Susuviri
JF-Expert Member
- Oct 6, 2007
- 3,713
- 889
Hakina hata risiti!!!!
Wizi mtupu! Na wanaendelea kumwibia!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hakina hata risiti!!!!
Mkuu ujinga ni pale Raia Tanzania ilipotoa story na evidence ya miamala ya Mbowe, msemaji wa Chadema kaibuka na kuongea vitu vya ajabu ila utetezi wenyewe ni malalamiko tu hakuna facts.
Bora waache tu na warudi kukaa kimya. Sidhani kama kuna mtu na akili timamu na mwenye weledi kabaki Chadema hivi sasa!
Sakata la Mabilioni nje ya nchi
MBOWE HACHOMOKI
? BENKI KUU YAMKANA
L Ni kwa kashfa ya Kutorosha mabilioni ya fedha kwenda akaunti za nje
Na Mwandishi Wetu
Sakata la kukamatwa kwa mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe kutokana na kashfa ya kutorosha fedha nje ya nchi limezidi kuchukua sura mpya baada ya benki Kuu ya Tanzania kulithibitishia gazeti hili kuwa benki hiyo haina taarifa zozote zinazohusu umuliki wa akaunti hizo tofauti na sheria inavyoelekeza.
Sheria ya usimamizi na wa fedha za kigeni ya mwaka 1998 (Foreign Exchange Circular)inatamka inatamka bayana kwamba mtanzania yeyote, hataruhusiwa kumiliki ama kufungua akaunti nje ya nchi bila kwana kupata kibali cha Gavana wa Benki kuu.
Kifungu namba 3.3 cha sheria hiyo ya waka 1998 kinatamka ??itakuwa ni marufuku kwa raia wa Tanzania kufungua akaunti kwenye benki nje ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzaniakama sio mkazi katika nchi hiyo isipokuwa tu aweamepata kibali cha gavana wa benki kuu??
Kifungu hicho cha sheria kinakwenda tofauti kabisa na kitendo cha mtanzania freeman mbowe anayemiliki akaunti kadhaa nje ya nchi zikiwemo zile za kampuni yake ya ARETRAWORLD WIDE LIMITED yenye maskani yake falme za kiarabu ikiwa na akaunti za fedha za kimarekani yaani dola na fedha ya kiarabu yaani Riyar kila moja kwa akaunti namba 001105549660010 na 00110549660010.
Uchunguzi uliofanywa na Jamvi la Habari umebaini kwamba pamoja na sheria kutamka bayana, lakini wafanyabiashara kadhaa akiwemo Mbowe, wanaomiliki makampuni nje ya nchi wamekuwa wakifungua na kumiliki akaunti hizo bila kupata kibali cha gavana wa benki kuu kama ambavyo sheria inaelekeza.
Jamvi la Habari, lilipomuuliza Gavana wa benki kuu ya Tanzania kama ufunguaji wa akaunti hizo zinazomilikiwa na Freeman Mbowe kuwa zimefuata utaratibu na kupata kibali ya Gavana wa Benki kuu, Gavana Profesa Benno Ndullu, alijibu kuwa Benki kuu haina taarifa yoyote kuhusu akaunti hizo, jambo linaloongeza sintofahamu kuhusiana na uvunjwaji huo wa sheria unaofanywa na kiongozi huyo mkuu wa CHADEMA.
??Benki kuu haina taarifa juu ya akaunti hizi?? alisema Gavana ndulu akijibu swali la mwandishi wa gazeti hili.
Kutokufuatwa kwa matakwa hayo ya sheria hiyo kwa mfanyabiashara huyo kunamuweka katika hatihati ya kukutana na kifungo cha miaka 14 jela ama kutozwa faini ya kulipa mara tatu zaidi ya fedha alizotunza katika akaunti hizo zilizopo nje ya nchi kama sehemu ya 13(4) ya sheria namba 14 ya mwaka 1992 ya fedha za kigeni inavyosema.
Hivi karibuni gazeti hili liliandika uwezekano wa jeshi la Polisi Nchini kumkamata Mwenyekiti huyo wa CHADEMA, Freeman Mbowe kwa kudaiwa kutorosha mabilioni ya fedha kwenda nchi mbalimbali za Bara za Asia.
Uchunguzi uliofanywa na JAMVI LA HABARI, umebaini kwa kiasi kikubwa uchunguzi uliokuwa unafanywa na Kitengo cha Uchunguzi wa Fedha kilicho chini ya Wizara ya Fedha (FIU) kimekamilika huku Polisi ikitarajia kuanza kuchukua hatua zaidi.
