Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Utakuta aliye leta hii mada hapa ni huyo huyo mwanamke mwenyewe mwenye tamaa na mali ambazo hakuzitolea jasho yeye, hawa wadada wa sasa ni tatizo sanahuyo dada anashindwaje yeye kuwalea watoto wake...Yeye si amebaki na mikono, miguu, macho na ule uzuri wake aendelee tu kulea watoto vizuri kama alivyokuwepo baba yao, Huo ndio utakuwa upendo otherwise hata kwa baba yao alifuata mali tu..
Mirathi ya marehemu Dkt Mengi imezua balaa baada wasimamizi wake kuburuzwa mahakamani kwa tuhuma za kukataa kuwahudumia watoto wa Mengi aliozaa na Jacqueline Ntuyabaliwe.
Kesi hii imefunguliwa ikiwa mke huyo mdogo wa Mengi akiwa amezuiwa kukanyaga Kilimanjaro hata kwenda kusafisha kaburi la marehemu mme wake.
Kuna kila dalili hao watoto mapacha wa billionea Mengi wakaishi maisha ya dhiki na umasikini uliotopea ili hali baba yao amewaachia mali nyingi sana ikiwemo kampuni ya IPP Media, yote hayo yatasababishwa na tamaa za mali za ndugu na watoto wa mke mkubwa wa Dkt Mengi.
Source. Gazeti la mwananchi.
=====
Wasiamamizi wa mirathi ya aliyekuwa mfanyabiashara maarufu nchini Reginald Mengi wameburuzwa mahakamani wakidaiwa kukataa kuwahudumia watoto wa mfanyabiashara huyo aliowazaa na mkewe Jacqueline Ntuyabaliwe
Kesi hiyo imefunguliwa na Jacqueline katika Mahakama ya Watoto iliyoko katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam
Wasimamizi wa mirathi hiyo wanaokabiliwa na kesi ni mtoto wa marehemu, Benjamini Mengi.
Habari zambazo Mwananchilimezipata ni na kuthibitishwa na wakili wa mjane huyo, Audax Kahendaguza, kwa ridhaa ya mteja wake, katika shauri hilo la madai namba 50 la mwaka 202, Jacqueline anadai matunzo ya watoto hao ikiwamo ada ya shule.
Anadai kuwa watoto hao walikuwa wakigharamiwa ada na baba yao pamoja na huduma nyingine zote walizostahili kutokana na kipato alichokuwa anakipata kwenye shughuli zake za kibiashara, ambazo kwa sasa zipo chini ya wasimamizi hao wa mirathi.
Anadai kuwa hata baada ya kifo cha baba yao, awali wasimamizi hao walikuwa wakwalipia ada na huduma nyingine japo mara mojamoja; kwamba sasa wameacha kabisa kuwalipia ada ya shule pamoja na huduma nyingine licha ya kuwaomba mara kadhaa.
Mawakili wa wadaiwa walieleza kuwa hawajaandaa majibu ya madai hayo kwa kuwa wateja wao wako mikoani huku mahakama ikiwataka kuwasilisha majibu yao Februari 17, mwaka huu siku ambayo pia kesi hiyo itatajwa tena.
Kesi hii iekuja wakati bado kuna mgogoro wa mirathi ya marehemu Mengi kati ya pande hizo mbili, kwani bado kuna shauri la mirathi linasubiri uamuzi.
Chanzo: Mwananchi
View attachment 2108732View attachment 2108733
Mleta topic utakuta ndo yeye mwenyewe mwanamke tamaaFunzo kwa wasichana wa siku hizi wakome kudandia Ndoa za watu wenye ukwasi wao.
Huyo Ntuyabaliwe mwenyewe kapuyanga na wengi mno.
Isisahaulike kuwa alikuwa na kashfa ya kuhusishwa na mwarabu aliekuwa master mind wake akusafiri nae sambamba na Marehemu kwa siri.
Ukimuuliza hata historia kamili ya Marehemu haijui zaidi ya kukariri akaunti zake tu.
Mleta topic umeandika kimaslahi binafsi.
Watoto wake lazima watapata
Ameweka mpaka nakala.Angalia mwananchi wasijekukushtaki kwa kuwachafulia jina lao.
Hii sio haki kusema kweli....Noma.. sio poa kabisa
...Kama alikwishazaa ni sawa.... ila kama bado hajawahi kuzaa....azae tu hata akiwa na miaka zaidi ya 50.Hivi mengi aliwaza nini kuzaa uzeeni vile,tulikubaliana kuwa wanaume kuzaa mwisho miaka 5o
Yap!....ila hao watoto wana haki ya kurithi mali zilizoachwa na baba yao na mama yao ni lazima alisimamie hili.huyo dada anashindwaje yeye kuwalea watoto wake...Yeye si amebaki na mikono, miguu, macho na ule uzuri wake aendelee tu kulea watoto vizuri kama alivyokuwepo baba yao, Huo ndio utakuwa upendo otherwise hata kwa baba yao alifuata mali tu..
Ujengewe sanamuLadies, here is a lesson.
"Success is not sexualy transmitted like gonorrhoea"
Wameiandika kiudakuHii no habari, sio udaku Mkuu! Watoto kunyimwa mirathi ya baba yao kushitakiwa mahamani in Udaku? We we in upande.ulioshitakiwa?
Nasimama hapaYeye alipoenda kuzaa na mtu ambae tayari keshachuma mali na watoto wake wakubwa alitegemea nini? Kwanini asingezaa na kijana mwenzake wakaanza wote maisha from zero? Acheni tamaa
Kule chini habari nyingine mkuu, tubakishe akiba ya manenoHivi mengi aliwaza nini kuzaa uzeeni vile,tulikubaliana kuwa wanaume kuzaa mwisho miaka 5o
Msimamiz wa mirathi wa kina mengi ni ukoo wa kina mengi. Nimeuliza watoto wa mpakanjia wamezurimiwa na ukoo wa mpakanjia ama wa ukoo wa chifupa ama ukoo wa nani ?
Sijasema kupeleka moto nimesema kuzaa moto tupeleke mpaka kifutio kiisheKule chini habari nyingine mkuu, tubakishe akiba ya maneno
Utajiri una mambo sana huu usikute ni maagano kuwa apatecutajiri ila kizazi kisiendelee,motie alikufa akiwa kijana,hawa wengine dah unakufa na mihela hata mjukui hunaWatoto wakubwa sio rizki, mzee akaona isiwe tabu manake nisipoangalia kizazi changu kinaishia hapa...bora hata alivyowapata hao twins.
Mjane wapi sema jambazi lililotumia silaha za kibailojia kwa maana ya urembo wakeHapana hao wasimamizi wanapaswa watenguliwe usimamizi mara moja.
aliye stahili kuwa msimamizi ni mjane wa marehemu akisaidiwa na ndugu mwengine.
Lengo la hao wasimamizi naa ndugu ni kumdhulumu mjane na watoto wake.
wanawake mko wapi? mjane huyu Jaquline ananyanyaswa kiasi hiki wakati ana haki!!
Vyama vya kutetea Haki za wanawake mko wapi? taasisi na NGO mbalimbali mko wapi kinacho fanyika ktk sakata hili ni unyanyasaji wa kijinsia.
mfumo dume unakandamiza haki za mjane.
ndiye aliye kuwa anampa furaha marehemu.Mjane wapi sema jambazi lililotumia silaha za kibailojia kwa maana ya urembo wake