Wasichana wa kiislamu wamekamatwa wakiwa wamefungiwa kwenye nyumba Dodoma, inayosadikika kupewa elimu ya dini

Wasichana wa kiislamu wamekamatwa wakiwa wamefungiwa kwenye nyumba Dodoma, inayosadikika kupewa elimu ya dini

Hilo ni soko la binadamu, ambapo wanaandaliwa kwenda kuuzwa kwa waume zao nje ya nchi
 
Uongo chuo hakina maprofesa na chuo kikuu chochote kisicho na maprofesa ni duni

Walimu wote wa CHuo hawa hapo nimetoa list toka website yao wenyewe angalia CV zao hakuna Proffessor

Shot...
Nimefika MUM nimepokelewa na Prof. Mussa Assad na Prof. Hamza Njozi.

Nimewahi halikadhalika kuwa kwenye mradi wa utafiti na Prof. Ibrahim Juma kutoka MUM.

Nashangaa kuwa hawapo kwenye hiyo orodha.

Nakumbuka pia alikuwako Prof. kutoka Malaysia lakini alikwenda likizo kwao na hakurejea kwa sababu za corolla.
 
Hongera watu usalama kwa kuwahi maana walikuwa wanaandaliwa kuwa watu hatari
Ash...
Hapakuwa na tishio la usalama.
Ingekuwa hilo limethibiti Sheikh Yusuf Muhammad angefikishwa mahakamani kujibu mashtaka.

Ugonjwa ni ule ule wa kuogopa Uislam uwe ni historia yao katika kupigania uhuru wa Tanganyika au kujenga taasisi zao huru.
 
Niz...
Unahitaji kuijua historia ya uhuru wa Tanganyika ili kuweza kuchangia kwa uhakika.

Wote walioasisi African Association mwaka wa 1929 walikuwa na elimu kwa kiwango cha wakati wao.

Halikadhalika mabadiliko makubwa yalipofanyika ndani ya TAA mwaka wa 1950 viongozi waliokuwapo wakati huo walikuwa wameelimika kwa kiwango cha nyakati hizo.

Alikuwapo Abdul Sykes, Hamza Mwapachu, Dr. Vedasto Kyaruzi, Dr. Wilbard Mwanjisi na mdogo wake Roland Mwanjisi, Dr. Joseph Mutahangarwa, Dr. Luciano Tsere, John Keto, Thomas Saudtz Plantan, Schneider Abdillah Plantan, Ramadhani Mashado Plantan, Erica Fiah, Clement Mohamed Mtamila, Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo na katika majimbo walikuwapo wazalendo wengi kama hawa, Kanda ya Ziwa kulikuwa na Paul Bomani, Ali Migeyo, Sued Kagasheki.

Hawa walikuwa wameelimika vya kutosha.
TAA hakikuwa chama kinachoongozwa na watu wajinga.

Wala kilichomfanya Julius Nyerere apewe uongozi wa TAA mwaka wa 1953 si elimu yake pekee.

TAA ilimuhitaji kiongozi Mkristo akamate nafasi ya juu ili kuleta umoja wa Watanganyika vinginevyo laiti kiongozi wa harakati za uhuru angekuwa Muislam vuguvugu lote lile lingechukua sura kuwa ni Waislam peke yao ndiyo wanaochochea wananchi kudai uhuru.

Hili lingesababisha kwa Waingereza kuwashawishi Wakristo na wao waunde chama chao.

Tanganyika ingeingia katika siasa za kudai uhuru ikiwa imegawanyika.

Huu ndiyo ulikuwa msimamo na fikra ya Hamza Mwapachu mtu aliyemwingiza Nyerere katika harakati za uhuru Dar es Salaam kupitia kwa Abdul Sykes.

Wakati Nyerere alinafika Dar es Salaam mwaka wa 1952 hawa ndiyo walikuwa viongozi wa TAA wakiendesha mambo kupitia TAA Political Subcommittee: Dr. Vedasto Kyaruzi (President), Abdul Sykes (Secretary), Hamza Mwapachu, Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Steven Mhando na John Rupia.

Hii ndiyo historia ambayo wengi hamuifahamu.

Ukitaka kuijua historia ya uhuru wa Tanganyika nakushauri usome kitabu cha Abdul Sykes.

View attachment 2898343
Naijua sana historia ya uhuru wa Tanganyika, lakini narudia Tena wakati wa TAA na hatimaye kuundwa kwa TANU mwenye elimu ngazi ya Digrii alikuwa ni Kambarage tu na mwenye hela kuwazidi wote alikuwa John Rupia. Wengine walikuwa na elimu ya kawaida na hela kiduchu.
 
Ash...
Hapakuwa na tishio la usalama.
Ingekuwa hilo limethibiti Sheikh Yusuf Muhammad angefikishwa mahakamani kujibu mashtaka.

Ugonjwa ni ule ule wa kuogopa Uislam uwe ni historia yao katika kupigania uhuru wa Tanganyika au kujenga taasisi zao huru.
Hilo dini linafundisha chuki bwana unafikir hatujui
 
Naijua sana historia ya uhuru wa Tanganyika, lakini narudia Tena wakati wa TAA na hatimaye kuundwa kwa TANU mwenye elimu ngazi ya Digrii alikuwa ni Kambarage tu na mwenye hela kuwazidi wote alikuwa John Rupia. Wengine walikuwa na elimu ya kawaida na hela kiduchu.
Niz...
Hapana huijui sana historia ya uhuru wa Tanganyika.
Mimi naijua sana kiasi nimeandika kitabu cha historia hii.

