicho wanachotumia watendaji wa chini.
 
Eti jina halisi la mpemba anaitwa nani? Hata huku JF hatajwi kabisa. Niliamini akitajwa hii vita ya ujangili itaongeza speed.
 
Lema alie ota ndoto ananyimwa dhamana kwa maelekezo toka mbinguni,lakini hawa wanaomaliza rasilimali zetu wanapewa dhamana?.

Kweli mktaa pema pabaya panamwita(watu walikataa mabadiliko sasa wanaitwa na fisiemu).

Tatizo la Lema ni moja tu, Nafsi yake haiamini kuwa Mzee Kikwete kishastaafu!
 
Tuache mzaha, nchi unaumizwa sana. Ujangili unamaliza rasilimali hii adhimu.
Nani alikwambia nchi yetu inaangamizwa na majangili?
Huwezi kuwakamata Vibarua wa porini wenye njaa na wasio jitambua, halafu unakuja kutuambia hao ndio majangili wanaomaliza tembo wetu.
Nchi inamalizwa na makada wa CCM.

Embu fikiria, katika taifa lenye jeshi la Polisi, JKT, Jwzt, Kikosi cha wanyama pori, Mgambo, Polisi Jamii, TISS halafu........
Jangili gani huyo anayeweza Kukamata mamia ya wanyama mbali mbali kutoka Mbuga kuu, akasindikizwa na Msafara wa Kijeshi mpaka KIA, akaleta ndege kadhaa za Kijeshi kutoka Qatari, akawakunja Twiga na kuwaingia ndani ya ndege na kisha kuondoka.
 
Watuhumiwa wa kesi ya Uhujumu Uchumi, mauaji ya tembo 85, wameachiwa kwa dhamana katika namna inayotia shaka. Hapa ijulikane kuwa kesi za aina hii hazina dhamana.

Wazalendo tusimame imara.
Chanzo cha habari muhimu au wewe ni mgeni jf?bila ya chanzo usilete ukuda hapa
 
SAWA HIYO OLE WAKO MAMA TANZANIA.MAJANGILI DHAMANA LEMA HAKUNA DHAMANA.KAAZI KWELI KWELI!!!!!!!!!!
 
Hahhahah mahakama iachwe ifanye kazi halafu ww nilikushusha thaman tokea ulipoomba whiskey ikulu nikajua tu huna tofauti na kina makonda
alitaka kuzimua mkuu,inawezekana alilala nazo
 
Watuhumiwa wa kesi ya Uhujumu Uchumi, mauaji ya tembo 85, wameachiwa kwa dhamana katika namna inayotia shaka. Hapa ijulikane kuwa kesi za aina hii hazina dhamana.

Wazalendo tusimame imara.
ulisomea sheria wapi mkuu?
 
Back
Top Bottom