Wasimamizi wa mirathi ya Mengi wagoma kuhudumia watoto, waburuzwa mahakamani

Wasimamizi wa mirathi ya Mengi wagoma kuhudumia watoto, waburuzwa mahakamani

Kiturilo

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2021
Posts
708
Reaction score
2,859
Mirathi ya marehemu Dkt Mengi imezua balaa baada wasimamizi wake kuburuzwa mahakamani kwa tuhuma za kukataa kuwahudumia watoto wa Mengi aliozaa na Jacqueline Ntuyabaliwe.

Kesi hii imefunguliwa ikiwa mke huyo mdogo wa Mengi akiwa amezuiwa kukanyaga Kilimanjaro hata kwenda kusafisha kaburi la marehemu mme wake.

Kuna kila dalili hao watoto mapacha wa billionea Mengi wakaishi maisha ya dhiki na umasikini uliotopea ili hali baba yao amewaachia mali nyingi sana ikiwemo kampuni ya IPP Media, yote hayo yatasababishwa na tamaa za mali za ndugu na watoto wa mke mkubwa wa Dkt Mengi.

Source. Gazeti la mwananchi.

Pia, soma=> Wosia wa Mirathi ya Dkt. Reginald Mengi: Jacqueline Ntuyabaliwe adondokea pua

=====

Wasiamamizi wa mirathi ya aliyekuwa mfanyabiashara maarufu nchini Reginald Mengi wameburuzwa mahakamani wakidaiwa kukataa kuwahudumia watoto wa mfanyabiashara huyo aliowazaa na mkewe Jacqueline Ntuyabaliwe
Kesi hiyo imefunguliwa na Jacqueline katika Mahakama ya Watoto iliyoko katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam

Wasimamizi wa mirathi hiyo wanaokabiliwa na kesi ni mtoto wa marehemu, Benjamini Mengi.

Habari zambazo Mwananchilimezipata ni na kuthibitishwa na wakili wa mjane huyo, Audax Kahendaguza, kwa ridhaa ya mteja wake, katika shauri hilo la madai namba 50 la mwaka 2022, Jacqueline anadai matunzo ya watoto hao ikiwamo ada ya shule.

Anadai kuwa watoto hao walikuwa wakigharamiwa ada na baba yao pamoja na huduma nyingine zote walizostahili kutokana na kipato alichokuwa anakipata kwenye shughuli zake za kibiashara, ambazo kwa sasa zipo chini ya wasimamizi hao wa mirathi.

Anadai kuwa hata baada ya kifo cha baba yao, awali wasimamizi hao walikuwa wakwalipia ada na huduma nyingine japo mara mojamoja; kwamba sasa wameacha kabisa kuwalipia ada ya shule pamoja na huduma nyingine licha ya kuwaomba mara kadhaa.

Mawakili wa wadaiwa walieleza kuwa hawajaandaa majibu ya madai hayo kwa kuwa wateja wao wako mikoani huku mahakama ikiwataka kuwasilisha majibu yao Februari 17, mwaka huu siku ambayo pia kesi hiyo itatajwa tena.

Kesi hii iekuja wakati bado kuna mgogoro wa mirathi ya marehemu Mengi kati ya pande hizo mbili, kwani bado kuna shauri la mirathi linasubiri uamuzi.

Chanzo: Mwananchi

IMG_20220205_112616_518.jpg
IMG_20220205_112652_978.jpg
 
Huyo dada anashindwaje yeye kuwalea watoto wake...Yeye si amebaki na mikono, miguu, macho na ule uzuri wake aendelee tu kulea watoto vizuri kama alivyokuwepo baba yao, Huo ndio utakuwa upendo otherwise hata kwa baba yao alifuata mali tu..
 
Ndio akili za mwanamke mjinga, kipindi kile anaspend kwenye mahotel luxury Dubei pesa angaitumia kuiwekeza kwenye
real Estate Leo asingebaki analialia,

Wanawake wa bongo fleva na bongo movie wanapenda Sana show of wanazidiwa maarifa, ujanja na Shilole std 7 Igunga primary school?
 
Funzo kwa wasichana wa siku hizi wakome kudandia Ndoa za watu wenye ukwasi wao.

Huyo Ntuyabaliwe mwenyewe kapuyanga na wengi mno.

Isisahaulike kuwa alikuwa na kashfa ya kuhusishwa na mwarabu aliekuwa master mind wake akusafiri nae sambamba na Marehemu kwa siri.

Ukimuuliza hata historia kamili ya Marehemu haijui zaidi ya kukariri akaunti zake tu.

Mleta topic umeandika kimaslahi binafsi.
 
Kama ni kweli hao nao wana roho mbaya na uroho pamoja na tamaa za hizo mali.
Mali zote hizo wanapeleka wapi hadi wagome kuhudumia hao watoto zaidi tu nao watakufa na kuziancha kama alivoziacha mwenye nazo.
 
Back
Top Bottom