Wasifu wa Rais Samia Suluhu Hassan

Wasifu wa Rais Samia Suluhu Hassan

Naomba nijue wazazi wa mama yetu, sijawahi kuona makala Wala popote wakioneshwa au kusimuliwa. Imekuwa tofauti Kwa watangulizi wake hayati Magufuli wazazi wake wamesimuliwa na mama yake Susanna picha zake zinajulikana, Mzee wake apumzike Kwa amani. Pia mama mlezi wa JK amehojiwa na akaweka wazi kuwa wazazi wa JK walitangulia mbele za haki, mwenyezi Mungu awarehemu.

Kwa mama, yeye alisema baba yake alikuwa mwalimu, hajataja zaidi.

Vyombo vya habari hakuna vilivyomtaja, kama yupo au ametangulia.

Naomba wakuu mnisaidie kujua jina la Babu yetu, tumpongeze Kwa kuzaa mtoto mzuri, anaongoza vizuri na hakika alistahili kuwa alivyo.
Babu mzee mwalimu Suluhu alikuwa bingwa wa kufundisha....ni marehemu kwa sasa waliobaki ni watoto wake akina mzee Rashid na wadogoze pamoja na wajukuu zake.......unataka tukawafukue makaburini muwahoji?!!!
 
Nchi imefika mahali, tunaweza kuwekewa pandikizi toka popote na akawa ndiye kiongozi wanchi.
Kama hali hiyo siyo ya kutisha, tuiite ni hali ya namna gani hiyo?

Sijasema popote kuwa aliyepo sasa ni pandikizi, lakini inawezekana, kwa sababu hatujui alitokea wapi hadi akafika alipo sasa.
Mkuu Kalamu uwezo wako wa kiuchambuzi ni mkubwa zaidi ya ulichokiandika hapa......

Mh.Rais SSH kwao ni Kizimkazi....amepita katika machujio ya kizalendo kufikia hapo alipo.....wamakunduchi ni wahadimu Kutoka huku bara... wamakunduchi wanajulikana kwa umakini wao na kuupenda uafrika.....wamakunduchi wanajulikana kwa UKOMREDI wao juu ya CCM......

Mh.Rais SSH ameshawahi kuwa mkurugenzi wa NGO's Zanzibar.....ameshawahi kuwa waziri wa utalii.....ameshawahi kuwa waziri wa muungano wa JMT......unadhani ni kwa bahati mbaya?!!!

Huyu mama yetu ni zaidi ya umuonavyo na umjuavyo....ni komredi haswa....kwake Tanzania kwanza kabla ya nafsi yake......

Wanaomjua watakuwa wanaisoma comment hii kwa furaha kubwa.....

#Aishi Milele Chifu Hangaya amen[emoji120]
 
Bi Samia Suluhu alizaliwa Januari 27, 1960 visiwani Zanzibar. Alisomea shule za msingi za Chawaka (Unguja), Ziwani (Pemba) na Mahonda (Unguja) na kati ya 1966 na 1972 na kisha akasomea masomo ya upili Ngambo, Unguja (1973-1975) na Lumumba, Unguja (1976).

Alisomea kozi mbalimbali hadi akafikia kupata shahada ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Southern New Hampshire nchini Marekani.

Kazi
Aliajiriwa kama mchapishaji katika serikali ya Zanzibar mwaka 1977 na akapanda ngazi hadi kuwa afisa wa mipango serikalini kati ya 1987 na 1988.

Alihudumu pia kama meneja wa mradi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) Zanzibar kati ya 1985 na 1997, na pia kama meneja mkurugenzi wa Mwamvuli wa NGO 1998 hadi 1999.

Bi Samia anasema kuwa njia yake ya ufanisi haijakuwa rahisi kama inavyodhaniwa.

''Safari yangu katika siasa imekuwa njia ndefu na yenye tija.''

Kimsingi ufanisi wangu katika siasa za Tanzania umetokana na uweledi na umakini katika kila jambo ninalolifanya.''

''Sio rahisi kuwajibikia familia yako wakati huohuo ukiendelea na maisha ya siasa elimu na majukumu mengine ya kikazi," anasema Bi Samia.

Familia
Aliolewa mwaka wa 1978, kwa Bw Hafidh Ameir, ambaye wakati huo alikuwa afisa wa Kilimo .

Walijaliwa watoto wanne.

