Wasifu wa Rais Samia Suluhu Hassan

Wasifu wa Rais Samia Suluhu Hassan

Shida ya wabongo ndo hii sasa, wewe umeombwa CV ya SAMIA badala ya kuileta umeanza kuleta porojo za Mugabe.

Kwahiyo kwa hoja yako unataka tuamini kwamba Samia hana kisomo ila anaweza kuongoza? Okay tumekubali, lakini tunataka CV yake kama ipo.
Mtoa hoja na wewe mnaonyesha upumbavu wenu hapa, tunaosoma to understand, kitu ambacho ndio nakifanya, utaona lengo la uzi huu ni kutaka tumwone our president hajaenda shule, angetaka cv ya president angeipigia simu ikulu or google it,na pia why uhusishe cv yake na PS wa NGO!,huu ni upumbavu mkubwa usiotibika na wala sio ujinga
 
Hili alilizungumza yeye mwenyewe alirudishwa nyumbani mpaka alipofik8sha 18 ndipo akaendelea na kazi. Acheni nongwa.
"Nongwa", unanikumbusha Ile kauli ya marope aliulizwa swali lingine, akajibu lingine.
 
Ana mwaka 1 madarakani kila kitu bado ni masalia ya Uongozi wa Magu, uraisi wake utaanza kuonekana kuanzia 2024/25, hakuna kitu kipya alichokianzisha uniondoa madarasa ya mkopo wa World Bank na imf!
Sasa kama uongozi wake haujaanza kuonekana mbona anaanza kukosolewa sasa, anakosolewa kwa lipi wakati uongozi bado ni wa awamu iliyopita?
 
Kwamba kila mwenye shule ni lazima atawale? Hivi hizi hoja nyingine huwa mnatoa wapi aiseeh.

Tunajua kwamba tunaongozwa na asiye na shule kwasasa (kama ulivyodai) ila yupo pale kwa mujibu na sio kwa ridhaa ya watz, hakuna Mtz anaejielewa ambaye angekubaliana na hilo swala, maana ndiyo linalotutesa mpaka sasa.
Halina haja ya kukutesa wakati mlishangilia alipoteuliwa kuwa mgombea mwenza wa JPM na mkawapa kura 2015 na 2020. Au hamkuelewa maana ya mgombea mwenza? Kwa sasa nawashauri mtulie tu muuguze maumivu.
 
Bi Samia Suluhu alizaliwa Januari 27, 1960 visiwani Zanzibar. Alisomea shule za msingi za Chawaka (Unguja), Ziwani (Pemba) na Mahonda (Unguja) na kati ya 1966 na 1972 na kisha akasomea masomo ya upili Ngambo, Unguja (1973-1975) na Lumumba, Unguja (1976).

Alisomea kozi mbalimbali hadi akafikia kupata shahada ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Southern New Hampshire nchini Marekani.

Kazi
Aliajiriwa kama mchapishaji katika serikali ya Zanzibar mwaka 1977 na akapanda ngazi hadi kuwa afisa wa mipango serikalini kati ya 1987 na 1988.

Alihudumu pia kama meneja wa mradi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) Zanzibar kati ya 1985 na 1997, na pia kama meneja mkurugenzi wa Mwamvuli wa NGO 1998 hadi 1999.

Bi Samia anasema kuwa njia yake ya ufanisi haijakuwa rahisi kama inavyodhaniwa.

''Safari yangu katika siasa imekuwa njia ndefu na yenye tija.''

Kimsingi ufanisi wangu katika siasa za Tanzania umetokana na uweledi na umakini katika kila jambo ninalolifanya.''

''Sio rahisi kuwajibikia familia yako wakati huohuo ukiendelea na maisha ya siasa elimu na majukumu mengine ya kikazi," anasema Bi Samia.

Familia
Aliolewa mwaka wa 1978, kwa Bw Hafidh Ameir, ambaye wakati huo alikuwa afisa wa Kilimo .

Walijaliwa watoto wanne.

Mmoja kati ya wanawe Wanu Hafidh Ameir (1982), ni mwakilishi maalum katika bunge la Zanzibar

Siasa
Alijiunga na siasa mwaka wa 2000.

Wakati huo alijiunga na bunge la wawakilishi la Zanzibar kama mjumbe maalum.

Haikuchukua muda mrefu nyota yake ikaanza kung'aa na akateuliwa kuwa waziri na rais Amani Karume, akipewa wadhifa wa Waziri wa Leba, Jinsia na Watoto.

Alitumikia taifa hadi mwaka wa 2005 alipochaguliwa tena na kuteuliwa upya kama waziri, wakati huu akipewa wizara ya Utalii, Biashara na Uwekezaji katika serikali ya visiwani.

Mwaka wa 2010 alichaguliwa kuwa mwakilishi wa jimbo la Makunduchi.

Punde tu akateuliwa na rais Jakaya Kikwete kuwa waziri wa maswala ya muungano katika serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akihudumu chini ya Makamu wa Rais Mohamed Gharib Bilal.

Machi mwaka 2014, aliwania na kuchaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa Bunge maalum la Katiba nmjini Dodoma. Bi Hassan alichaguliwa kwa kura 390 sawa na asilimia 74.6 na kumshinda mpinzani wake Amina Abdalla Amour ambaye alipata kura 126 sawa na 24%.