Kitabu hiki kimebadili historia iliyokuwapo ya TANU na historia ya Julius Nyerere.

Kitabu kinakwenda chapa ya nne.
Kimepokelewa vyema ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Umuhimu wa kitabu hiki ni kule kueleza yale ambayo hayakupata kuandikwa kabla.

Ungekuwa unaijua historia ya TANU ungejua kuwa TANU ilikuwa na wafadhili wanne matajiri: John Rupia, Dossa Aziz na Abdulwahid na Ally Sykes ndugu wawili.

Dossa Aziz alikuwa na malori saba ya mchanga na kokoto aliyorithi kutoka kwa baba yake Aziz Ali pamoja na kampuni ya ujenzi wa majumba.

Dossa aliipa TANU gari yake ya kwanza iliyokuwa ikitumiwa na Nyerere.

Utajiri wa Sykes unafahamika na umedumu hadi leo.

Iko siku nitakuwekea hapa kisa cha kabati la fedha la Abdul Sykes lililokuwa liko wazi kwa TANU kuanzia 1954 hadi uhuru unapatikana.

Huyu Abdul Sykes ndiye aliyeishi na Nyerere nyumbani kwake Nyerere alipoacha kazi ya ualimu baada ya safari ya UNO 1955.

Mipango yote ya safari ikifanyika nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu.

Angalia picha ya nyumba hiyo ya Abdul Sykes iliyojengwa 1942 na hii iliyojengwa sasa.

(Hiki ndicho kilikuwa kituo cha mikutano yote ya siri ya TANU toka enzi za TAA).

Degree isingeweza kufanya haya na kuunda chama cha African Association 1929 na kuunda Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) 1933.

Wazalendo katika vyama hivi walianza harakati dhidi ya Waingereza miaka hiyo.

Sitaki kujirudia nimekueleza vipi Nyerere alichaguliwa na sababu zake.

Ikiwa huamini hakuna tatizo.
Nikueleze upate kujua.

Abdul Sykes 1953 alikuwa amekubaliwa kujiunga na Princeton University, New Jersey.

1707576108054.png

Nyumba ya Abdul Sykes aliyosihi Nyerere 1955
1707576217348.png

Nyumba ya Abdul Sykes kama ilivyo hivi sasa
 
Hilo dini linafundisha chuki bwana unafikir hatujui
Ash...
Uislam ungefundisha chuki Nyerere asingekuwa kiongozi wa TANU.

Angalia picha hizo hapo chini Nyerere yuko na watu gani na ikiwa huwajui hao ni nani uliza.

Unaona chuki na uadui hapo?

1707575630058.png

Baraza la Wazee wa TANU 1957
1707575705760.png

Safari ya kwanza UNO 1955
1707575827251.png

Wakati wa kupigania uhuru miaka ya 1955/56 Dodoma
1707576406300.png
 
Walianzisha harakati za kudai uhuru sawa lakini hawakuwa na elimu Dunia ndio maana wakamhitaji mtu anayeona mbali mwenyeelimu ya kutosha yaani Kambarage wa Butiama
Usijidanganye.

Elimu yoyote ile ni ya duniani.

Akhera kuna moto au pepo kwa utayoyachuma duniani.
 
Wasichana wa kiislamu wamekamatwa wakiwa wamefungiwa kwenye nyumba Dodoma inayosadikika kuwapa elimu ya dini.

Wapo zaidi ya mabikra 200, wanakula na kunywa bure kwa siri kubwa sana.

Wameambiwa wanafundishwa dini, ukweli haujuikani lakini maagizo ya mkuu wa mkoa yanatia shaka hasa baada ya kutoa maagizo mepesi.

Mkuu wa mkoa alitakiwa atonyeshe hao wamilki, atuambie namna wamewapata hao wasichana bikra,mwazazi wao na taarifa nyingine.

Huenda tunaambiwa kila siku watu wamepotea tuna hangaika kuwatafuta kumbe wahusika wapo na hatupewi taarifa.
Ndugu yangu, waziri mpendwa Doctor GWAJIMA naomba utusaidie kuhusu hawa watoto!

View attachment 2896255
Wapi habari imetaja 200?

Hiyo ni sifa kubwa tena kubwa sana mabinti kutunzwa na kusomeshwa dini na bikra zao. Au Ulitaka wasiwe bikra?
 
Hawa wengi wao wanawatoa Kondoa .. Kuna maeneo kule watu hawajui chochote Cha Dunia zaidi ya Uislam.. hata wakiona mtu wa Dini nyinginewanadhangaa mno..
Kuna Mwalimu Mkristu alipangwa kufundisha huko alipata shida sana!
Kuna chema cha dunia zaidi ya Uislam?

Au kwako wewe masomo ya kufundisha watoto namna ya kuvalisha wanaume kondom kuanzia shule ya msingi ndio ya maana?
 
Hata mimi nimesikitika dana mabinti kuwachishwa masomo ya dini yao kabla hawajahitimu.
Mabikra waachwe wasome ilm zote, ilm duniya na ilm akhera. Tatizo ni pale maustadh wanapolazmisha wapate ilm akhera pekee.
 
Wapi habari imetaja 200?

Hiyo ni sifa kubwa tena kubwa sana mabinti kutunzwa na kusomeshwa dini na bikra zao. Au Ulitaka wasiwe bikra?
Pitia youtubue, nikiwaka hapa mods wanaondoa, labda issue za copyrights.
 
Back
Top Bottom