Mara nyingine nyie akina mama wenye nyumba hamuishi nao kwa wema hawa mabint...
Mnawalundikia mikazi mpaka ambazo ni jukumu lenu(kufua vyupi vyenu na waume zenu)
Mnatafuta dada wa kazi kwa sababu ya uvivu sio kusaidiwa kazi
Na yeye ni binadamu mfanyie ukarimu muda mwingine msaidie anajenga uupendo na wewe...kuna umbea mwingine anaweza kukushirikisha..
Muamini, Atakuamini atajiamini sana endapo ukimtendea wema uadilifu na ukarimu atakuheshimu...sio alie yeye jikoni nyie mezani kuleni wote...usiwe mtu wa kumtilia tilia shaka tu...HAKUNA MTU ANAYEPENDA KUTOAMINIKA...HATA WEWE HUPENDI...
Mnawakaripia karipia sana...ondoeni hiyo akili chafu mliyonayo vichwani mwenu yaani kidogo mnawatolea kauli kali kama watoto zenu...
Msimkaripie mbele za watoto wenu, na ikiwezekana wakaripie watoto wako na wawajibishe mbele yake ili wamuheshimu...sio mnawatetea watoto wenu wakikosea kutwa kuwagombeza wao...
Sema nae vema na mwache afanye kazi kwa wastani...sio kwa sababu wamlipa ndio umlundukie kazi saa 24...huo ni utumwa na roho mbaya...
Acheni kutia HILA chakula wanachopika...MSIKISIMANGE CHAKULA CHAO...kama acha usile alafu sema nae kwa wema...
Usiisimange kazi aliyoifanya, sio kakosea kidogo tu UNAMSIMANGA, hujaridhika fanya wewe mwenyewe...KWANZA NDIO JUKUMU LAKO LA MSINGI...
Ukiwaletea watoto wako zawadi mletee na yeye...
Mshirikishe katika ibada zako kama mpo dini moja, ikiwa yupo tofauti MPE MUDA WA KUABUDU DINI YAKE...USIMNYIME FURSA HIYO...
ZINGATIA: huyu ni MSAIDIZI WA KAZI...
WATENDEENI WEMA, UKARIMU NA UADILIFU HAWA WATU...MTAONA MATUNDA YAKE...
ALLAH AWAONGOZE...