Akizungumza kwenye mahojiano yaliyorushwa na Nijuze Julai 22, 2026, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wasira, amesema mchakato wa maridhiano ya kitaifa hauhusu CHADEMA pekee bali unalenga jamii nzima ya Watanzania na makundi mbalimbali
Ameongeza kuwa vyama vya siasa vikiwemo CCM na CHADEMA ni sehemu tu ya taifa na wala havina idadi inayofika hata nusu ya Watanzania wote milioni 60, hivyo kuna haja ya kushirikisha makundi yote ya kijamii ili kufikia maridhiano ya kudumu yatakayolinda umoja na uhai wa taifa.
"Sijui kama mimi naridhika kuwasemea CHADEMA. Lakini wao wanachosema, wanasema wao hawataki maridhiano na wanafikiri wao ndio tunataka kuridhiana nao. Sasa kupitia kwako niwaambie tu, sisi tunataka kuridhiana na jamii yote, na CHADEMA ni sehemu tu ya jamii, Kama sisi tulivyo sehemu ya jamii."