Raia mdogo
JF-Expert Member
- Jan 5, 2018
- 1,387
- 1,518
Inasikitisha kamanda kufananishwa na wahalifu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Pale kwake tulikuwa tunaenda sana miaka hiyoAna nyumba maili 6 moshi na ndio huko huko walienda kummaliza mbele ya geti lake akishuka garini.
nilikuwa mdogo kipindi hicho ndugu wakaenda msibani mi nikabaki kuangalia katuni
Ex DG wa usalama anaheshikimika sana kama The late Dr. Lawrance Gama, hawa walitoka Jeshini japo na yule coronel Apson naye alitoka huko, hao wanaheshimika sana pale Makumbusho.
Vipi kuhusu ushawishi wake kwenye vyombo vya Usalama na medani za kisiasa??
Mkuu nashukuru sana kwa hizi nondo zenye uhakika wa kipekee kabisa. Binafsi nimejifunza mengi sana na natumai wadau wengi watajifunza mengi pia kutoka kwenye hili andiko lako maana limejaa ushahidi wa kutosha. Ahsante sana MkuuOooh sorry mr Malcom Lumumba for this late reply
Kombe alikuwa na ushawishi mkubwa sana jwtz na Usalama wa taifa kutokana na career yake, uwezo na ufanisi pamoja na akili nyingi mpaka kufikia katika ripoti zake za kijasusi CIA walimdescribe kama "Bright and hardworking''.
Ushawishi mkubwa jeshini ni kutokana senior command positions alizotumikia kwa weledi na umahiri nikianza ukamanda wake katika vita ya Kagera ambapo alikuwa ni mmoja kati ya makamanda wa Brigade waliofanya vizuri mpaka kupewa promotion kwenda cheo cha meja jenerali, alipata umaarufu huo mkubwa kwa jina la kamanda "ngono"
Sio hapo tu , miaka ya themanini Kombe alipewa madaraka ya chief of staff ambayo ni madaraka makubwa sana jeshini baada ya CDF, na hii ni akiwa na rank ya major general.
Alihamishiwa Usalama ambako huko nako alianza U DG akiwa na rank ya major General, hii ni baada ya kuwa mnadhimu mkuu JWTZ
Baada ya kufanya vizuri katika ukurugenzi TISS akapandishwa cheo kuwa Luteni jenerali, operations zimefanywa nyingi chini yake na kipindi pia nacho akiwa mkuu wa usalama kulikuwa na mambo mengi.Umaarufu wake ni mkubwa sana huko usalama kwani kawa mkuu wa usalama chini ya marais watatu(Nyerere, Mwinyi na Ben)
Kisiasa kwa kweli sidhani sana sababu makamanda wa weledi na siasa sawa na maji na mafuta isipokuwa wabishi kama Rtd Gen Mboma. Ila alipata umaarufu sana huko kwao Uchagani/kanda-hiyo labda hii political wise huko kwao huwaambii kitu, generally miaka hiyo(1990's) watu wazima wanaofuatilia mambo ya nchi hii hamna aliyekuwa hamjui au kutomkubali huyu General. Ila Kwa umaarufu na ushawishi huyu General Kombe ni zaidi ya zaidi