Wasifu wa Lowassa unataja aligombea urais wa JMT 2015 lakini hausemi aligombea kwa chama kipi. Je, kuna wivu wa CCM kwa CHADEMA hata msibani?

Nafikiri watu wa chini ndiyo wenye matatizo Rais hana shida kabisa, na anapigania maelewano mama wa watu,pengine hata haya yanayotokea ni mtu mmoja au kikundi kinamchafulia Rais aonekane R4 zake hazifanyi kazi wakilenga 2025. Hapa kuna kazi kweli kweli. si ajabu Rais ndiye aliyetoa na muda wa Mbowe kuongea kwa busara zake.
 
Sijui kwanini watu hawapendi kuzungumza ukweli jinsi ulivyo; ukweli kwamba hayati Lowassa alikuwa nguzo kubwa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi mwaka 2015 ndani cha CHADEMA hauwezi kufichwa.

CHADEMA ndio waliokuwa walezi wakubwa wa kisiasa wa nyakati za mwisho za hayati Lowassa na ukweli utabaki hivyo.

Je, huu ni wivu wa kisiasa wa CCM dhidi ya CHADEMA?
Mbona CCM hawalalamiki kwamba msoma wasifu hajataja chama chochote? Kwani lazima kutaja chama?
 
Ni kweli, hasa kama kitu chenyewe ni ukweli unaoumiza. Mfano mtu kafa kwa HIV, huwezi kuandika hata kama ni ukweli maana unaumiza na kutia fedheha. Lakini kutoandika ukweli hakuuondoi.
Kwahiyo ni fedheha kutaja kwamba marehemu aligombea urais kupitia Chadema? Kwamba ni sawa na kusema marehemu kafa kwa HIV?
 
Sasa wasiposema watabadili nini? Binafsi hadi kura nilimpigia kabisa.
Watuue kabisa tuliokuwepo 2015 kufuta kumbukumbu kiukamilifu.
 
Katika Moja ya jambo la aibu alilofanya Marehemu ambalo linaria dosari utumishi wake serikali ni hilo.

Amepewa nafasi Mbowe ameeleza. Malalamiko ya nini?
 
Sijui kwanini watu hawapendi kuzungumza ukweli jinsi ulivyo; ukweli kwamba hayati Lowassa alikuwa nguzo kubwa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi mwaka 2015 ndani cha CHADEMA hauwezi kufichwa.

CHADEMA ndio waliokuwa walezi wakubwa wa kisiasa wa nyakati za mwisho za hayati Lowassa na ukweli utabaki hivyo.

Je, huu ni wivu wa kisiasa wa CCM dhidi ya CHADEMA?
Ni wivu wa matyako wazi
 
Sijui kwanini watu hawapendi kuzungumza ukweli jinsi ulivyo; ukweli kwamba hayati Lowassa alikuwa nguzo kubwa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi mwaka 2015 ndani cha CHADEMA hauwezi kufichwa
Ndo maana huwa naamini ccm na upinzani wapo pamoja au ccm wanaijua siasa. Kama kweli ccm hawakutaka chadema itajwe kwanini wampe nafasi kiongozi wa chadema kuzungumza? Kama ilikuwa lazima azungumze kwanini wasiitaje chadema?

Inshort tushapewa hoja sasa tuishi humo. Ni rahisi tu 'usiitaje chadema kwenye wasifu wa marehemu halafu mbowe apewe nafasi aitaje mjadala uibuke tuendelee na mambo yetu mengine.

Ukiwa na jamii inayohoji mambo muhimu ni ngumu sana kutawala ila ukiwa na jamii inayohoji mambo yasiyo muhimu kazi yako ni kuwapo hizo hoja wazihoji halafu inakuwa rahisi kweli kutawala.
 
Sio nguvu za social media hizo?
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Back
Top Bottom