Hii ndio itafanya achaguliwe tena?
Hizi habari za kuonyesha kuwa mzee ni kigogo haina tija hapa JF, badala yake eleza mzee kafanyia nini wananchi wa Mtera kwa kipindi chote alichokuwa mbunge?
Pesa za kodi ya mazao na mifugo tunazokatwa sisi wananchi yeye ndio anakatia ticket ya ndege kwenda US, UK?
Kama kila siku yeye safari lini anawatumikia wananchi wake?
Kama kweli ana uchungu na wananchi wa Mtera, inakuwaje aishi Sea view halafu awawakilishe? Shuruba wanazopata wananchi wa Mtera hataki kuzisikia, yeye anajirusha Jijini Dar es Salaam.
Hizo Tshs milioni saba anazolipwa kwa mwezi kama mbunge, wananchi wa Mtera wanafaidika nazo vipi kama kweli yeye ni mwakilishi wa Wanamtera? Tumechoka, ni muda wa yeye kula pension yake.