Chakaza
Platinum Member
- Mar 10, 2007
- 41,034
- 74,732
Jana nimesikiliza kwa makini sana wasifu wa aliyekuwa Makamu wa kwanza wa Rais na Waziri mkuu marehemu Cleopa Msuya.
Nilibaki mdomo wazi baada ya kusikia baadhi ya SIFA zake zikisemwa mbele ya Rais na viongozi wengine wa serikali na CCM.
Nilivutiwa sana na kauli mbili ambazo zilionyesha alikuwa ni mwanachama wa CCM asiyekuwa na tabia za hawa wanaccm tuwajuao na nina hakika jana kuna aibu fulani viongozi waliokuwepo pale walijisikia mioyoni mwao.
1. Watoto walikiri kabisa kuwa Baba yao aliwakataza kabisa kutumia jina lake katika kutafuta maisha yao na kuyaendesha. Hii ni kinyume na watoto wa viongozi hawa wa sasa ambao mpaka serikalini wanatoa amri au kugawa vyeo yaani mf. Mtoto wa mama au unanijua mimi?
2. Nchimbi Katibu mkuu wa CCM jana kasema wazi kuwa yeye na Warioba walijadili sana tabia yake ya kupenda kusikia mawazo ya wengine na hakuwa ANA KASIRIKA kusikia mawazo mbadala, tofauti kabisa na haya tuonayo kwa sasa.
Utekaji, vipigo vya wapinzani, kuharibu uchaguzi na kubambikiana kesi ni tabia inayotokana na KUCHUKIA mawazo mbadala.
Hakika marehemu Msuya alikuwa Mwanachama wa CCM ambaye hakuwahi kuwa na Tabia za Kiccm ambazo kwa sasa ni desturi yaani Ubinafsi, chuki, ukatili na uongo dhidi ya wengine.
Rest in peace mzee Msuya, kampe salamu Julius na mwambie chama chake alicho kiasisi kwa sasa sio kile kinacho jali utu tena.