Wasimamizi wa mirathi ya Mengi wagoma kuhudumia watoto, waburuzwa mahakamani

Wasimamizi wa mirathi ya Mengi wagoma kuhudumia watoto, waburuzwa mahakamani

ndiye aliye kuwa anampa furaha marehemu.
hivyo anayo haki utake usitake.
Ndugu wa Marehemu wanataka kupora na kudhulumu Haki ya Mjane kwa kutumia mfumo dume kandamizi.
Kama kuna furaha sijui lakini pia alinpa stress zilizommaliza uhai wake yule mzee angebaki single au angeoa mzee mwenzake huenda angekuwa hai bado,dangote mpaka leo hana mke anajua hawa majambazi ni hatari
 
Pale aibu inapokupata kuingiza udini pasipostahili. Acha kukurupuka kuleta udini. Kesi za mirathi hazijali ni ndugu wala mtu baki. Iwe muislamu wala mkristo mambo yale yale.

Nimeshajibu swali lako la kusema kwenye uislamu hakuna longolongo,wamsaidie basi mtoto wa mpakanjia na wenzie

Swali hujajibu bali umepiga chenga kulijibu. Lisome tena swali hapa chini

Kwamba ukoo wa nani umemzulumu mtoto wa mpakanjia?
 
Funzo kwa wasichana wa siku hizi wakome kudandia Ndoa za watu wenye ukwasi wao.

Huyo Ntuyabaliwe mwenyewe kapuyanga na wengi mno.

Isisahaulike kuwa alikuwa na kashfa ya kuhusishwa na mwarabu aliekuwa master mind wake akusafiri nae sambamba na Marehemu kwa siri.

Ukimuuliza hata historia kamili ya Marehemu haijui zaidi ya kukariri akaunti zake tu.

Mleta topic umeandika kimaslahi binafsi.
huo ndio mshahara wa gold diggers.
 
Kila mtu anafahamu kwamba Huyo dada alimkuta mzee Mengi na mali zake.

Labda angedai kiasi kile kichopatikana wakati wa ndoa yao.

Ila hao wasimamizi wanapaswa kuangalia hao twins kwani ni sehemu ya familia yao.

Huyo mama sio lazima sana.
 
Ndio akili za mwanamke mjinga,kipindi kile anaspend kwenye mahotel luxury Dubei pesa angaitumia kuiwekeza kwenye
real Estate Leo asingebaki analialia,

Wanawake wa bongo fleva na bongo movie wanapenda Sana show of wanazidiwa maarifa,ujanja na Shilole std 7 igunga primary school?
Huyohuyo Shishi std vii "B" nyumba yake kaiweka ubaoni iuzwe.
 
Kama ni kweli hao nao Wana roho mbaya na uroho pamoja na tamaa za hizo mali.
Mali zote hizo wanapeleka wapi hadi wagome kuhudumia hao watoto zaidi tu nao watakufa na kuziancha kama alivoziacha kwenye nazo.
Asilimia 95% ya Mali zinapatikana kishirikina kwa iyo mwisho wake zinakuwa ivyo

Sent from my Nokia 1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Hapana hao wasimamizi wanapaswa watenguliwe usimamizi mara moja.
aliye stahili kuwa msimamizi ni mjane wa marehemu akisaidiwa na ndugu mwengine.


Lengo la hao wasimamizi naa ndugu ni kumdhulumu mjane na watoto wake.

wanawake mko wapi? mjane huyu Jaquline ananyanyaswa kiasi hiki wakati ana haki!!

Vyama vya kutetea Haki za wanawake mko wapi? taasisi na NGO mbalimbali mko wapi kinacho fanyika ktk sakata hili ni unyanyasaji wa kijinsia.
mfumo dume unakandamiza haki za mjane.
Unataka wanawake washirikiane kumpa mwanamke mwenzao hata visivyo halali yake. Atapata haki yake mahakamani. Hakuna Janja janja.
 
Naona wengi tumeivamia hii mada kwa hisia na mambo binafsi kuliko uhalisia.

