LGE2024 Wasimamizi wa vituo vya Uchaguzi 1,213 wapewa mafunzo na kula kiapo

LGE2024 Wasimamizi wa vituo vya Uchaguzi 1,213 wapewa mafunzo na kula kiapo

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Kuelekea siku ya Uchaguzi wa serikali za Mitaa, wasimamizi wa vituo vya Uchaguzi 1,213 wamepewa mafunzo na kuapishwa kwa ajili ya kusimamia uchaguzi huo utakaofanyika siku ya Jumatano ya Novemba 27, 2024.
IMG_0889.jpeg

Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Nachingwea Mhandisi Chionda M. Kawawa amewasihi wasimamizi hao kuhakikisha wanazingatia mafunzo na viapo walivyopewa ili kusimamia Uchaguzi huo kwa weledi na kuhakikisha wananchi wanapata haki yao ya kimsingi kwa ajili ya maendeleo ya Wilaya na Taifa kwa ujumla.
IMG_0890.jpeg

Aidha, Mhandisi Kawawa amewakumbusha wasimamizi hao kuwa wamechaguliwa kwa kuzibgatia taaluma na nizamu walizonazo hivyo ni vizuri kufuata kanuni na sheria za nchi katika kuhakikisha usimamizi wa Uchaguzi huo unakua vizuri, mafunzo hayoyaliuzuliwa na wasimamizi wa kata, vijiji na Makarani.
IMG_0891.jpeg
 
Back
Top Bottom