Wasifu wa Rais Samia Suluhu Hassan

Nataka tuingie karne ya 21 lakini bado tunaishi maisha waliyoishi wenzetu karne ya 18. Sasa hao wasomi wana faida gani?
Hata kufikiri kidogo huwezi? Hao "wenzenu wa karne ya 18" hata hujui iliwachukuwa muda gani kufikia hapo walipofika?

Wewe unadhani ilitokea tu mara vuuu, wakawa kama walivyo leo?
 
Huwezi kuwakwepa watu wa nje hilo ndio tatizo. Alishindwa Nyerere na uwezo wake wote wa kufikiri na kujenga hoja hatakuja kuweza rais mwingine yoyote.

Na huwezi kuishi kwa kujitenga, utakosa fursa nyingi za uwekezaji. Utalii unaongezeka sana baada ya Royal Tour.
 
Rais Samia ni msomi mzuri tu, huu uzi umeandikwa na wale wenye donge wanapomuona mwanamama ana cheo cha juu kabisa Tanzania.
 
Rais Samia ni msomi mzuri tu, huu uzi umeandikwa na wale wenye donge wanapomuona mwanamama ana cheo cha juu kabisa Tanzania.
Hapo sawa, kama ni hivyo. Lakini mbona uendeshaji wake wa serikali una tashwishi nyingi? Mbona hajiamini? Kwa nini haamini kwamba Tanzania itafanikiwa tu kwa kutumia siasa na sera za maendeleo ya kujitegemea, na wala siyo kujikomba ughaibuni akitafuta hisani, fadhila, misaada na mikopo, huku kuwadhalilisha Watanzania, na mwishowe taifa kuishia kunyonywa zaidi?

Ndiyo maana wazalendo bila shaka wameamua kuhoji kiwango na ubora wa elimu yake.
 
Huyu na Magufuli na Kikwete wote elimu Yao ni ya kuunga unga tu kwahiyo hawana usomi wowote tena Bora na Kikwete kidogo.
Lakini lazima turejee maana halisi ya elimu ya kweli. Wakati ambapo mie ni mdau, mbia, na msoda wa elimu, sina mahaba na elimu tu ya darasani ambayo haijipambanui katika ufanisi wa maisha halisi na utendaji.

Nadhani mtihani wa kweli unaoonesha kwamba mtu ana elimu, amesoma na kupata maarifa yenye tija, ni matumizi ya elimu husika uraiani.

JK, JPM, na SSH (plus wengineo), wanaweza tu kupimwa kihalali kwa kigezo hiki.

Angalia mfano mmoja tu kuhusu wasaidizi wa SSH. Hivi unaanzaje kumtoa kiongozi hodari kama Lukuvi kwenye Wizara ya Ardhi? Hata kama, tuseme, kwa kukiakiza hoja, Lukuvi angekuwa na makosa 99 kwa 100, bado angefaa saa kuendelea na wizara husika.

^Elimu^

^Elimu^

^Elimu^~ Alisema ENL.

Inaweza isiwe elimu ya makaratasi fulani-fulani, per se, anayokosa Bibie, lakini elimu ya uzalendo, elimu ya kutambua kwamba zaidi ya 80% ya Watanzania ni fukara, elimu ya kutambua kwamba UJINGA, MARADHI, na UMASKINI--maadui aliopambana sana JKN ili kuwatokomeza, hivi sasa wameshamiri kama jana!

Elimu ya kutambua kwamba hakuna mjomba wala shangazi atakayetoka Ulaya ili kuyapambania maendeleo ya nchi yetu.

Narudia tena, kuna ukasisi mkubwa kuhusu elimu kwa mtu mwenye akili timamu asiyetambua na kutumikia mahitaji mahususi ya wananchi. Hivi unawezaje hata kufurahia kiti cha urais ilhali wapo mamilioni ya watu wako kila kona ambao hata hawajui watakula nini leo mchana? Maji? Afya? Elimu yao? Furaha? Maendeleo kijumla?

Nasema hivi, hakuna elimu hapo. Hiko ni kitu kingine, siyo elimu. Nyerere alisema elimu inakomboa fikra na utu na kuleta maendeleo himilivu. Kwetu hapa Tanzania, elimu inafanya kinyume cha haya. Halafu mnaleta habari za CV? Nonsense!
 
