Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Maafisa na wasimamizi wa uchaguzi katika mikoa ya Mwanza na Mara wametakiwa kuhakikisha wanavishirikisha vyama vya siasa kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi, huku wakizingatia sheria na kuiepuka migogoro inayoweza kuibuka wakati wa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Wito huo umetolewa na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Asina Omary, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo maafisa na wasimamizi hao, yaliyofanyika jijini Mwanza.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuweka mazingira rafiki kwenye vituo vya kupigia kura, hasa kwa watu wenye ulemavu ili kuhakikisha kila raia anapata haki ya kushiriki mchakato wa kidemokrasia kwa usawa.
Katika mafunzo hayo ambayo yamepewa kaulimbiu ya “Kura Yako, Haki Yako – Jitokeze Kupiga Kura”, washiriki wameeleza kuwa yamewapa mwanga mpana kuhusu wajibu wao katika kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru, haki na wa kuaminika.