Wasiostahili kurudi bungeni 2010

Wasiostahili kurudi bungeni 2010

Job Yustino Ndugai - Kongwa. Huyu jamaa hafai kabisa, miaka 10 hakuna maendeleo, pengine anataka kumwiga Senyagwa aliyekaa miaka 20 akitaraji kupata japo ka-uwaziri na kusahau kabisa kuwaletea wananchi maendeleo. nadhani hastahili kurudi 2010 hata kama wanamwamini na kumwachia aongoze bunge wakati mwingine. mbunge gani ambaye 'anapita' kwa wananchi badala ya kwenda kwa wananchi? yeye hupita njia tu akiwa amefunga vioo tinted, huku wakulima na wafugaji wakiuana mpakani mwa Kongwa na Kiteto. inatosha miaka 10 bwana.
 
Manywele--Monduli!
L Masha-wa mambo ya ndani
Viji-cent
Karamagi
 
1.Mary nagu(hanang:huyu mama ana wivu sana na wanawake wenzake,hapendi kabisa kuona wanawake wengine wanakuja juu zaidi kisiasa hata kama wana uwezo kumzidi yeye, hana point za maana katika mazungumzo, hadithi zake nyingi zinaonesha yuko shallow tuuu, nadhani umbumbu wake ndio chanzo cha kuchaguliwa na JK kuwa waziri)

2.Damasi Nakei(babati vijijini:ni mzigo tuu,hana lolote awapo bungeni, babati vijijini maji ni ya shida, anahongwa na wahindi wa hapa kijiji alinde maslahi yao)

3.Omari Kwaang(babati mjini: huyu alikuwa headmaster enzi zile nasoma kiru primary, jama ni looser wa nguvu bungeni anahistoria ya kuuliza swali moja tuu, hivi majuzi tumepata taarifa kuwa anataka,2010, kwenda babati vijijini akagombee ubunge,ameskwisha ongoza miaka 15 sasa jimbo la babati mjini, leo anataka kwenda vijijini baaada ya kuona hakuna upinzani mkali, onyooo, tutakutoa kwa marungu, ukome na kampeni zako chafu za kutumia mgongo wa dini)
 
Nyie watu acheni longolongo zenu. Nyie ndio mlimuingiza Mrema mkengeni kwa kufanya maandamano makubwa na kusukuma gari lake lakini wakati wa uchaguzi hamkujiandikisha.
 
Celine Kombani na Dr. Ngasongwa wataondoka kwa sababu ya Zombe na wenzake.
 
Jamani mmemsahau MUNGAI

Mungai kishasoma alama za nyakati, kwa kipigo alichopata alipogombea ujumbe wa NEC mkoani Iringa na pia alivyozomewa kule Mufindi na wananchi mwaka 2005 wakati wa kujinadi; akisimama kugombea atakua MWEHU!!
 
VIJANA CHUKUENI FORM MKA GOMBEE< BAHATI NASIBU HAUWEZI KUSHINDA BILA KUCHEZA. TUSI LALAMIKE TU KUTO KUACHIA UWANJA< WE HAVE TO ENTER THE FIELD. As for me entrepreneurship is more my thing then politics but I'm sure kama vijana we all have different interests. Those who feel they will do good in politics please enter.

Bravo!.....leo umetoa point ya maana MwanaF!.....Watu kama wanataka change then wakati ndiyo huu vijana chakarikeni acheni kupiga campagin za online.....

au kama vipi basi muandaeni mt cuzin mwanakijiji.....ili uchaguzi ujayo after 2010 asimame kidedea....mjumbe kutoka JF!......The forumn of great thinker....
 
7.Ligalama Casto- Kilombero.

nasikia huyu jamaa hajawahi kuchangia chochote tangu achaguliwe na inasemekana kama hajui kuwa yeye ni mbunge wa kuchaguliwa na wananchi
 
Mi naona Wabunge wote wa SISIEM na baadhi ya wabunge wa vyama vya Upinzani WABANDULIWE
 
Masha kwa kweli hata wana Nyamagana wamemchoka mafisadi ana kaa kimya anabaki anajibishana na mzee Mengi badala ya kuhangaika na mafisadi PAPA.
 
Pombe Magufuli kwa kweli ni kifaaa ila papara anatakiwa apunguze asikilize hata na ushauri wa watu wa chini yake. kwa mfano wakati yuko katika wizara ya ujenzi kuna mazuri mengi kayafanya ila lile la kuamrisha kuvunjwa kituo cha mafuta cha Mansoor maeneo ya kirumba mwanza kwa madai kua kiko barabarani na baadae Mansoor kushinda kesi na kupelekea serikali kumlipa huyo mansoor kwa kweli alichemka.
 
Rostam Azizi huyo anatakiwa asirudi kabisa nafikiri uongozi wa nchi hii unge kuwa ndio kama wa ndugu zetu Wachina Rostam angenyongwa kabisa.
 
Mzee wa mabomu!Chrisant Majitayanga Wachepa Mzindakaya!Jimbo la kwela-Rukwa.
 
Kule Tanga siwajui hata majina lakini kwa hali mkoa ulivyo naomba wekeni majina yao hapa, ili wajue kuwa tumeshawachoka and this is the begining of their end.
 
Back
Top Bottom