Wasifu wa Rais Samia Suluhu Hassan

Wasifu wa Rais Samia Suluhu Hassan

Habari wakuu, kama mada inahatarisha usalama wa nchi Moderator unaweza ukaufuta Uzi...
Nchi imefika mahali, tunaweza kuwekewa pandikizi toka popote na akawa ndiye kiongozi wanchi.
Kama hali hiyo siyo ya kutisha, tuiite ni hali ya namna gani hiyo?

Sijasema popote kuwa aliyepo sasa ni pandikizi, lakini inawezekana, kwa sababu hatujui alitokea wapi hadi akafika alipo sasa.
 
Hivi humu si ndio kila siku tunaambiwa ukikubali kuwa kiongozi ujuwe wewe u.ekuwa Public property hivi sio kujua wazazi wako tuu, bali hata maisha yako yote yalikuwaje toka utoto, umesoma wapi, tabia zako na katika maisha ya kawaida unapenda nini zaidi.

Maisha yako ya ndoa maana hatuwezi kuwa na kiongozi muhuni muhuni.

Sasa mbona kuna watu wanakuja juu kama ni jambo la siri linailizwa?

Ndio maana vinaandikwa vitabu kwa viongozi ili tuwajue, mbona hapa kama kuna woga?
 
Hivi humu si ndio kila siku tunaambiwa ukikubali kuwa kiongozi ujuwe wewe u.ekuwa Public property hivi sio kujua wazazi wako tuu, bali hata maisha yako yote yalikuwaje toka utoto, umesoma wapi, tabia zako na katika maisha ya kawaida unapenda nini zaidi...
Hizo nyingine utaambiwa tu ni highly classified information mkuu
 
Hii CV ya Rais wetu aielezi amezaliwa katika Familia gani!

Screenshot_20230522-184116_Chrome.jpg


 
Baba yake ni marehemu Mzee Suluhu Hassan.

Kaka yake ni Rashid Suluhu Hassan.

Dada yake ni Mgeni Suluhu Hassan.

Kwa mujibu wa makala hii ya BBC.

'Rais Samia alipenda kusoma, baba yetu alimhimiza afaulu’. Familia yake yaeleza​

  • Halima Nyanza
  • BBC Swahili
20 Aprili 2021
---

Akiwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya urais nchini Tanzania, Watanzania wamekuwa na hisia na mitazamo mbalimbali juu yake.

Lakini familia yake na watu wake wa karibu wanamfahamu vizuri kuliko ilivyo kwa watu wengine .

Rashid Suluhu Hassan ni kaka wa Rais Samia anasema jitihada anazozionesha hii leo , alianza tangu akiwa mdogo.

''Alikuwa mtu ambaye ana ari ya kusoma, bidii ya kusoma, alikuwa anapenda kuambiwa soma uwe kama mtu fulani, unamuona kaka yako hapa kwasababu Baba yetu alikuwa mwalimu, hivyo openness alikuwa nayo tangu zamani sana kwa hiyo watoto wake alikuwa akiwaachia nafasi''. Alisema Bw. Rashid.

Kaka yake anasema hakuna yeyote kwenye familia aliyewahi kuwa na ndoto kuwa siku moja atakuwa kiongozi...

''Hakuna mtu alijua.. kama ingewezekana kumfufua marehemu Mzee Suluhu sasa hivi akaamka ukamwambia leo Samia ni rais atakushangaa sana''. Alisema Bw. Rashid

Mgeni Suluhu Hassan ni dada wa Rais Samia anasema hakutarajia mdogo wake kushika nafasi ya juu kabisa ya uongozi nchini Tanzania.

Lakini pia hakushangazwa pia kutokana na rekodi yake ya kushika nafasi mbalimbali akipanda hatua kwa hatua.

''Kapita kwenye nyanja nyingi akianza tangu chini kabisa, mpaka akawa mbunge, kaliongoza bunge la katiba pia, anaweza na anajitahidi kuweza na ataweza''.

Tumsaidie na kumshauri vizuri.'' alisema Bi.Mgeni

Chanzo cha picha, Ikulu Tanzania

Chanzo: BBC

 
Taja jina la Baba Samia?
Aliyepewa Gari Mpya aina ya Benz iliyo chini sana miaka kadhaa iliyopita ili asipate shida Kuipanda kutokana na sasa kuwa ni Mzee mno huku akikosa hata Kumbukumbu za Kuwajua Wanawe baadhi wenye Vyeo kama alivyokuwa navyo Yeye kati ya mwaka 1985 hadi 1995.
 
Back
Top Bottom