Frank Wanjiru
Platinum Member
- Apr 12, 2012
- 25,686
- 46,842
Mwanasiasa mkongwe ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Stephen Wasira, amesema kuwa katika siasa za ulimwengu hakuna njia za mkato za kuleta amani isipokuwa maridhiano na kuzungumza.
Katika mahojiano maalumu na TBC, Wasira amesema kuwa jambo hilo linatekelezwa na serikali kupitia mpango maalumu wa 4R ulionzishwa na Rais Samia Suluhu Hassan huku asisitiza kuwa maridhiano ni hatua muhimu ya kupata katiba mpya.
Aidha, ameongeza kuwa maridhiano yaliyofanyika kati ya Chama cha ACT Wazalendo na CCM yataleta manufaa makubwa nchini ikiwemo kuondoa tofauti za kisiasa pamoja na kuleta umoja na mshikamano.