'Wasimamizi wa ndoa ni 'Pisi Kali' kuliko Mabibi Harusi'

IMG_0971.jpg
 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk Amon Mpanju amesema siku hizi wasimamizi wa ndoa wamekuwa ni fasheni na siyo wale wenye sifa ya kufanya kazi hiyo katika ndoa.

Sambamba na hilo amesema wakati mwingine wanakuwa ‘pisi kali’ kuliko bibi harusi mwenyewe.

Mpanju ameyasema hayo leo Ijumaa Novemba 25, 2022 katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku 16 za uanaharakati dhidi ya ukatili wa kijinsia, yaliyofanyika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.

Amesema hii ni tofauti na huko nyuma ambapo msimamizi alipaswa kuwa mtu anayejua vizuri masuala ya ndoa na kutumika kama msuluhishi pindi kunapotokea changamoto.

Amesema hii imekuwa tofauti kwa sasa ambapo wasimamizi hao imekuwa ni fasheni na wanaangalia zaidi mvuto wa kimaumbile na sura na wengine wanakuwa hawajaingia kwenye ndoa hivyo kunavyotokea mtikisiko kwa wenye ndoa anashindwa kuwasaidia kwa kuwa hana uzoefu.

Hata hivyo, katika kuendelea na kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia vikiwemo vya ndani ya ndoa, katibu huyo amesema Serikali inaenda kushuka chini kwenye jamii ikiwemo kuwashirikisha viongozi wa dini makanisani misikitini na madrasa.

"Huko msikitini na makanisani kwa viongozi wa dini ndio watu wanaoweza kupata mafunzo ya uchaguzi mzuri wa mtu wa kuoa au kuolewa naye.

“Pia inatakiwa ifike mahali jamii itofautishe tendo la ndoa na taasisi ya ndoa ambayo ni kubwa kuliko mnavyofikiria hivyo katika mkakati ya kutokomeza ukatili wa kijinsia safari hii tunataka kumshirikisha kila mwanajamii wakiwemo viongozi hao wa dini,"amesema Mpanju.

Katika kukabiliana na vitendo vya vipigo katika ndoa, katibu huyo amesema kwa wale walio na mahusiano na wanaume wenye tabia ya kuwapiga wakati wakiwa kwenye uchumba wasitegemee mwanaume huyo akabadilika akiwa kwenye ndoa.

Ameeleza hiyo ni trela ndani akiingia atakuta mkanda wenyewe na kushauri waanze kuwaepuka mapema kabla ya kuja kufanyia madhara makubwa.

MWANANCHI
Picha umepeleka wapi
 
Nafikiri ameongelea matron kizaidi.. ila wengi nawona hamufahamu alilonena.. hivyo munafikiria ma maids. Inasikitisha sana.. ongezeni na wazee wenu wawafunze..

Nachojua wengine hata wakisimamia walio kwa ndoa ndio wanasaini.. bali wapo pembeni na ukubwa wao 😄
 
“Pia inatakiwa ifike mahali jamii itofautishe tendo la ndoa na taasisi ya ndoa ambayo ni kubwa kuliko mnavyofikiria hivyo katika mkakati ya kutokomeza ukatili wa kijinsia safari hii tunataka kumshirikisha kila mwanajamii wakiwemo viongozi hao wa dini,"amesema Mpanju.
Hii tu ndio nimeona point
 
Nahisi kuna kitu anachanganya hapo. Mfano kwa wakristu najua wasimamizi lazma nao wawewana ndoa
1669534426580.png

alaf sasa kuna vile vidada vinavyo misindikiza bibi harusi sijui ndio mnaviita bridesmaids
1669534575925.png
 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk Amon Mpanju amesema siku hizi wasimamizi wa ndoa wamekuwa ni fasheni na siyo wale wenye sifa ya kufanya kazi hiyo katika ndoa.

Sambamba na hilo amesema wakati mwingine wanakuwa ‘pisi kali’ kuliko bibi harusi mwenyewe.

Mpanju ameyasema hayo leo Ijumaa Novemba 25, 2022 katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku 16 za uanaharakati dhidi ya ukatili wa kijinsia, yaliyofanyika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.

Amesema hii ni tofauti na huko nyuma ambapo msimamizi alipaswa kuwa mtu anayejua vizuri masuala ya ndoa na kutumika kama msuluhishi pindi kunapotokea changamoto.

Amesema hii imekuwa tofauti kwa sasa ambapo wasimamizi hao imekuwa ni fasheni na wanaangalia zaidi mvuto wa kimaumbile na sura na wengine wanakuwa hawajaingia kwenye ndoa hivyo kunavyotokea mtikisiko kwa wenye ndoa anashindwa kuwasaidia kwa kuwa hana uzoefu.

Hata hivyo, katika kuendelea na kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia vikiwemo vya ndani ya ndoa, katibu huyo amesema Serikali inaenda kushuka chini kwenye jamii ikiwemo kuwashirikisha viongozi wa dini makanisani misikitini na madrasa.

"Huko msikitini na makanisani kwa viongozi wa dini ndio watu wanaoweza kupata mafunzo ya uchaguzi mzuri wa mtu wa kuoa au kuolewa naye.

“Pia inatakiwa ifike mahali jamii itofautishe tendo la ndoa na taasisi ya ndoa ambayo ni kubwa kuliko mnavyofikiria hivyo katika mkakati ya kutokomeza ukatili wa kijinsia safari hii tunataka kumshirikisha kila mwanajamii wakiwemo viongozi hao wa dini,"amesema Mpanju.

Katika kukabiliana na vitendo vya vipigo katika ndoa, katibu huyo amesema kwa wale walio na mahusiano na wanaume wenye tabia ya kuwapiga wakati wakiwa kwenye uchumba wasitegemee mwanaume huyo akabadilika akiwa kwenye ndoa.

Ameeleza hiyo ni trela ndani akiingia atakuta mkanda wenyewe na kushauri waanze kuwaepuka mapema kabla ya kuja kufanyia madhara makubwa.

MWANANCHI
Weka picha mkuu
 
Back
Top Bottom