Julai mwaka 2015, Dkt John Magufuli alimteua kuwa mgombea mwenza.
===
First Name: Samia
Middle Name: Hassan
Last Name: Suluhu
Member Type: Elected Member
Political Party: Chama Cha Mapinduzi
Office Location: P.O. Box 3021, Dar Es Salaam
Office Phone: +255 774 010 203/+255 784 717 712 Office Fax:
Date of Birth 27 January 1960

EDUCATION
  • School Name/Location Course/Degree/Award Start Date End Date Level
  • Ziwani Primary School, Pemba CPEE 1970 - 1971 Primary School
  • Mahonda Primary School, Unguja CPEE 1972 - 1972 Primary School
  • Chwaka Primary School, Unguja CPEE 1966 - 1968 Primary School
  • Ngambo SecondarySchool, Unguja CSEE 1973 1975 Secondary School
  • Lumumba Secondary School, Unguja CSEE 1976 1976 Secondary School
  • National Institute of Public Administration, Lahore Pakistan Course 1989 1989 Certificate
  • Institute of Management for Leaders, Hyderabad, India Management Course 1991 1991 Certificate
  • Zanzibar Institute of Financial Administration, ZIFA Statistics 1983 1983 Certificate
  • Institute of Development Management, IDM, Mzumbe (Morogoro) Advanced Diploma 1983 1986 Advanced Diploma
  • Manchester University, London Postgraduate 1992 1994 Postgraduate Diploma
  • Open University Southern New Hampshire, USA M.A 2004 2005 Masters Degree

EMPLOYMENT HISTORY
  • Company Name Position From To
  • The Parliament of Tanzania Member - Makunduchi Constituency 2010 2015
  • Ministry of Tourism, Trade and Investment, Zanzibar Minister 2005 2010
  • Ministry of Labour, Gender Development and Children Minister 2000 2005
  • Mwamvuli wa NGO Managing Director 1998 1999
  • Revolutionary Government of Zanzibar Planning Officer 1987 1988
  • World Food Programme, WFP - Zanzibar Project Manager 1985 1997
  • Revolutionary Government of Zanzibar Typists (Typing Pool) 1977 1986

POLITICAL EXPERIENCE
  • Ministry/Political Party/Location Position From To
  • Chama Cha Mapinduzi, CCM Guardian (Warden) - North Unguja Region 2009 Todate
  • Chama Cha Mapinduzi, CCM Guardian (Warden) - North Pemba Region 2004 2007
  • Chama Cha Mapinduzi, CCM Member - National Executive Committee (NEC) 2002 Todate
dah hata cijaelewa mbona anama-certificate nyingi nyingi kumzidi Mugabe, halafu nyingi ni za ughaibuni naona kama tumepigwa hapo
 
Lkn Harvey ni Comedian na Ronaldo ni footballer na wamelipwa na kutajirika kwa kazi zao, sijaona ulitaka kumaanisha nini, kwamba unalinganisha Steve Harvey failure yake kwenye Elimu na kushindwa kumaliza Chuo na Raisi wetu au ?

Nijuavyo mimi Ronaldo au Harvey hawaongozi nchi ni watu binafsi, raisi yuko responsible na maisha ya watu zaidi ya milioni 45, hivyo hiyo siyo kamali ni maisha ya watu , na ni sawa kabisa watu hao kuhoji uwezo ikiwa ni pamoja na Elimu ya anayewaongoza!
Wangehoji hiyo elimu wakati amependekezwa kuwa mgombea mwenza NOT now. Au hawakuelewa maana ya mgombea mwenza. Kwa sasa haina maana tena. Watulie tu
 
Wangehoji hiyo elimu wakati amependekezwa kuwa mgombea mwenza NOT now. Au hawakuelewa maana ya mgombea mwenza. Kwa sasa haina maana tena. Watulie tu
Capacity ndo inafanya watu kuhoji.

Hadi sasa siamini kama mwigu na marope Bado wamekalia ofisi za UWAZIRI.

Siamini, ni TANZANIA pekee.
 
Anaupiga mwingi sana na elimu yake inayodharaulika humu ndani. Anao uwezo mkubwa wa kuwasiliana na watu wa mataifa mbalimbali, ni msikilizaji mzuri na anayekubalika kimataifa.

Elimu kuna wakati inakuwa ni mbwembwe tu za kishamba, Steve Harvey hana degree ya aina yoyote ni tajiri mkubwa USA.

Cristiano Ronaldo hana hata diploma, ni tajiri mkubwa anayelisha mamilioni ya watu na kusomesha wasio na uwezo duniani pote.

Punguzeni huu ushamba wa kupapatikia elimu.
Tofautisha utajiri na kuiongoza serikali. Mikataba unaijua? Sera na sheria? Huwezi kuwahimiza wananchi wajitutumue kutafuta kisomo, tena kwa gharama kubwa, ilhali wewe huoneshi mfano.

President anapaswa kuwa kielelezo ladhimu (impeccable role model) almost katika kila nyanja za bora.
 
Halina haja ya kukutesa wakati mlishangilia alipoteuliwa kuwa mgombea mwenza wa JPM na mkawapa kura 2015 na 2020. Au hamkuelewa maana ya mgombea mwenza? Kwa sasa nawashauri mtulie tu muuguze maumivu.
Ni kweli inabidi tutulie tuugulie haya maumivu ya kuongozwa na slow learner.
 
Back
Top Bottom