Kiranja wa jamii
JF-Expert Member
- Jan 2, 2023
- 441
- 1,065
Kitu kitakachokumbukwa sana kwenye bunge la bajeti mwaka huu 2024 utakuwa mjadala wa sukari kati ya Mpina na Bashe.
Dkt. Tulia ameuliza swali la msingi sana kuhusu muda ambao viwanda vyetu vinahitaji ili viweze kuzalisha sukari kwa utoshelevu na hatimaye bei iwe sawa na nchi zilizotuzunguka
Wawekezaji wengi wanaowekeza Tanzania wamekuwa wakitumia mbinu chafu kuwanyonya wananchi kwa muda mrefu sana kwa kisingizio cha kuzalisha kwa hasara
Viwanda vya sukari vipo kwa muda mrefu sana na uzalishaji umeendelea kuwa wa kusua sua na sasa hawataki serikali ihifadhi sukari ili kudhibiti upandaji holela wa sukari. Hii ni tafsiri kuwa wao wanataka waendelee kunufaika na uhaba wa sukari nchi hii hivyo hakuna siku watataka kuongeza uzalishaji wao kwani hilo sio lengo lao. Ni lazima wabanwe ili wajitutumue
Hali hii haipo kwenye sukari pekee. Hapo nyuma tumekuwa tukisikia mambo ya Tax exemption kwa makampuni kadhaa kwa visingizio vya kutopata faida katika uwekezaji wao. Ifike mahali mambo kama haya yaishe anayeshindwa ampishe mwingine. Dunia ni ya ushindani sio ya kubembelezana
Unaweza kushuhudia makampuni kama ya simu yanavyotengeneza pesa kwenye kila angle. Lakini serikali ikipeleka tozo wanazileta kwa walaji. Haya mambo hadi lini?
Leo tumeona taarifa ya Makamba kutaka kuonana na mabalozi ambao wawekezaji wao wanalalamikia kodi za TRA. Si ajabu nao ni wababaishaji tu. Hayo tumeyaona kwenye makampuni ya madini
Namna Dkt. Tulia alivyoendesha mjadala wa sukari imetoa picha kuwa kumbe viongozi wa nchi hii wanajitoa ufahamu. Wakiamua kuisaidia nchi ipige hatua wanaweza. Siasa za vyama na uchawa ndio mchawi wa maendeleo ya nchi hii.
Atakaye ikomboa nchi hii ni atakayeweza kufuta mind set ya wanasiasa kutanguliza vyama vyao na uchawa kwa viongozi kabla ya maslahi ya nchi. Hiki ndicho kinawatafuna CCM na hatimaye wanadumaza nchi