Wasira ataka WANA CCM wakutane, wasiingie mkenge wa maneno ya Mtandaoni

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
WhatsApp Image 2026-08-19 at 18.24.26.jpeg

WhatsApp Image 2026-08-19 at 18.24.23.jpeg
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Ndugu Stephen Wasira, amewataka wanachama wa CCM kukutana mara kwa mara katika vikao rasmi vya chama ili kujadili masuala muhimu na kuepuka kupotoswa na taarifa zisizo na ukweli zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Akizungumza leo tarehe 19 Agosti, 2026 Wilaya ya Ikungi mkoani Singida wakati wa kuanza ziara rasmi ya kikazi ya kukagua uhai wa chama, Wasira amesema vikao hivyo vinawapa wanachama fursa ya kupata taarifa sahihi na kuambizana ukweli.

"Wanachama wetu nchi nzima, kwa mujibu wa Katiba mna vikao vya wanachama. Mkutane muambizane. Siku hizi kwenye mitandao kuna uongo mwingi sana. Usipoangalia unaweza hata wewe kushirikishwa kusema uongo," amesema.

Amesisitiza kuwa ni muhimu wanachama kukutana na kujadili madai yanayosambaa, kisha kumtafuta mtu mwenye ujuzi awasaidie kuyafafanua.

"Kwa hiyo ni vizuri kukutana mkasema hili jambo limesemwa sana, maana yake ni nini? Mkamwita mtu anayejua akawasaidia kufafanua," ameeleza.

Makamu Mwenyekiti huyo amebainisha kuwa mikutano ya wanachama ni fursa muhimu ya kujadili masuala yanayoendelea nchini ili waweze kukitetea chama ipasavyo.

Kuhusu uhuru na umoja wa nchi, Wasira amesema CCM itaendelea kulinda urithi huo uliopatikana kwa kazi kubwa.

"Hii ndiyo CCM. Kazi ya kwanza tulipewa ni uhuru na tunalinda. Ya pili ni umoja na tunahakikisha unabaki. Yeyote anayetaka kuubomoa anabomoa msingi ambao hawezi. Anaweza kutikisa matawi lakini mizizi itabaki chini," amesema.

Ameongeza kuwa wapo wanaodai CCM haijatekeleza chochote tangu uhuru, jambo ambalo amelisema ni kinyume na ukweli.

"Wanasema hatujafanya chochote tangu uhuru. Lakini uhuru wa kusema ndio huo walionao. Mdomo una kazi mbili: kusema na kula. Mtu akisema hakuna chochote tangu uhuru, muache tu. Huyo ana matatizo anahitaji msaada," amehitimisha.
.
WhatsApp Image 2026-08-19 at 18.24.32.jpeg

WhatsApp Image 2026-08-19 at 18.25.10.jpeg

WhatsApp Image 2026-08-19 at 18.25.12.jpeg

WhatsApp Image 2026-08-19 at 18.24.38.jpeg
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira, amewataka wanachama wa CCM kukutana mara kwa mara katika vikao rasmi vya chama ili kujadili masuala muhimu na kuepuka kupotoswa na taarifa zisizo na ukweli zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Akizungumza leo tarehe 19 Agosti, 2026 Wilaya ya Ikungi mkoani Singida wakati wa kuanza ziara rasmi ya kikazi ya kukagua uhai wa chama, Wasira amesema vikao hivyo vinawapa wanachama fursa ya kupata taarifa sahihi na kuambizana ukweli.
"Wanachama wetu nchi nzima, kwa mujibu wa Katiba mna vikao vya wanachama. Mkutane muambizane. Siku hizi kwenye mitandao kuna uongo mwingi sana. Usipoangalia unaweza hata wewe kushirikishwa kusema uongo," amesema.

Amesisitiza kuwa ni muhimu wanachama kukutana na kujadili madai yanayosambaa, kisha kumtafuta mtu mwenye ujuzi awasaidie kuyafafanua.
"Kwa hiyo ni vizuri kukutana mkasema hili jambo limesemwa sana, maana yake ni nini? Mkamwita mtu anayejua akawasaidia kufafanua," ameeleza.

Makamu Mwenyekiti huyo amebainisha kuwa mikutano ya wanachama ni fursa muhimu ya kujadili masuala yanayoendelea nchini ili waweze kukitetea chama ipasavyo.

Kuhusu uhuru na umoja wa nchi, Wasira amesema CCM itaendelea kulinda urithi huo uliopatikana kwa kazi kubwa.

"Hii ndiyo CCM. Kazi ya kwanza tulipewa ni uhuru na tunalinda. Ya pili ni umoja na tunahakikisha unabaki. Yeyote anayetaka kuubomoa anabomoa msingi ambao hawezi. Anaweza kutikisa matawi lakini mizizi itabaki chini," amesema.
Ameongeza kuwa wapo wanaodai CCM haijatekeleza chochote tangu uhuru, jambo ambalo amelisema ni kinyume na ukweli.

"Wanasema hatujafanya chochote tangu uhuru. Lakini uhuru wa kusema ndio huo walionao. Mdomo una kazi mbili: kusema na kula. Mtu akisema hakuna chochote tangu uhuru, muache tu. Huyo ana matatizo anahitaji msaada," amehitimisha.
Hili ndio chama cha sias sasa!. Sio vyama vingine kama Chadema wanaofikiri kuropokaropoka na kutukana eti ndio kufanya siasa!
 
Wewe ndio unaropoka. Habari ya CCM umesharukia CHADEMA.
Sawa. Wacha niropoke. Ila nimekuwa naropoka tangu 2014 nilipojiunga JF. Na tangu kipindi hicho naropoka na CCM inashinda chaguzi za kuifanya itawale nchi hii. Wewe ambaye hauropoki umekisaidaje chama chako cha Chadema na Mwenyekiti wake Lissu ambaye anakunya kwenye ndoo jela mwaka na nusu sasa? Ahahahahaha!!!

Mhudumuuuuii!! Ongeza Konyagi kubwa hapa!! Ahahahahaha!!
 
CCM ya sasa inaishi na kupumua kwa msaada wa polisi. Bila ya polisi, ccm inajifia kifo cha mende.
 
Back
Top Bottom