LiverpoolFC
JF-Expert Member
- Apr 12, 2011
- 11,483
- 3,369
Hebu niwekeni sawa wana JF, kwani daraza la saba na Form four huwezi kuwa mbunge???
Na kama nimeishia form four na profile ya bunge inasema STD 7 ni kosa la nani??
Ni kweli kabisa, ila kwenye story hii sijaona utata mkubwa kama ulivyoelezwa kwenye headline.
Kama sijakosea ili kuwa mbunge wa TZ inatakiwa uwe raia halali umri kuanzia 18yrs ujue kusoma na kuandikausiwe ulikwisha hukumiwa kwa kosa la jinai----mengine tusaidieni wengi sana humu hatuelewi zaidi ya kupiga kelele urithi mwingine tuliojaaliwa na mwenyezi MUNGU
Elimu ya Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini, GODBLESS LEMA aliyoieleza Mahakamani wakati ya kesi inayomkabili kufuatia ushindi wake wa Ubunge jimboni humo ni tofauti kabisa na ile iliyoko kwenye profile yake iliyooneshwa kwenye tovuti ya Bunge. Aidha hakuna ukweli wa moja kwa moja wa CHUO ambacho Mh. huyo mwenye Mbwembwe sana alichosomea.
Kuna Pro-Chadema mmoja aliniambia Lema, ana Bachelor of Laws alichukuwa pale University of Dar es Salaam.
WanaJF, kuna utata mkubwa sana wa taarifa za wabunge zilizopo katika kumbukumbu za bunge. Nadhani ni uzembe wa kitengo cha uchapaji unaoendekezwa na bunge lenyewe. Kwanza hawana utamaduni wa ku update profile za wabunge.
Hata hivyo kuna baadhi ya wabunge wameshatoa taarifa juu ya kukosewa kwa taarifa zao, na bado kitengo hicho kimeshindwa kufanya marekebisho muafaka. Hivyo taarifa nyingi zinazohusu wasifu wa wabunge kwa mujibu wa kumbukumbu za Bunge sio RELIABLE
Kwani niulize ndugu zangu wana Jamii Forums, Elimu anayotakiwa kuwa nayo Mbunge ni ipi??maana naona kama tuna make so much of a big issue kuhusu Elimu za wawakilishi wetu.Kama mtu ana elimu ndogo ya darasani lakini anatuwakilisha vizuri sio tatizo, maana wapo wenye elimu kubwa zenye distinction lakini hawana wanachotusaidia zaidi ya kutufanya tunazidi kuwa maskini. Nchi yetu ina rasilimali za kutosha lakini wawakilishi wetu waliosoma hakuna wanachotusaidia zaidi ya kujisaidia wao binafsi.Let's be serious and concentrate on key issues ambazo zitatukomboa kutoka kwenye umaskini na ukoloni mambo leo. Tuliukataa ukoloni lakini sasa tumeurudisha kwa mlango wa nyuma, nadhani ni muhimu zaidi.Ahsanteni kwa kunielewa.
Hii thread yako haina mashiko hasa kwa hali ya sasa ya mtanzania ilivyo,awe ni darasa la saba,ngumbaru au level ya PHD Lema ni mbunge mteule wa Arusha mjini! Msubiri Ngongo mkereketwa wa Lema atakusaidia
Kaka hili changa la macho, credit zake za form IV hazimruhusu kugusa MLIMANI, hata kuwa mfagiaji wa mabweni hawezi, ni udhalilishaji kusema lema kasoma MLIMANI na uombe msamaha.