Mmoja kati ya wanawe Wanu Hafidh Ameir (1982), ni mwakilishi maalum katika bunge la Zanzibar

Siasa
Alijiunga na siasa mwaka wa 2000.

Wakati huo alijiunga na bunge la wawakilishi la Zanzibar kama mjumbe maalum.

Haikuchukua muda mrefu nyota yake ikaanza kung'aa na akateuliwa kuwa waziri na rais Amani Karume, akipewa wadhifa wa Waziri wa Leba, Jinsia na Watoto.

Alitumikia taifa hadi mwaka wa 2005 alipochaguliwa tena na kuteuliwa upya kama waziri, wakati huu akipewa wizara ya Utalii, Biashara na Uwekezaji katika serikali ya visiwani.

Mwaka wa 2010 alichaguliwa kuwa mwakilishi wa jimbo la Makunduchi.

Punde tu akateuliwa na rais Jakaya Kikwete kuwa waziri wa maswala ya muungano katika serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akihudumu chini ya Makamu wa Rais Mohamed Gharib Bilal.

Machi mwaka 2014, aliwania na kuchaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa Bunge maalum la Katiba nmjini Dodoma. Bi Hassan alichaguliwa kwa kura 390 sawa na asilimia 74.6 na kumshinda mpinzani wake Amina Abdalla Amour ambaye alipata kura 126 sawa na 24%.

Julai mwaka 2015, Dkt John Magufuli alimteua kuwa mgombea mwenza.
===
First Name: Samia
Middle Name: Hassan
Last Name: Suluhu
Member Type: Elected Member
Political Party: Chama Cha Mapinduzi
Office Location: P.O. Box 3021, Dar Es Salaam
Office Phone: +255 774 010 203/+255 784 717 712 Office Fax:
Date of Birth 27 January 1960

EDUCATION
  • School Name/Location Course/Degree/Award Start Date End Date Level
  • Ziwani Primary School, Pemba CPEE 1970 - 1971 Primary School
  • Mahonda Primary School, Unguja CPEE 1972 - 1972 Primary School
  • Chwaka Primary School, Unguja CPEE 1966 - 1968 Primary School
  • Ngambo SecondarySchool, Unguja CSEE 1973 1975 Secondary School
  • Lumumba Secondary School, Unguja CSEE 1976 1976 Secondary School
  • National Institute of Public Administration, Lahore Pakistan Course 1989 1989 Certificate
  • Institute of Management for Leaders, Hyderabad, India Management Course 1991 1991 Certificate
  • Zanzibar Institute of Financial Administration, ZIFA Statistics 1983 1983 Certificate
  • Institute of Development Management, IDM, Mzumbe (Morogoro) Advanced Diploma 1983 1986 Advanced Diploma
  • Manchester University, London Postgraduate 1992 1994 Postgraduate Diploma
  • Open University Southern New Hampshire, USA M.A 2004 2005 Masters Degree

EMPLOYMENT HISTORY
  • Company Name Position From To
  • The Parliament of Tanzania Member - Makunduchi Constituency 2010 2015
  • Ministry of Tourism, Trade and Investment, Zanzibar Minister 2005 2010
  • Ministry of Labour, Gender Development and Children Minister 2000 2005
  • Mwamvuli wa NGO Managing Director 1998 1999
  • Revolutionary Government of Zanzibar Planning Officer 1987 1988
  • World Food Programme, WFP - Zanzibar Project Manager 1985 1997
  • Revolutionary Government of Zanzibar Typists (Typing Pool) 1977 1986

POLITICAL EXPERIENCE
  • Ministry/Political Party/Location Position From To
  • Chama Cha Mapinduzi, CCM Guardian (Warden) - North Unguja Region 2009 Todate
  • Chama Cha Mapinduzi, CCM Guardian (Warden) - North Pemba Region 2004 2007
  • Chama Cha Mapinduzi, CCM Member - National Executive Committee (NEC) 2002 Todate
Duuh kaanza kufanya KAZI akiwa na miaka 17 kwani chuo kamaliza na umri gani
 
Hivi humu si ndio kila siku tunaambiwa ukikubali kuwa kiongozi ujuwe wewe u.ekuwa Public property hivi sio kujua wazazi wako tuu, bali hata maisha yako yote yalikuwaje toka utoto, umesoma wapi, tabia zako na katika maisha ya kawaida unapenda nini zaidi.

Maisha yako ya ndoa maana hatuwezi kuwa na kiongozi muhuni muhuni.

