Tetesi: Washtakiwa kesi ya Uhujumu Uchumi waachiwa kwa dhamana

Tetesi: Washtakiwa kesi ya Uhujumu Uchumi waachiwa kwa dhamana

Manyerere Jackton bado kuna watu waamini "Mtukufu " ana nia ya dhati ya kupambana na ufisadi ndani ya nchi yetu kama wahujumu uchumi waachiwa kwa dhamana unategemea nini?
Kuna wabunge wa CCM walihongwa milioni 10 kila mbunge wapitishe muswada wa habari ambao waliupitisha wa kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari.
Ulisikia kauli ya mtukufu kuhusu tuhuma za wabunge hao?
Tembo watu wetu watakuja kuwaona kwenye picha tuu.
Usimuulize alisikia kauli ya mtukukufu. Pia yeye mwenyewe alitetea hilo?
 
Lema anaingiaje katika hili? We kweli ni mvivu wa kufikiri. Yaani watu wakisema ukweli ni lazima uuhusishe ukweli huo na kesi ya Lema. Kweli elimu ni ya muhimu sana!
Sasa na wewe kwa akili ya kawaida tu unamnyima dhamana lema ambaye kosa lake aliota ndoto kuwa Juma atakufa unampa dhamana mhujumu uchumi kwanini tusishangae? Huu ni mfano tu jamaa katoa.
 
Na mafisadi akina Rugemarila, lugumi, IPTL, EPA, MV ufisadi, Chenge, Tibaijuka etc lini hawa wahujumu wa uchumi watapandishwa kizimbani.

Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, maarufu Mahakama ya Mafisadi imewapa masharti sita ya dhamana washtakiwa wa kesi ya uhujumu uchumi wanaodaiwa kukutwa na nyavu haramu za kuvulia samaki katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Katika masharti hayo, Mahakama imemtaka mshtakiwa Ally Raza (34) kuwasilisha mahakamani fedha taslimu Sh2,582,191,666 (zaidi ya Sh2.5 bilioni), au hati ya mali yenye thamani sawa na kiasi hicho.

Mshtakiwa Jeremiah Kerenge (40), ametakiwa kuwasilisha mahakamani Sh4,454,241,666 (zaidi ya Sh4.4 bilioni), au hati ya mali yenye thamani sawa na kiasi hicho.

Chanzo:Mwananchi

Manyerere Jackton hii habari sio ndio hiyo uliotuletea labda umechanganya tu?Kama ni habari tofauti,basi tunahitaji wanasheria watusaidie katika hili.
 
Ile mahakama kuzinduliwa kwa mwendo kasi ilikua kumpatia mkuu cha kusema kwa waandishi wa habari, tatizo la mafisadi nchi hii sio mahakama. Tatizo ni pale anaotakiwa kutokomeza au kufuatilia ufisadi nao wanapokosa usafi. Hili zoezi la ufisadi na ukaguzi wa vyeti tunge outsource tu.
 
Na mafisadi akina Rugemarila, lugumi, IPTL, EPA, MV ufisadi, Chenge, Tibaijuka etc lini hawa wahujumu wa uchumi watapandishwa kizimbani.
Hao wanalindwa kama mboni ya jicho alafu kuna watu wanajisifu eti wao wamekuja kupambana na ufisadi.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kwa hapa Tanzania wanasema ni rahisi sana kwa fisadi wa mabilioni kupewa dhamana kuliko kwa muota ndoto na maono anayetangaza ndoto au maono yake
 
Angetoka ungesema haki imetendeka...akibanwa amri imetoka juu...mnafikiri kila siku tu haki kuwa upande wenu ndo mahakama iwe huru.
 
Hakunaga dhamana kwenye kesi zinazohusu ndoto na maono hasa ya wapinzani.
 
Lema alie ota ndoto ananyimwa dhamana kwa maelekezo toka mbinguni,lakini hawa wanaomaliza rasilimali zetu wanapewa dhamana?.

Kweli mktaa pema pabaya panamwita(watu walikataa mabadiliko sasa wanaitwa na fisiemu).
Mkuu we Hacha tu Mungu Anawaona.
 
Katika hili sina Uzalendo wowote.
Hao jamaa waachiwe kabisa huru, sijaona kosa lao mpaka sasa, tunataka wakamatwe wahusika halisi wa Biashara hiyo na kushtakiwa.

Mimi bila Kinana kufikishwa mahakamani, sitavaa huo uzalendo kabisa.
Sijuwi Kama Itawezekana.
 
Alipopambika na kurembeka aliwasahau ndugu zake hadi akamponza mjomba wake kuchomwa mkuki..... I still love this story [emoji8][emoji8][emoji8][emoji8] umenikumbusha mbali sana
Hadithi imenikuna sana, hebu idadavue vizuri, inaelekea ni tamu mno
 
Back
Top Bottom