Taarifa ilizozipata gazeti hilo kutoka FIU, ilisema tayari kila kitu kimemalizika na kilichobaki ni suala hilo, kulipeleka Polisi kwa ajili ya kuchukua uamuzi zaidi wa jambo hilo.
"Tumemaliza kila kitu na kilichobaki ni Polisi, lakini mie sio msemaji wa suala hilo, ungezungumza na watu wa FRAUD kutoka Polisi, ambao watakupa nafasi nzuri ya suala hilo, ambalo ni kubwa sana,''alisema.
Hata hivyo, Gazeti hili liliwasiliana na mmoja wa askari wanaoelezwa kulishikiria suala hilo, Salum Kisai, ambapo alisema yeye sio msemaji na kumtaka mwandishi awasiliane na Kamanda wa Upelelezi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, ZCO Costastine Massawe na kukata simu.
"Embu wasiliana na ZCO mie sio msemaji wa suala hilo,''alisema na kukata simu.
Mbowe, ambaye alisafirisha fedha hizo mwanzoni mwa mwezi wa Agosti, mwaka huu baada ya kuamisho mabilioni ya fedha kwenye akaunti yake hivi karibuni bila kuwa na vielelezo vya kufanya hivyo na kutakiwa kukamatwa na kumfikisha katika vyombo vya dola.
Mbowe, ambaye pia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Mbunge wa Hai na mfanyabiashara mwenye makampuni mengi hapa nchini, amefanya uhamisho huo wa fedha kwa kutumia kampuni isiyofahamika sana ijulikanayo kwa jina la Aretra World Wide Limited na imethibitika kwamba amefanya uhamisho huo wa fedha kwa kumtumia mtu anayeitwa Junaid Ali, ambaye ni Meneja wa Mahusiano ya Wateja wa Benki ya Noor ya Falme za Kiarabu mwezi huo.
Taarifa zaidi zinathibitisha kwamba, Kwa kumtumia Ali, Mbowe aliagiza fedha hizo zipelekwe katika akaunti tatu tofauti ambazo zote ziko nje ya Tanzania.
Kampuni hizo na kiasi cha fedha kilichopelekwa ni Puku Hong Kong Limited iliyotumiwa dola 230,555 (shilingi milioni 461), TanChin Trading Co. Limited iliyotumiwa dola 302,614 (shilingi milioni 605) na Hong Kong Da Web International Tradings Limited iliyotumiwa dola 489,860 (shilingi milioni 980). Jumla ya fedha zote zilizohamishwa ni zaidi ya shilingi bilioni mbili.
Makampuni yote yaliyotumiwa fedha yana ofisi zake nchini Hong Kong na yote yamefunguliwa akaunti katika benki maarufu ya HSBC.
Junaid Ali ambaye amepewa maelekezo ya kufanya malipo hayo ni mtaalamu wa masuala ya kufungua makampuni yanayojulikana kama offshore ambayo mara nyingi hutumiwa na wafanyabiashara kufanya malipo pasipo kujulikana na watu.
Taarifa zinaendelea kusema kwamba makampuni ya namna hii hufunguliwa katika nchi zenye usiri mkubwa kwa watu wanaohifadhi fedha na ndiyo maana wakati wa sakata la ununuzi wa rada, Andrew Chenge na aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), Dk. Idris Rashid, walitumiana fedha kupitia akaunti zao zilizo katika nchi zinazoongoza kwa kuwa na makampuni mengi ya namna hii.
Akimwandikia Junaid, Freeman Mbowe alisema; ? Tafadhali, nakuomba na kwa haraka, ufanye uhamishaji wa fedha kutoka katika benki yako na kwenda kwenye akaunti zifuatazo; Puku, TanChin na Hong Kong Da Web,? aliandika Mbowe.
Katika barua hiyo ambayo JAMVI LA HABARI imefanikiwa kuona nakala yake, Mbowe ameitambulisha kampuni yake kwa anuani ya S.LP 293816, iliyopo katika jengo la World Trade Centre, Mtaa wa Sheikh Zayed, Dubai falme za kiarabu.
Kwa kuwa kampuni hiyo ya Mbowe ni offshore, gazeti hili limeshindwa kufahamu ni kiasi gani cha fedha Mbowe amehifadhi au ameweka kwenye akaunti hiyo na chanzo cha mapato hayo ni kipi kwa vile biashara zake nyingi anafanya hapa nchini, ingawa ameanza kujitanua kimataifa.
Sambamba na hilo , uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba Mbowe alitakiwa kupokea kiasi cha dola 330,000 (shilingi milioni 660) ?takribani sawa na fedha aliyoihamishia TanChin Hong Hong, kutoka kwa wafadhili wa chama hicho waliopo nchini Japan.