Sasa mbona kuna watu wanakuja juu kama ni jambo la siri linailizwa?

Ndio maana vinaandikwa vitabu kwa viongozi ili tuwajue, mbona hapa kama kuna woga?
Mbona kila kitu kiko wazi....hivi wanaJF hamjishughulishi kuangalia mambo rahisi?!!!

Mh.SSH ni mmakunduchi wa kizimkazi....

Ni mhadimu Kutoka huku bara.... wahadimu walihamia huko miaka mingi iliyopita.....

Wamakunduchi WANAUPENDA uafrika.....

Wamakunduchi ni wazalendo kwa ASP na CCM.....

Mmakunduchi SSH amepitia chekecho kali kuwa hapo alipo....akili yake kali ,uzalendo wake wa kuigwa ,ari ,ujasiri na ukakamavu wake ulimfanya awe mkurugenzi wa NGO's Zanzibar....akawa mjumbe wa baraza la wawakilishi.... akawa waziri wa utalii....akawa waziri wa muungano wa JMT.......

Baba yetu anajulikana....wanawe wanajulikana.....dada na kaka zake wanajulikana.....

Karibu katika sherehe za kitamaduni za kuoga mwaka(mwakakogwa) mwezi wa 7 utapata majibu yako yote utakayo......

Siempre SSH amen[emoji120]
 
Baba yake ni marehemu Mzee Suluhu Hassan.

Kaka yake ni Rashid Suluhu Hassan.

Dada yake ni Mgeni Suluhu Hassan.

Kwa mujibu wa makala hii ya BBC.

'Rais Samia alipenda kusoma, baba yetu alimhimiza afaulu’. Familia yake yaeleza​

  • Halima Nyanza
  • BBC Swahili
20 Aprili 2021
---

Akiwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya urais nchini Tanzania, Watanzania wamekuwa na hisia na mitazamo mbalimbali juu yake.

Lakini familia yake na watu wake wa karibu wanamfahamu vizuri kuliko ilivyo kwa watu wengine .

Rashid Suluhu Hassan ni kaka wa Rais Samia anasema jitihada anazozionesha hii leo , alianza tangu akiwa mdogo.

''Alikuwa mtu ambaye ana ari ya kusoma, bidii ya kusoma, alikuwa anapenda kuambiwa soma uwe kama mtu fulani, unamuona kaka yako hapa kwasababu Baba yetu alikuwa mwalimu, hivyo openness alikuwa nayo tangu zamani sana kwa hiyo watoto wake alikuwa akiwaachia nafasi''. Alisema Bw. Rashid.

Kaka yake anasema hakuna yeyote kwenye familia aliyewahi kuwa na ndoto kuwa siku moja atakuwa kiongozi...

''Hakuna mtu alijua.. kama ingewezekana kumfufua marehemu Mzee Suluhu sasa hivi akaamka ukamwambia leo Samia ni rais atakushangaa sana''. Alisema Bw. Rashid

Mgeni Suluhu Hassan ni dada wa Rais Samia anasema hakutarajia mdogo wake kushika nafasi ya juu kabisa ya uongozi nchini Tanzania.

Lakini pia hakushangazwa pia kutokana na rekodi yake ya kushika nafasi mbalimbali akipanda hatua kwa hatua.

''Kapita kwenye nyanja nyingi akianza tangu chini kabisa, mpaka akawa mbunge, kaliongoza bunge la katiba pia, anaweza na anajitahidi kuweza na ataweza''.

Tumsaidie na kumshauri vizuri.'' alisema Bi.Mgeni

Chanzo cha picha, Ikulu Tanzania

Chanzo: BBC

[emoji2956]
 
Aliyepewa Gari Mpya aina ya Benz iliyo chini sana miaka kadhaa iliyopita ili asipate shida Kuipanda kutokana na sasa kuwa ni Mzee mno huku akikosa hata Kumbukumbu za Kuwajua Wanawe baadhi wenye Vyeo kama alivyokuwa navyo Yeye kati ya mwaka 1985 hadi 1995.
Ujinga wako utakutoka lini?!!!
 
Kuna mzee mmoja kwenye uzinduzi wa Ikulu mpya juzi Dodoma, alipewa kiti akae wakati viongozi wote walikua wamesimama pale nje wakiwa wanasubiri kumpokea Samia akague gwaride. Jina lake limenitoka yule mzee.
Ujinga huo
 
Back
Top Bottom