Kwanza ni haki kwa watoto wa marehemu Mengi kusomeshwa na mali za marehemu baba yao.

Pili ni haki kwa Jackline Mengi kudai hilo jambo kisheria litekelezwa ipasavyo.

Tatu hatujui upande wa pili (wasimamizi wa mirathi) wana maoni gani katika hili.
 
Naona wengi tumeivamia hii mada kwa hisia na mambo binafsi kuliko uhalisia.

Kwanza ni haki kwa watoto wa marehemu Mengi kusomeshwa na mali za marehemu baba yao.

Pili ni haki kwa Jackline Mengi kudai hilo jambo kisheria litekelezwa ipasavyo.

Tatu hatujui upande wa pili (wasimamizi wa mirathi) wana maoni gani katika hili.
Hizo mali alichuma na mke mkubwa au na mke mdogo??
 
Mirathi ya marehemu Dkt Mengi imezua balaa baada wasimamizi wake kuburuzwa mahakamani kwa tuhuma za kukataa kuwahudumia watoto wa Mengi aliozaa na Jacqueline Ntuyabaliwe.

Kesi hii imefunguliwa ikiwa mke huyo mdogo wa Mengi akiwa amezuiwa kukanyaga Kilimanjaro hata kwenda kusafisha kaburi la marehemu mme wake.

Kuna kila dalili hao watoto mapacha wa billionea Mengi wakaishi maisha ya dhiki na umasikini uliotopea ili hali baba yao amewaachia mali nyingi sana ikiwemo kampuni ya IPP Media, yote hayo yatasababishwa na tamaa za mali za ndugu na watoto wa mke mkubwa wa Dkt Mengi.

Source. Gazeti la mwananchi.

=====

Wasiamamizi wa mirathi ya aliyekuwa mfanyabiashara maarufu nchini Reginald Mengi wameburuzwa mahakamani wakidaiwa kukataa kuwahudumia watoto wa mfanyabiashara huyo aliowazaa na mkewe Jacqueline Ntuyabaliwe
Kesi hiyo imefunguliwa na Jacqueline katika Mahakama ya Watoto iliyoko katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam

Wasimamizi wa mirathi hiyo wanaokabiliwa na kesi ni mtoto wa marehemu, Benjamini Mengi.

Habari zambazo Mwananchilimezipata ni na kuthibitishwa na wakili wa mjane huyo, Audax Kahendaguza, kwa ridhaa ya mteja wake, katika shauri hilo la madai namba 50 la mwaka 202, Jacqueline anadai matunzo ya watoto hao ikiwamo ada ya shule.

Anadai kuwa watoto hao walikuwa wakigharamiwa ada na baba yao pamoja na huduma nyingine zote walizostahili kutokana na kipato alichokuwa anakipata kwenye shughuli zake za kibiashara, ambazo kwa sasa zipo chini ya wasimamizi hao wa mirathi.

Anadai kuwa hata baada ya kifo cha baba yao, awali wasimamizi hao walikuwa wakwalipia ada na huduma nyingine japo mara mojamoja; kwamba sasa wameacha kabisa kuwalipia ada ya shule pamoja na huduma nyingine licha ya kuwaomba mara kadhaa.

Mawakili wa wadaiwa walieleza kuwa hawajaandaa majibu ya madai hayo kwa kuwa wateja wao wako mikoani huku mahakama ikiwataka kuwasilisha majibu yao Februari 17, mwaka huu siku ambayo pia kesi hiyo itatajwa tena.

Kesi hii iekuja wakati bado kuna mgogoro wa mirathi ya marehemu Mengi kati ya pande hizo mbili, kwani bado kuna shauri la mirathi linasubiri uamuzi.

Chanzo: Mwananchi

View attachment 2108732View attachment 2108733
Wakulaumiwa ni Mengi mwenyewe kwa usomi na exposure aliyokuwa nayo inashangaza sana kwa nini hakuweka vizuri mirathi yake huku akijua ana wake wawili.alikumbuka kutunga kitabu akasahau mirathi.Tuna la kujifunza.
 
Back
Top Bottom