Kwa mujibu wa mawasiliano baina ya viongozi wa juu wa Chadema na wafadhili hao wa kijapani kupitia kwa mtu anayefahamika kwa jina la Naomi pamoja na Mchungaji Mariko Morikubo, Chadema ilikuwa ichangiwe fedha za kijapani (Yen), milioni 40 ambazo ni sawa na dola 330,000 kabla ya mwisho wa Julai mwaka huu.
Ndani ya CHADEMA, ni viongozi wakuu watatu ndiyo wanaonekana kushiriki katika mazungumzo hayo; Mbowe, Slaa na Reginald Munisi ambaye ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa chama hicho.
Mpaka sasa haijafahamika mara moja ni kwa nini Mbowe amehamisha kiasi kikubwa namna hiyo cha fedha na kukipeleka nje ya nchi na kwamba imeendelea kutia mashaka kama kuna kodi halali ya serikali imekatwa katika muamala huo.
Wakizungumza na gazeti hili lilipotaka kujua mtazamo wao kuhusu kinachoitwa ?utumbuaji majipu wa magufuli? wananchi kadhaa wamesema hicho nacho ni moja kati ya kipimo kikubwa cha uimara wa serikali ya magufuli na kwamba kama ataweza kumkamata Mbowe basi ataonekana kweli amedhamiri kulikomboa taifa letu na kuthibitisha msemo kwamba sheria ni msumeno.
Abdallah Hussein, mkazi wa Kichangani Morogoro amesema, ili nchi yoyote inayofuata na kuheshimu utawala wa sheria ni lazima watu wote waishi misingi na utaratibu wa nchi hiyo, Hussein amesisitiza ikiwa Mbowe ameweza kufanya hivyo na kama hatua haitachukuliwa dhidi yake, basi kuna uwezekano mkubwa wa wanasiasa wengine kutumia uanasiasa wao kufanya biashara halali na haramu kujinufaisha.
??Hebu ona hii,mtu kama mbowe anaweza kusafirisha zaidi ya bilioni mbili kiharaka haraka hivyo, unatarajia kuna uhalali hapo? ,nani amekagua hizo hela na kuthibitisha ni halali na hazina madhara wala viashiria vya rushwa???.
Ameendelea kushangaa na kuonyesha taadhari ya hali ya juu na kumtaka Rais Magufuli kuhakikisha anaendelea kutumbua majipu na kusisitiza kwamba asimuangalie mtu yeyote usoni na kwamba ni lazima sasa vyombo vya dola vikachukua nafasi yake na kuthibitisha uhalali wa fedha hizo .
Taarifa ambazo gazeti hili linazo zinasema kwamba kitengo cha udhibiti wa Fedha FIU kinaendelea kulishuhulikia suala hilo na kwamba inatarajiwa hatua kuchukuliwa wakatio wowote kutoka sasa.
Mara kadhaa Mbowe amekaririwa kama mtu anayetetea sana uwepo wa utawala wa sheria na kwamba amekuwa akiilaumu serikali na taasisi nyingine zisipofuata sheria, jambo ambalo yeye pia anakabiliwa nalo hivi sasa,.
Ikiwa FIU watakamilisha uchunguzi wao haraka kama inavyotarajiwa, jeshi la polisi litakuwa na wajibu wa kumkamata na kumfikisha mahakamani kwa tuhuma za usa
Chanzo. GAZETI LA JAMVI LA HABARI
Nashauri Mh Freeman Mbowe achukue fursa hii kukanusha tuhuma zilizozagaa kila kona ya nchi kuwa alipokea tsh 12 billioni kama gharama ya "kiingilio/registration fee" ya Lowassa chadema. Akishindwa kukanusha tuhuma hizo mbele ya jamii hii, nadhani tutakuwa tumetenda haki kama tukiifanyia amendment list of shame na kumuongeza Mh Freeman Mbowe
Pole Pole tutawafikia tuNashauri Mh Freeman Mbowe achukue fursa hii kukanusha tuhuma zilizozagaa kila kona ya nchi kuwa alipokea tsh 12 billioni kama gharama ya "kiingilio/registration fee" ya Lowassa chadema. Akishindwa kukanusha tuhuma hizo mbele ya jamii hii, nadhani tutakuwa tumetenda haki kama tukiifanyia amendment list of shame na kumuongeza Mh Freeman Mbowe
Kama ni kweli tuone sasaBila shaka wote tunapinga ufisadi na uovu mwingine wote unaowafanya watanzania wasisonge mbele kama taifa
Ufisadi upi huo?Hongera Magufuli kwa kupambana na ufisadi
Wa kuficha fedha chumbaniUfisadi upi huo?