Born 60 .. kazi 77 ...akiwa na miaka 17 tayari ajira serikalini na bado unasema alisoma kozi mbali mbali ... zilikuwa kozi za week week nini
 
Hakuna nchi inayoweza kuwa kama kisiwa, siasa za hayati JPM zilikuwa na matatizo.

Ukiongelea sana kujitegemea pia unakuwa unaficha ubaguzi ule ule walionao wazungu kwa kigezo cha kutukuza uafrika wako.

Samia alikuwa mwerevu kwa kumpa yule mama wizara ya mambo ya nje, kuifufua diplomasia ya kiuchumi tofauti kabisa na Profesa Kabudi.
 
Hata kufikiri kidogo huwezi? Hao "wenzenu wa karne ya 18" hata hujui iliwachukuwa muda gani kufikia hapo walipofika?

Wewe unadhani ilitokea tu mara vuuu, wakawa kama walivyo leo?

Nyerere si alisema siye tunakimbia wengine wanatembea? Hizo mbio zote za miaka 60 tangu tupate uhuru tumeshindwaje kuwafikia wanaotembea?
 
"Walijaliwa watoto wanne.

Mmoja kati ya wanawe Wanu Hafidh Ameir (1982), ni mwakilishi maalum katika bunge la Zanzibar".
Ni nani mwenye jukumu la ku update hii CV humu jukwaani!!?
Mbona hao watoto wengine haisomeki wapo wapi/ wana nafasi gani!!??
Ritz tafadhali njoo uipange upya huu wasifu uliouanzisha hapa jukwaani ili uweke rekodi sawa.
 
Born 60 .. kazi 77 ...akiwa na miaka 17 tayari ajira serikalini na bado unasema alisoma kozi mbali mbali ... zilikuwa kozi za week week nini
Kumbuka tu kwamba miaka ile ya 70 ukimaliza form 4 tu kazi ziko tayari. Kujiendeleza inakuja baadae ukiwa kazini.

Mbona hata mimi nilimaliza form 6 nikiwa miaka 17 na miaka 18 nimeanza kazi baadae ndiyo nikaenda University.
 
Nani kasema kuishi kwa kujitenga kama siyo kutafuta upotoshaji wa hoja.

Nyerere alishindwa nini, kwenda nje, mbona kama unajichanganya mweyewe!

Nyerere hakwenda nje kutafuta watu wa nje walete maendeleo Tanzania.
 
Nyerere si alisema siye tunakimbia wengine wanatembea? Hizo mbio zote za miaka 60 tangu tupate uhuru tumeshindwaje kuwafikia wanaotembea?
Hivi hukuona tulipoanzia 1961, au hata historia huwezi ukaisoma na kuielewa?
 
Nani kasema kuishi kwa kujitenga kama siyo kutafuta upotoshaji wa hoja.

Nyerere alishindwa nini, kwenda nje, mbona kama unajichanganya mweyewe!

Nyerere hakwenda nje kutafuta watu wa nje walete maendeleo Tanzania.
Sera za Nyerere zilikufa kitambo tu. Kubali au kataa huwezi kuendesha uchumi kwa kutegemea nguvu kazi hii ya kibongo peke yake.

Tungekuwa na jeuri ya kujitegemea tusingetaifisha mashirika ya umma zaidi ya 50. Tusingekuja na dhana hizi za kuingia ubia.
 
Mbona ni kama huelewi, au unapenda sana kupotosha uonekane una hoja?

Nani kasema "tutegemee nguvu kazi hii ya kibongo pekee", na ni wapi uliposikia Nyerere akisema hatuwezi kushirikiana na watu wengine toka nje katika maendeleo yetu?

Lakini jukumu ni letu, na hatuwezi kamwe kutegemea kupata maendeleo kwa kwenda huko kuyatafuta yaletwe hapa.

Hilo swala la mashirika unalitumbukiza hapa pasipo kujua maana yake ni nini. Kwani ni Tanzania pekee ndiko mashirika ya umma yalipokuwa?
 
Anaendelea kuupiga mwingi sisi tuendelee kukosoa na kulalama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…