Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa ametoa siku thelathini (30) kwa wamiliki wote wa ardhi wanaodaiwa Kodi ya Pango la Ardhi ambao hawajalipa hadi sasa kulipa kodi husika na baada ya muda huo kupita hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Waziri Silaa ameyasema hayo leo tarehe 10 Mei 2024 katika Ofisi za Wizara ya Ardhi zilizopo Magogoni jijini Dar es salaam.
Waziri Silaa amesema kuwa kila mmiliki wa ardhi analo jukumu la kulipa kodi ya pango la ardhi kila mwaka amepewa sharti la kulipa Kodi ya Pango la Ardhi kwa kila mwaka kwa mujibu wa Fungu la 33 (1) la Sheria ya Ardhi (Sura ya 113).
Aidha, ameongeza kuwa kwa mujibu wa Fungu la 44 (1) la Sheria ya Ardhi (Sura ya 113), kila mmiliki wa ardhi anatakiwa kutimiza masharti ya umiliki ikiwa ni pamoja na sharti la kulipa Kodi ya Pango la Ardhi.
Silaa amesema Kitendo cha kutolipa Kodi ya Pango la Ardhi ndani ya muda uliowekwa na sheria, kinasababisha mmiliki wa ardhi kuvunja moja ya sharti la umiliki.
Ameongeza kuwa Wizara kwa nyakati tofauti, imekuwa ikihamasisha na kuwakumbusha wamiliki wa ardhi kulipa Kodi ya Pago la Ardhi. Hata hivyo, baadhi ya wamiliki wa ardhi hawajatekeleza wajibu huo wa kisheria.
“Naelekeza wamiliki wote wa ardhi wanaodaiwa Kodi ya Pango la Ardhi, kulipa kodi husika ndani ya siku thelathini (30) kuanzia tarehe ya tangazo hili. Baada ya muda huo kupita, hatua za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na wamiliki hao watafikishwa mbele ya Mahakama na taratibu za kisheria za ubatilisho wa milki zao zitaendelea” Amesema Silaa.
Silaa amehitimisha kwa kusema kuwa katika kipindi hicho cha siku thelathini (30), vituo vya makusanyo ambavyo ni; Ofisi za Ardhi za Mikoa na Ofisi za Ardhi za Halmashauri zote nchini, kwa siku za kazi zitakuwa wazi hadi muda wa saa 2:00 Usiku. Hivyo, naagiza watendaji wote wa Sekta ya Ardhi, kuratibu mazingira rafiki kwa ajili yakufanikisha utekelezaji wa mkakati huu.
Kuna kodi ya pango (nyumba) na kodi ya ardhi. Kwa hiyo ukiwa na hati ya ardhi utaiilipia na kama umejenga nyumba juu ya aridhi hiyo utalipia nyumba hiyo kodi.
Kodi ya pango la ardhi ni kodi ya kiwanja/shamba kilichopimwa.
Kodi ya jengo inalipwa kwenye ardhi ilioendelezwa ndio ile tunalipa kupitia LUKU.
Wataalam watanisahihisha kama nimekosea.
Kuna kodi ya pango (nyumba) na kodi ya ardhi. Kwa hiyo ukiwa na hati ya ardhi utaiilipia na kama umejenga nyumba juu ya aridhi hiyo utalipia nyumba hiyo kodi.
So natakiwa niende TRA wanikadirie gharama ya kodi ya ardhi, sahihi? Mana nina hati na nimeshajenga, sikuwaza hayo ya ardhi maana najua wanakata kwenye Luku.
Ikiwemo kutangazwa na kufikishwa mahakamani nimepitia mtaani kwa watu wengi hawajalipa na hawatishiki na hilo tangazo, bado watu wengi kulipa inakuwa uzito Fulani kwanini watu hatulipi kodi kwa hiari kuna tatizo vitu vingi tunahamasishwa Ila hatuvifuati kwanini mfano kudai risiti Leo hii hata hapa Jamiiforums waliodai risiti ni wachache sana.
Ikiwemo kutangazwa na kufikishwa mahakamani nimepitia mtaani kwa watu wengi hawajalipa na hawatishiki na hilo tangazo, bado watu wengi kulipa inakuwa uzito Fulani kwanini watu hatulipi kodi kwa hiari kuna tatizo vitu vingi tunahamasishwa Ila hatuvifuati kwanini mfano kudai risiti Leo hii hata hapa Jamiiforums waliodai risiti ni wachache sana.
Ugumu unaanzia pale unapotakiwa ukapange foleni huko maofisini wafanye namna hata kulipia kwa njia ya mtandao watu wengine wako mbali wengine majukumu yanabana