ushuhudaunaoishi
Member
- Dec 1, 2025
- 7
- 3
Nina kero inayohusu Halmashauri ya Jiji au Halmashauri ya Ilala, sisi Vibarua tunaosimamia Vyoo vya Halmashauri ya Jiji tunacheleweshewa mishahara mara kwa mara na hatuzingatiwi na Viongozi wa Juu licha ya kuwa kazi tunayofanya ni ngumu.
Wakubwa wao wanachojali ni mapato tu hawajali kuhusu changamoto zozote zile kwenye vyoo ambazo sisi wasimamizi tunakutana nazo.
Mfano kuna mwenzetu mmoja ana miezi miwili shimo lake la maji taka limejaa, lakini Viongozi wakipigiwa simu ili watoe hela lishughulikiwe, majibu yao ni yaleyale "Mhasibu katoka" ama "Tunafatilia" na hapohapo ukipunguza mapato kutokana na changamoto zako inakuwa kesi kubwa kwako.
Tatizo kubwa ni Viongozi wa Ilala kutotatua changamoto zetu huku wao wakiwa wanajali mapato yanayoingia, wakumbuke kuwa na hao wanaowaona vibarua wana familia, wamepanga na kuna Watu wanawategemea kwa kazi hiyohiyo.
Jambo lingine ni kuwa, vyoo vya Halmashauri ya Ilala vinakuwa vibovu kutokana na wao kutozingatia changamoto wanazopewa na collectors.
Mikataba pia hatupewi, unasainishwa tu na kuondoka nayo hakuna collector ambaye hata ana nakala ya mkataba wake labda kama alipiga picha wakati wa kusaini.
Suala ya vitendea kazi kama sabuni, madawa ya chooni na mifagio na squeezers vyote vinatakiwa kutoka halmashauri lakini vitu vyote tunanunua sisi.