Wasioujua ukweli kuhusu Corona Tanzania

Wasioujua ukweli kuhusu Corona Tanzania

Wanapima COVID19 pale Mabibo kwa malipo ya Tshs. 100,000//=, records wanaweka na wanatoa certificate kwa walio test negative. I can confirm this 101%. Atleast hii inafanyika kwa drivers wa malori (prior booking) na wasafiri wengine japo sijajua kama wanapima yeyote anayejipeleka pale kama hasafiri.

Nilimdadisi dada mmoja kwenye chumba cha kutoa majibu na akaniambia kwamba wanapata positive cases often kwa watu wasio hata na dalili. Ukikutwa unayo, cheti hupati na unaambiwa uende kwako ukajitibu huku ukiwakinga uwapendao
Korona bado ipo ingawa imepungua kweli. Kuna mtu namfahamu Ni staff mwenzetu Tena tuko Wilaya moja ya Kigoma huku wiki mbili zilizopita tuliarifiwa na na top management kuwa ametest positive. So you can imagine huku mikoani bado ipo maana jamaa hata hajasafiri siku za hivi karibuni.
 
Ubarikiwe sana mkuu
Leo baada ya kuapisha viongozi mbalimbali Ikulu ya Chamwino Dodoma, Dr. Magufuli alitamka kuwa Corona imeshapotea na kuongeza kuwa "tuko salama". Kuna ukweli gani juu ya madai haya?

Swali langu ni je tunajuaje tuko salama wakati hatujui hali halisi na serikali haijatoa takwimu rasmi za ugonjwa huu toka tarehe 29/04/2020? Ukweli ni kwamba hamna anaejua hali ya Corona nchini, ikiwemo serikali yenyewe kwasababu wameacha kufanya testing toka mwezi wa tano.

Vyanzo vyangu vya kuaminika vimeniambia kuwa baada ya wagonjwa wenye dalili kutiririka mahospitalini kutaka kupimwa, serikali ilikataza madaktari kupima na kupokea wagonjwa wa corona (Madaktari wa Hospitali za Temeke na Amana wanaelewa hili vizuri). Na waliambiwa kuwa kama kuna wagonjwa watafariki kwa matatizo ya kupumua wasiandike hivo kwenye vyeti.

Mimi ninaamini kuwa Corona imepungua sana, ni kwa sababu ya watu kupata immunity na pia kutumia tiba asili ila ninaamini pia huu ugonjwa bado upo japo si sana kama ilivyokuwa awali.

Katika wiki mbili zilizopita Mwalimu wangu Professor Mbwete alifariki kwa matatizo ya kupumua na aliugua ghafla. Wiki iliyopita, Jaji Bongole naye alifariki kwa matatizo ya kupumua. Huyu Jaji, vyanzo ndani ya familia vinasema alikua na dalili za corona kwa takribani wiki na alitambua hilo, sema alikua muumini sana wa kujifukuzia, na aliwaambia familia yake wafanye hivo pia.


Kama nilivosema mwanzoni ni vigumu kujua hali ya Corona nchini ikoje kwa sababu hamna takwimu na serikali yenyewe haijui pia maana hawafanyi testing kabisa. Balozi na mashirika ya kimataifa hapa nchini yote bado yanafanyia kazi nyumbani kwa kushauriwa na WHO kuwa hali haitabiriki. Serikali haitoi ushirikiano wowote ule kwa mashirika haya na imeamua kufocus kwenye campaign

Nawaombeni tuwe makini na tuendelee kuchukua tahadhari. Tuwe makini na kauli za wanasiasa, Corona bado ipo, jilinde wewe jirani yako na familia yako
 
Ukiwa underlying issues inaondoa faster. Nina hofu na mkutano mkuu,waliambukizana.
Hapo kuna utata sana,kuna watu walikuwepo katika ule mkutano wanajulikana kabisa afya zao si nzuri na hawakuwa hata na barakoa ni wazi tungetegemea kuona hali kuwa mbaya kutokana na record za Afya zao.
 
Ukifa tunakufukia futi 3 tu
Nadhani una tatizo mahali fulani akilini mwako. Unatutuuma kwenda ulizia habari za mareehemu ati nini kilimuua. Ili iweje?? Tena unasema Dr. John ana uwezo wa kupata matibabu ya hali ya juu. Huyo Mbwete uliambiwa alikuwa mnyonge? Huyo jdg uliambiwa alikosa pesa? Nitamwamini rais wangu 100% kuwa Korona kaondoka kama alivyokuja. Tuendelee na mambo yetu kama kawa. Nenda kaji lock down mwenyewe lakini sisi tutaendelea na yetu
 
Kufa wewe basi ili uwe mwakilishi
Yeye ni muhimu kwa Tanzania kuliko watu kama wewe milioni 1 bora watz wapuuzi kama wewe milioni moja mfe kuliko raisi magufuli
 
Mungu ni mkubwa
Wakuu huu ugonjwa upo na hata sasa uwezekano wa kuupata upo , huwezi kuukwepa kama unavyoambukizwa mafua, kuna wakati huwezi kujua umeyapatia wapi. Kwa maamuzi tuliyoyachukua ingekuwa ni ugonjwa unaoua moja kwa moja ukiupata basi watu wengi sana wangeteketea, unaua lakini si kila anayeupata lazima afe ama ahitaji hata kulazwa hospitali.

Kuna thread ya mdau mmoja nilijibu kama wiki 3, zilizopita niliumwa ugonjwa usioeleweka lakini ulikuwa na dalili zote za corona, kinachosaidia tu ni kutumia tiba asili kupunguza makali/maumivu na kujitenga na wenzako ili kukata mnyororo wa maambukizi, unasumbua kweli na kuna muda unaweza kukata tamaa lakini kama sio siku yako unavuka salama.
 
Wewe usiwatakie watu wapate maambukizi, wewe kama unaona imeisha fine. Waache wenzako wanaochukua tahadhali wafanye hivyo
MKUU mnyonge mnyongeni ila haki yake mpe bila kupepesa macho , binafsi nazunguka sana but mpaka sasa corona wenda imebaki kwa asilimia 15 tu na hapa namanisha kweli kabisa maana sijui unafiki,
so tz narudia kwa hili kupitia MAGHUFULI ,corona tumeikomesha na ikome kweli
 
Sahihi mkuu, za kuambiwa unachanganya na zako.
Usijidanganye mkuu,corona ipo. Wapi watu wa karibu kabisa wanaumwa corona. Wamepima na sasa wanaendelea kutumia dawa bila kusahau kusali. La msingi tumuombe Mungu atuepushe nalo jumla. Wanasiasa sio wa kuamini 100%. Take care yourself.
 
Back
Top Bottom