Ha ha ha ha ha uvumilivu huutaki kabisa wewe haya
Dellah mapenzi hayachagui huyu ni mume wa mtu.....kaacha mke au what....Kinachojalisha kwangu ni ananipenda kweli? wengine hawajaoa na tabia zao ni mbaya kuliko wale walioacha wake zao.... mbona husemi kama mkewe alimtenda au? Mi nashauri umjali mtu kwa utu wake hasa katika mapenzi ukimchunguza bata hutoweza kumla... huenda wakati yupo na mkewe hakujua nini maana ya kupenda na kupendwa kwako atabadilika na kuwa mwanaume anajali hisia za mwanamke
Mama Big hapo kwenye red kuna siku yake leo ni specifically kwa kina bacha tu
Hebu nambie unavumilia nini??
No love, no peace, no.........
Unavumilia nini, mama ako huyo, dada ako huyo
Where is Love? Au kinyume cha upendo ni uvumilivu nn??
Unajua unavyoniharibia mipango yangu hapa jamvini? Utakava nafasi zao wewe?Tena wewe ndo mtuhumiwa namba moja
We Dena unanitafuta ubaya?
Wewe kwakuwa hujaacha mke, hii sredi haikuhusu.haya haya jamani hebu nipeni summary ya kinachoendelea hapa....!nimetoka kwenye jukwaa la stress nimetolewa knock-out nimerud nyumbani!
kwa hiyo next post tunachangia nin?
NB yako ingekuwa: "Usikubali mwanaume amuache mkewe akuoe wewe." hapo ningekuelewa. Mwanaume wa hivyo ipo siku atakuacha wewe akaoe pengine.
Tukumbuke mwanaume kumuacha mkewe sometimes makosa hutokea kwa mke. Mengine mazito hayavumiliki.
Habari zenu wote.
Katika pita pita zangu nimekutana na mambo mengi ambayo yamekuwa yakinishangaza sana. Katika wanaume 25 walioachana na wake zao (niliowafanyia uchunguzi) hawawi na mapenzi tena. Kama kuna msichana humu akikutana na mwanaume kama huyu namshauri akae mbali nae kabisa na uweze kujiuliza maswali yafuatayo:
1. Kwanini aliachana na huyo mkewe??
2. Wewe unakipi kipya hasa ambacho utamfanya asikuache kama huyo mwingine??
3. Kakufuata wewe kwa sababu gani??? (Pesa, uzuri, nk)
4. Alikuwa anatafuta pa kupumzika then ale kona lakini ukambana akashindwa kuchomoka
5. Endeleza na sababu zako nyingine nyingiiiiiiiiiii
NB: Usikubali kuolewa na mwanaume alieacha mkewe wa ndoa kamwe!!!!!!!!!!!!!!!11
Husninyo sijui nikuzawadie nini kwa hili jibu lako mama!YOU HAVE NAILED IT!!!!!!!!!!!
pipi tu inatosha.
hao uliokutana nao Dena wamekupa mtazamo usio sahihi. na tatizo sasa wewe umetoa majumuisho ambayo siyo sahihi pia, hii nadhani ni kutokana na picha uliyopata. kuna wengi tu walioachika (wake kwa waume) ambao wanapenda tena na wanaishi vizuri na wenzi wao
Maelezo yako yanaonyesha umeachana na mumeo sasa unawasiwasi atadakwa na uliowaita wasichana wa JF, sasa nikuambie nikiwa kama MRS, uzembe uliofanya wa kuachana na mumeo lazima uujutie, mume bwana usimuache hata siku moja we mlie kobisi tu lazima siku atakubembeleza tu,halafu nikuulize wewe unauchungu gani na hao wasichana? unajua wameshapitia kuachwa na wanaume ambao hawajaoa mara ngapi? Uhusiano hasa wa kimapenzi hautabiriki bwana! Basi wasiooa wangekuwa hawana shida ile first touch tu msichana angeolewa. Pole fanya juhudi za kurudiana na mumeo, dua la kuku halimpati mwewe! Siku hizi mume tunamng'ang'ania mwenzio.