The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira, amesema hali ya kisiasa nchini ni tulivu, ambako amemjibu mwanazuoni mmoja aliedai kuwa hali ya siasa ni mbaya.
Mkongwe huyo wa siasa nchini amesema mwanazuoni huyo anachanganya hali mbaya ya chama chake na Tanzania kwa ujumla. Huku akisisitiza kwamba siasa Tanzania ni 'stable.
Kiongozi huyonguli wa siasa ameyasema hayo wakati wa mahojiano maalum na BBC jana.
“Nimesikia mwanazuoni, sijui mwandishi wa habari, akisema hali ya siasa Tanzania ni mbaya sana. Nilimuelewa yeye kwa sababu ana chama chake, na hali ya chama chake ni mbaya sana," amesema.
Akijibu madai kuhusu vyombo vya dola kunyamazisha upinzani, Wasira amesema hana ushahidi juu ya vyombo hivyo kunyamazisha wakosoaji, ingawa matukio yaliyotokea nchini yanachunguzwa na Jeshi la Polisi.
Mojawapo ya matukio aliyoyataja Wasira ambayo Jeshi la Polisi linafanyia uchunguzi ni kujeruhiwa kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Dk. Charles Kitima, na kupotea kwa mwanaharakati Nyangali Mdude.
“Ukisema vyombo vya dola vinanyamazisha, napata tabu kukubaliana kwa sababu sina ushahidi wa vyombo hivyo kunyamazisha na kumnyamazisha nani? Maana wapinzani wa CCM wapo ndani ya vyama," amehoji.
"Hoja nyingine inayozungumzwa ni kuhusu Tundu Lissu, hakunyamazishwa na vyombo vya dola bali alijikoki mwenyewe,” amesema Wasira.
Kuhusu sakata la wanaharakati kuingia nchini kutokana na kesi ya Mwenyekiti wa Chadema, Lissu, Wasira amesema aliyewaponza wengine ni Martha Karua kwakuwa aliingia nchini na kwenda mahakamani akieleza kuwa alifika kwa kofia mbili.
“Moja, amekuja nchini kama muangalizi kama mwanasheria, wakili, na raia wa Afrika Mashariki. Hayo yote tulisema ni sawa, lakini akasema vilevile amekuja kama mwanasiasa wa Kenya mwenye chama chake kinachoitwa People's Liberation Party.
"Akasema palepale Kisutu kwamba kukamatwa kwa maana yake ni serikali inaiogopa CHADEMA, na akataka serikali imuachie Lissu bila masharti. Pia akisema kwamba CHADEMA iruhusiwe kugombea uchaguzi,” amesema Wasira.
Chanzo Nipashe