DOKEZO Wasimamizi wa mtihani wa taifa kidato cha 4 Babati mji waambiwa warudishe kiasi cha pesa walilicholipwa kwa ajili ya usimamimizi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Anonymous

Senior Member
Joined
Apr 6, 2006
Posts
118
Reaction score
339
Halmashauri ya Babati mji iliyoko wilayani Babati mkoani Manyara ni moja ya halmashauri zinazoendelea na tukio la ufanyikaji wa mtihani wa taifa kidato cha 4 huku wasimamizi wakiwa ni moja ya wahusika wakuu katika zoezi hilo.

Wasimamizi hao walipewa kiasi cha pesa kulingana na siku wanazosimamia katika vituo husika kupitia ofsi ya uhasibu ya halmashauri lakini cha kushangaza ni baadae kuitwa ofsi za idara ya elimu kurudisha kiasi cha pesa hizo walizolipwa.

Sababu walizopewa ni kuwa wataenda wachache kwa kubadilishana siku za Practicals kwa masomo ya fizikia, kemia na mengineyo ambayo ni optional subjects. Wadau wanahoji, kama ilikuwa ni official kwa nini pesa isingekusanywa na idara iliyowalipa (uhasibu)?

Je, pesa zitarudi sehemu husika au zitakaa mifukoni mwa watu? Utaratibu huo ndo unatumika sehemu zote au ni double standard?
 
Roho mbaya tu yaani mwalimu akipata vilaki tano wanavifuatilia!

Anyway sifahamu chochote ila pesa ikilipwa huwezi ambiwa rudisha! Kweli SERIKALI imelala kiasi hiki?
Kwako wewe mwandishi anasomekaje?
 
Roho mbaya tu yaani mwalimu akipata vilaki tano wanavifuatilia!

Anyway sifahamu chochote ila pesa ikilipwa huwezi ambiwa rudisha! Kweli SERIKALI imelala kiasi hiki?
Watapewa kazi ya kusimamia chaguz serikali mitaa
 
Utarudishaje hela uliyolipwq kwa utaratibu stahiki? Kwanza ukilipwa hela halali ndani ya dakika 0 unakuwa umeishaanza kuipiga!
 
Halmashauri ya Babati mji iliyoko wilayani Babati mkoani Manyara ni moja ya halmashauri zinazoendelea na tukio la ufanyikaji wa mtihani wa taifa kidato cha 4 huku wasimamizi wakiwa ni moja ya wahusika wakuu katika zoezi hilo.

Wasimamizi hao walipewa kiasi cha pesa kulingana na siku wanazosimamia katika vituo husika kupitia ofsi ya uhasibu ya halmashauri lakini cha kushangaza ni baadae kuitwa ofsi za idara ya elimu kurudisha kiasi cha pesa hizo walizolipwa.

Sababu walizopewa ni kuwa wataenda wachache kwa kubadilishana siku za Practicals kwa masomo ya fizikia, kemia na mengineyo ambayo ni optional subjects. Wadau wanahoji, kama ilikuwa ni official kwa nini pesa isingekusanywa na idara iliyowalipa (uhasibu)?

Je, pesa zitarudi sehemu husika au zitakaa mifukoni mwa watu? Utaratibu huo ndo unatumika sehemu zote au ni double standard?
 
Attachments

  • 354506.jpg
    354506.jpg
    14.5 KB · Views: 9
Back
Top Bottom