Wasiostahili kurudi bungeni 2010


Mwawado: Pande za milimani mvyee anakuwa amekula chumvi zaidi. Ahsante kwa kuweka majina yao, watu kumbe ni wale wale na haishangazi kuwa hakuna mabadiliko Tanga. Hawa wazee wamejikita kisiasa na kifedha wamekaa vizuri, all in all wananchi kama wanataka maendeleo inabidi wawaambia hawa watu enough is enough.
 
mkuu
1. Naunga mkono hoja kwa asilimia zote isipokuwa pale kwa 'Pombe Magufuli' pls dont kid with the man.

2.Napendekeza kwanza tupate orodha ya wabunge ambao hawajawakilisha majimbo yao kabisa namaanisha hawajaongea kabisa bungeni zaidi ya kupiga makofi.
Something which as the result imewakosesha wananchi haki yao ya kikatiba ya kuwakilishwa!
3.Wale wenye tuhuma za kufoji kago za vyeti kuanzia PhD,Masters,Bachelors ...mpaka kwa nanihii kule mwanza.

Then tufanye decision accordingly!
 
Huku kwetu Kawe mi nataka aje Mheshimiwa Mdee.......🙂

Hivi huyo mama amesema anagombea tena Kawe? na Mdee ana nia ya Kawe? mana panahitaji mabadiliko kiukweli..

@Kijijini kwetu
Mbunge wangu sitaki aondoke, yupo juu na anakubalika sana pia kazi yake inaonekana. Big up Mbunge!!
 
Tuongeze na wabunge wote waliopo NEC. Kuwataja tu haitoshi. Ukiweza kumbadilisha japo mtu mmoja tu kutokuchagua CCM, utakuwa umesaidia mapambano haya.
 
wabunge wazee wote watoke..labda abaki malecela tu..
angalau yeye amekemea ufisadi..sio akina mzindakaya na galinoma na kingunge..rostam hawezi kuwa mzalendo..sisi watu weusi sijui tutabadilika lini..huyu rostam inabidi arudishwe na kwao..au anyongwe.
 
Tuongeze na wabunge wote waliopo NEC. Kuwataja tu haitoshi. Ukiweza kumbadilisha japo mtu mmoja tu kutokuchagua CCM, utakuwa umesaidia mapambano haya.

Hivi hakuna wabunge wa upinzani wasiofaa?
 
John Samwel Malecela--Mzee umri umeenda sana jamani,apumzike tu awaachie vijana akina William Malecela,Livingstone Lusinde na Hoya(mmiliki wa mabasi na mabucha ya Mshikamano) wapambane kupata nafasi ya kugombea ubunge wa Mtera.Ni vizuri mzee yeye akabaki kuwa mshauri tu ndani ya chama....Pia wazee wengine kama akina Mzindakaya,Kingunge Ngombare Mwiru,Kusila,Makweta,Shelukindo,Galinoma,Lubeleje,Degera n.k wapumzike wawaachie vijana nafasi sasa,maana tumewaona wakiwa wabunge kwa kipindi kirefu sana na hakuna mabadiliko yoyote tunayoyaona katika majimbo yao...
 
Hivi hakuna wabunge wa upinzani wasiofaa?

Historia inaonyesha kwamba wabunge wa upinzani licha ya uchache wao, mara zote wanapiga kura kwa maslahi ya nchi. Ndiyo maana inabidi tuongeze idadi yao bungeni. Kwa upande mwingine CCM [kutokana na idadi yao]wamefanya bunge kama moja ya jumuiya za CCM.
 
Bia umekunywa moja,Supu ya nini?

He he hee. Balantanda, wengine tukinywa bia moja tunakua tilalila, ndiyo maana twanywa supu....lol...
 
yah man Jumanne Malecela zama zake zimekwisha kwa kweli....lakini no no noo huyo mtotoe hafai hata chembe......
 
wengineo ni Abdi Mshangama wa Lushoto, Dk wanyancha wa serengeti, prof sarungi wa Rorya na wale wa viti maalum kibao.
 

Heee imekuwa kupokezana kijiti sasa, kwani hakuna wengine zaidi ya ukoo wa Malecela na mdogo wake Lusinde. Kwa mtaji huu CCM wataendelea kulindana maana wakiondoka wazee wanakuja watoto wao na watoto wadogo miaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…