Naona CCM wanaendelea kukazia kwamba vijana tulilipwa na NGO's kufanya maandamano mbona hawasemi walipora uchaguzi na kuuwa wenzetu 
------------
Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Stephen Wasira, amewataka vijana kutokubali kutumiwa kuhatarisha amani ya nchi kwa kivuli cha kudai haki zao.
Amesema kuna baadhi ya taasisi zisizo za kiserikali zinazowahonga vijana kwa fedha ili kuwashawishi kufanya vurugu, huku zikijificha nyuma ya madai ya kutetea haki.
Wasira amesema hayo leo, Jumatatu Desemba 1, 2025, katika mahafali ya 10 ya chuo hicho, Kampasi ya Zanzibar, yaliyofanyika Bububu, Wilaya ya Magharibi A, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Amesisitiza kuwa haki haiwezi kupatikana kwa kuvuruga amani ya nchi, badala yake kufanya hivyo kunaweza kusababisha watu kupoteza hata haki za msingi ikiwemo ya kuishi.
Wasira ameongeza kuwa vijana wanapaswa kulinda amani iliyopo ili waweze kupata haki wanazozitaka kwa njia sahihi.
"Nchi hii haina hati miliki ya mtu, ipo kwa ajili ya Watanzania wote, kwa maana hiyo kila mmoja ana wajibu wa kuitunza amani hiyo na vijana msikubali kutumika vibaya," amesema Wasira
Soma pia PostGE2025 - Wasira: Haki inadaiwa kwa amani na si kuchoma nchi
Chanzo: Mwananchi_official