PreGE2025 Wasira akutana na Jaji Waryoba na Mzee Joseph Butiku, wateta

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Labda wamenisikiliza

Hakika mkuu
 
Maisha ni fumbo kuna kipindi Mzee wasira alikuwa na benz bovu kapauka ana Nokia 3310 aka kijeneza anawasha kwa kuunga nyaya nakwambia uwezi kunielewa nampa lift nilikuwa nakavitara kangu milango 3! Ila nikimwendea sasa nikamkumbusha lazima anipige ngumi!
 
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Stephen Wasira amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi waandamizi wastaafu wa Serikali.

Viongozi hao ambao amekutana nao leo June 4, 2025 jijini Dar es Salaam ni Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Waryoba pamoja na Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Mzee Joseph Butiku ambaye pia amewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikali.
Wa kushoto na wa kulia nawaelewa, nawaamini sana, Mungu awajalie miaka zaidi ya mia, ila huyo wa katikati mmmmmh,
Mungu nisamehe.
 
TumainiEl Pascal Mayalla hawa wazee wawili hawa wa Kigonda cha mwalimu Nyerere wameshaandaa watu Strong kwa ajili ya Taifa?
 
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Stephen Wasira amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi waandamizi wastaafu wa Serikali.

Viongozi hao ambao amekutana nao leo June 4, 2025 jijini Dar es Salaam ni Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Waryoba pamoja na Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Mzee Joseph Butiku ambaye pia amewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikali.
Wasirra hana Maamuzi wala ushawishi ndani ya ccm, anazidiwa kwa mbali sana na Steve Nyerere
 
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Stephen Wasira amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi waandamizi wastaafu wa Serikali.

Viongozi hao ambao amekutana nao leo June 4, 2025 jijini Dar es Salaam ni Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Waryoba pamoja na Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Mzee Joseph Butiku ambaye pia amewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikali.
Hao jamaa wawili wa pembeni ndo tumebaki nao wanaojua maana ya Tanzania. Na uzee wao wakipewa nchi( Warioba na Butiku) wataendesha vizuri sana. Mstaafu hasiyetaka kustaafu amebaki kuwa chawa tu.
 
....sikiliza mzee Wassira, hao wazee muda wowote wataitisha press na walaani kinachoendelea. Sasa basi, naomba uitishe kikao nao cha zuga ili tuwapumbaze na wasifanye kile tunachokitarajia kutoka kwao.

Alisikika mwanamke mmoja aliye laaniwa!
kah!
 
Amechanwa ukweli au walikua pamoja tangu mwanzo halafu akafeli ghafla!!?

Nahisi:-

"Ndugu yetu hatuwezi ingia kwenye uchaguzi Kwa katiba na Tune huru iliyopo,ukilazimisha kumpigania utazikwa kabla ya muda"

Au

"Sasa kazi tuliyotaka uifanye inatosha,umeonyesha kwamba umepigania uchaguzi lakini brake zimekata na wananchi wanadai reforms ,kwahiyo tulia kwanza Ili ionekane umeshindwa ili reforms zifanyike"

Nadharia ni nyingi mno!!?
 
Wazee wenye akili na hekima ndio wanaelekea mwisho,

Sasa hawa vijana wa kushika hizo Nafasi sasa!
wapo kina mwigulu, nape, january, makonda, ndejembi, mavunde, heri jamesi, kihongosi, ally happy, chalamila
 
Wasira mimi binafsi nimemuona ni mtu mwenye uroho wa madaraka mno huyu pamoja na Waitara ni kama mapacha. Wakiona wewe ndio mtoa vyeo watakukumbatia na kukupamba hata kama unafanya vibaya as long as wananufaika na mfumo .Kwa hiyo hapa sidhani kama Wasira anaweza fikisha maazimio ya kikao walicho kubaliana sehemu husika.
 
Ukipinga utekaji si mwenzao hawa wanywa damu za watu ccm,hapo awe makini sana mzee warioba akijipindua tu wanamkatisha pumzi.
 
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Stephen Wasira amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi waandamizi wastaafu wa Serikali.

Viongozi hao ambao amekutana nao leo June 4, 2025 jijini Dar es Salaam ni Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Waryoba pamoja na Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Mzee Joseph Butiku ambaye pia amewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikali.
Labda busara itapatikana kuhusu mwafaka wa kitaifa kuelekea uchaguzi mkuu...
 
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Stephen Wasira amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi waandamizi wastaafu wa Serikali.

Viongozi hao ambao amekutana nao leo June 4, 2025 jijini Dar es Salaam ni Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Waryoba pamoja na Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Mzee Joseph Butiku ambaye pia amewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikali.
Kanda maalum.
 
Kabla sijasoma mada: Wataambiwa wote ni wa mkoa mmoja.

Lakini hilo si hoja. Hoja ni maslahi ya nchi hii.

Ni dalili njema kuhusu ushauri aliotoa Warioba juu ya "Marekebisho kabla ya uchaguzi"? Bunge ndiyo linaelekea ukingoni sasa.

Inaweza pia kuwa dalili mbaya; kwamba "Gari Bovu" kaenda kutoa vitisho na msimamo wa Mwenyekiti wake, kwamba wazee waache kihelehele. Hili litamwondolea kila kitu alichowahi kuaminisha waTanzania kuwa anajali maslahi ya nchi hii; na hasa katika hatua yake ya kumalizia maisha. Nini anakipigania?
 
Hivi inawezekana kweli askari amlawiti mwandishi toka nchi jirani Kisha amshurutishe kumshikuru Samia?
Elewa maana yake ni nini.
Haya mambo tunayachukulia kijuujuu bila ya kuyapa tafakuri makini.

Huyo mtu anamfanyia kazi Samia, haifanyii kazi Tanzania.
 
Wa kushoto na wa kulia nawaelewa, nawaamini sana, Mungu awajalie miaka zaidi ya mia, ila huyo wa katikati mmmmmh,
Mungu nisamehe.
Ngoja nikupe matumaini juu yake.

Pamoja na mabovu yake yote wa miaka ya nyuma; Mungu kamjaalia fursa hii adimu sana katika uhai wake, tena mwisho mwisho. Kamweka kwenye nafasi ya kuliokoa taifa linaloangamia. Fursa hii kweli ataitupa?

Dalili tayari zimekwisha onekana katika siku za hivi karibuni. Ulimsikia akiropoka chochote wakati wa mkutano wao (CCM), hivi karibuni?
Umemsikia sauti yake baada ya yule padre kuponea chupuchupu?

Bila shaka na yeye akili zimemrudia kujuwa kuwa alichowekewa hapo kwenye nafasi hiyo ni kutumiwa tu kama kikaratasi cha chooni cha kufutia uchafu. Kuhalalisha na kutetea maovu.

Huyu mzee Mungu kampa nafasi ya kipekee kabisa kujijengea jina na historia ya kipekee katika taifa hili katika dakika za mwisho wa uhai wake.

Wewe 'mkuu 'Emmanuel Misalaba' ungejaaliwa fursa kama hiyo ungeacha kweli ipite hivi hivi?

Nitamsikitikia sana kama hataelewa jukumu kubwa alilopewa na Mungu juu ya nchi hii.
 
Elewa maana yake ni nini.
Haya mambo tunayachukulia kijuujuu bila ya kuyapa tafakuri makini.

Huyo mtu anamfanyia kazi Samia, haifanyii kazi Tanzania.
Buibui ya kuzuga kumbe lucifer
 
Back
Top Bottom