Wasioujua ukweli kuhusu Corona Tanzania

Kaulize mtu wa karibu wa Prof Mbwette watakueleza amefariki kwa nini
Nadhani una tatizo mahali fulani akilini mwako. Unatutuuma kwenda ulizia habari za mareehemu ati nini kilimuua. Ili iweje?? Tena unasema Dr. John ana uwezo wa kupata matibabu ya hali ya juu. Huyo Mbwete uliambiwa alikuwa mnyonge? Huyo jdg uliambiwa alikosa pesa? Nitamwamini rais wangu 100% kuwa Korona kaondoka kama alivyokuja. Tuendelee na mambo yetu kama kawa. Nenda kaji lock down mwenyewe lakini sisi tutaendelea na yetu
 
Safi, ila kumbuka Mzee wetu likimpata ana access na the best health services, wewe? Sijui
Yeye ni muhimu kwa Tanzania kuliko watu kama wewe milioni 1 bora watz wapuuzi kama wewe milioni moja mfe kuliko raisi magufuli
 
Na aliyekuwa Waziri wa maliasili Magembe yupo Aga Khan corona inamsokota!
 
Wakuu huu ugonjwa upo na hata sasa uwezekano wa kuupata upo , huwezi kuukwepa kama unavyoambukizwa mafua, kuna wakati huwezi kujua umeyapatia wapi. Kwa maamuzi tuliyoyachukua ingekuwa ni ugonjwa unaoua moja kwa moja ukiupata basi watu wengi sana wangeteketea, unaua lakini si kila anayeupata lazima afe ama ahitaji hata kulazwa hospitali.

Kuna thread ya mdau mmoja nilijibu kama wiki 3, zilizopita niliumwa ugonjwa usioeleweka lakini ulikuwa na dalili zote za corona, kinachosaidia tu ni kutumia tiba asili kupunguza makali/maumivu na kujitenga na wenzako ili kukata mnyororo wa maambukizi, unasumbua kweli na kuna muda unaweza kukata tamaa lakini kama sio siku yako unavuka salama.
 
Ukisha fahamu dawa ya ugonjwa huna sababu ya kuwa na wasi wasi. Tanzania tupo salama sana. Hao wadhungu wenyewe wamenywea hivi sasa ugonjwa kwao unaua na wanafungua mipaka yao. Ni lazima kujifunza kuishi na haka kau-gonjwa kadogo.
 
MKUU mnyonge mnyongeni ila haki yake mpe bila kupepesa macho , binafsi nazunguka sana but mpaka sasa corona wenda imebaki kwa asilimia 15 tu na hapa namanisha kweli kabisa maana sijui unafiki,
so tz narudia kwa hili kupitia MAGHUFULI ,corona tumeikomesha na ikome kweli
 
Tanzania hamna Corona. Labda mniambie Tanzania kuna umasikini ndio nitaelewa.
Usijidanganye mkuu,corona ipo. Wapi watu wa karibu kabisa wanaumwa corona. Wamepima na sasa wanaendelea kutumia dawa bila kusahau kusali. La msingi tumuombe Mungu atuepushe nalo jumla. Wanasiasa sio wa kuamini 100%. Take care yourself.
 
Mliokuwa mnanibeza kwenye huu uzi sasa mmepata jawabu kuwa CORONA bado ipo. Tuendelee kuchukua tahadhari
 
Jamaa kashajua watanzania hawana akili lolote akiongea wanashangilia.
 
Kweli kabisa, ikija watokea kwa ndugu au rafiki zao wa karibu ndio wataelewa
 
Ni aibu sana kwake, na ndio maana sababu ya kifo cha Mkapa kimekua siri, maana ukitangaza amefariki kwa Corona ni aibu kwake sababu ashasema Tanzania Corona imepotelea kwengine
 
Ukweli ni kwamba hamna anaejua hali ya Corona nchini, ikiwemo serikali yenyewe kwasababu wameacha kufanya testing toka mwezi wa tano.
Wanapima COVID19 pale Mabibo kwa malipo ya Tshs. 100,000//=, records wanaweka na wanatoa certificate kwa walio test negative. I can confirm this 101%. Atleast hii inafanyika kwa drivers wa malori (prior booking) na wasafiri wengine japo sijajua kama wanapima yeyote anayejipeleka pale kama hasafiri.

Nilimdadisi dada mmoja kwenye chumba cha kutoa majibu na akaniambia kwamba wanapata positive cases often kwa watu wasio hata na dalili. Ukikutwa unayo, cheti hupati na unaambiwa uende kwako ukajitibu huku ukiwakinga uwapendao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…