Wasiostahili kurudi bungeni 2010

Wasiostahili kurudi bungeni 2010

Dr Slaa - Karatu

Hata mie naona SLAA hafai kabisa kuwa mbunge wa Karatu. Mbunge gani huyu jamani? Hebu muoneni mambo anayoyafanya kila siku. Tabia zake ndiyo kabisaaaa.........

DR. SLAA FOR NEXT PREZIDAA.

NB:
Sisi Sikonge twasema :- Saidi Juma Nkumba kwishieni.
 
Hussein Mwingi sii nasikia anaandaliwa kuwa Presidaaa Visiwani??

Ila I just like the Guy! Wala sijui kwa nini!!
 
Bill said:
Unataka Anne Kilango ayabebe hayo maendeleo kichwani ayapeleke? Ikiwa Fisadi Yona hakuweza ataweza Kilango ndani ya miaka 5 na kwa namna gani...

Bill,
daniel ndhira yona na anna kilango malecela ni watu wawili tofauti kabisa. yona nia yake ilikuwa kupata uwaziri ili aweze kufanya ufisadi. hakuwa na nia ya kufanya kazi na wananchi kuleta maendeleo jimboni kwetu. hata ukitembelea kijiji cha bendera alipozaliwa yona utasikitika jinsi alivyoshindwa kuwa mfano kwa wanakijiji wenzake.

anna kilango malecela ameshindwa katika majukumu yake kama mbunge wa same mashariki. anaweza kuwa anawasisimua huko magazetini kwa makelele yake dhidi ya ufisadi lakini katika suala la kuchochea na kusimamia shughuli za maendeleo jimboni kwake anapata maksi SIFURI.

inawezekana kupiga vita ufisadi na kuchochea na kusimamia maendeleo kwa wakati mmoja. anna kilango malecela ametusahau wananchi wake na kazi yake ni kupiga makelele ya ufisadi.
 
Mkukuti said:
Kwani mshahara wake kama mbunge ni kiasi gani. Jaribu kuchukua mshahara wake na marupu rupu pamoja na kiinua mgongo chake, then tuone kama utaweza kutatua taizo moja tu la kijamii ulilolioredhesha hapo juu.

Lakini kinyume cha hapo, ukichukua bilioni 40 za KAGODA na ukaziwekeza kutatua matatizo ya kijamii kwenye jimbo la mama Kilango, basi matatizo hayo yatakuwa historia. Ndio maana nadhani, mama Kilango amewekeza nguvu nyingi kupambana na ufisadi, akijua kuwa pesa zinazopotea huko ni nyingi na zinaweza kutatua matazo yote ya kijamii, kuliko akiba yake ambayo pengine haiwezi kulisha familia yake mwenyewe kwa mwaka mzima.

Mkukuti,
hakuna aliyependekeza anna kilango malecela atumie pesa zake za mfukoni kutatua matatizo ya wananchi wa same mashariki. hata wabunge wa majimbo mengine ya kilimanjaro ambao tulikuwa tumewaacha mbali kimaendeleo, lakini leo wametuzidi kimaendeleo, hawajatumia pesa zao za mfukoni kupeleka maendeleo majimboni kwao.

billioni 40 zilizoibiwa na mafisadi zinaweza kusaidia kutatua matatizo mengi sana ya wananchi. tunampongeza sana anna kilango malecela kwa kupiga makelele fedha hizo zirudishwe. anna kilango malecela aliahidi mambo mengi sana wakati wa uchaguzi, na hakueleza kwamba atatekeleza ahadi zake kwa kuhemea bilioni 40 za mafisadi. haya masuala ya ufisadi hakuyazungumza kabisa wakati wa kampeni ameyakuta huko Dodoma.

kwa upande mwingine wabunge wenzake wa kilimanjaro wanachapa kazi bila kusubiri bilioni 40 zirudishwe na mafisadi. maendeleo katika majimbo hayo yanaonekana wakati same mashariki inaendelea kudorora.
 
. Charles Kenja- Ubungo

hee ubungo na shida zote kumbe ina mbunge;loh keenja shame on you

Kingunge Ngombale Mwiru

Anna Kione Kilango Malecela-Same Mashariki. jimbo la Same Mashariki liko nyuma kuliko majimbo yote katika mkoa wa Kilimanjaro. Same Mashariki iko nyuma ktk elimu,afya,maji,mazingira,misitu,kilimo,barabara.

WEE SHIKA ADABU YAKO...........BUNGENI UTANGAKA WEYEEEEEE??????

huyu tumwachie JK....
 
FisadiNyangumi

Join Date: Mon May 2009
Posts: 5
Thanks: 0
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power: 0

Mazee karibu sana kwa jina jipya....
 
- Majungu matupu wasirudi ili aingie nani, wewe? Yaaani sasa mnaweza kuwachagulia wananchi nani aongoze majimbo yao? Acheni majungu haya, wananchi wa majimbo ndio wanajua nani anawafaa, labda muongelee majimbo yenu ambayo huwa mnapigia kura, kama kweli huwa mnapiga kura!

- Halafu mtutajie wabunge wanaofaa na walichofanya!

FMEs!

Mkuu FMES,
Naona sasa umeanza kuchoka.
Wakati watu wa Kyela-mbeya wanasema hawamtaki mbunge wao kutokana na kwamba hajawafanyia kitu,wewe ulikuwa wa kwanza kwa kusema kuwa tunaongelea Utaifa na sio jimbo mojamoja.Sasa ya kwako ni ya kitaifa?
 
Anna Kione Kilango Malecela-Same Mashariki. jimbo la Same Mashariki liko nyuma kuliko majimbo yote katika mkoa wa Kilimanjaro. Same Mashariki iko nyuma ktk elimu,afya,maji,mazingira,misitu,kilimo,barabara.

Ni yeye ndio alisababisha maendeleo kutokuwepo au naye alikuta maendeleo hakuna?
 
Wabunge wote wa CCM hawafai waondoke kwani hakuna walilolifanya zaidi ya wizi hakuna msafi hata mmoja. Mbaya zaidi wameiba kushibisha matumbo yao na vimada.
 
VIJANA CHUKUENI FORM MKA GOMBEE< BAHATI NASIBU HAUWEZI KUSHINDA BILA KUCHEZA. TUSI LALAMIKE TU KUTO KUACHIA UWANJA< WE HAVE TO ENTER THE FIELD. As for me entrepreneurship is more my thing then politics but I'm sure kama vijana we all have different interests. Those who feel they will do good in politics please enter.
 
Back
Top Bottom